MWALIKO KWENYE MAKAMBI

Mtukutu wa Nyaigela

JF-Expert Member
Sep 4, 2018
6,554
11,097
Wooote mnakaribishwa kwenye makambi.
Huu ni msimu wa makambi kwa waumini wa kanisa la Waadventista wa Sabato.
Kwa mfano kuna makambi mtaa wa mabibo yanayoanza kesho. Kutakuwa na wachungaji wanne kwenye kambi hilo.
Kuna wataalam wa malezi ya watoto na vijana
Kutakuwa na mafundisho kwa wajane na Wagane
Kutakuwa na session kwa aijli ya mafundisho ya ndoa
Pia kutakuwa na masomo ya afya
Huu ni wakati unaweza ukampata mchungaji ukamuuliza maswali yoote ya kiroho yanayokutatiza
Namna ya kufika kwenye kambi: Kwa wale wanaotokea kigogo na kupita hiyo njia ya mburahati unaombwa ushuke kituo cha mafuta(shell) cha simba oil. hapo utaona makambi
Karibuni sana tujifunze Biblia
 
Samahani sana umenikumbusha nilikuwa na mtu wangu yupo kurasini SDA alikuwa anapenda sana makambi kuna siku kaniambia twende anagalau usikilize ata kidogo kumbe anaimba kwaya akani surprise
 
Hapana Dini yenye chuki na Dini nyingine kujiona wanastahili wenyewe.Sipendi kusikia chochote kutoka kwao.
N:B MUNGU ni Upendo
 
Muwafundishe wadada wa kazi kuomba ruhusa, kuaga kwenda kwenye hayo Makambi. Yaani dada kaamka J3 anajiandaa kwenda Makambi bila kutoa taarifa. Muwafundishe kuwaheshimu wakuu wao wa kazi. Wiki nzima anafunga nyumba anasepa kurudi saa 1 kasoro jioni, Makambi. Hakuna kuomba ruhusa, hakuna maelezo. Muwafunze na adabu za kazi huko. :confused::rolleyes:
 
Wooote mnakaribishwa kwenye makambi.
Huu ni msimu wa makambi kwa waumini wa kanisa la Waadventista wa Sabato.
Kwa mfano kuna makambi mtaa wa mabibo yanayoanza kesho. Kutakuwa na wachungaji wanne kwenye kambi hilo.
Kuna wataalam wa malezi ya watoto na vijana
Kutakuwa na mafundisho kwa wajane na Wagane
Kutakuwa na session kwa aijli ya mafundisho ya ndoa
Pia kutakuwa na masomo ya afya
Huu ni wakati unaweza ukampata mchungaji ukamuuliza maswali yoote ya kiroho yanayokutatiza
Namna ya kufika kwenye kambi: Kwa wale wanaotokea kigogo na kupita hiyo njia ya mburahati unaombwa ushuke kituo cha mafuta(shell) cha simba oil. hapo utaona makambi
Karibuni sana tujifunze Biblia
balikiweni mtu wa Baba
 
Muwafundishe wadada wa kazi kuomba ruhusa, kuaga kwenda kwenye hayo Makambi. Yaani dada kaamka J3 anajiandaa kwenda Makambi bila kutoa taarifa. Muwafundishe kuwaheshimu wakuu wao wa kazi. Wiki nzima anafunga nyumba anasepa kurudi saa 1 kasoro jioni, Makambi. Hakuna kuomba ruhusa, hakuna maelezo. Muwafunze na adabu za kazi huko. :confused::rolleyes:
Sawa mkuu. watafundishwa kutii mamlaka kwa bwana
 
Hapana Dini yenye chuki na Dini nyingine kujiona wanastahili wenyewe.Sipendi kusikia chochote kutoka kwao.
N:B MUNGU ni Upendo
Karibu ujifunze mkuu. Na kweli Mungu ni Upendo. Pole kwa aliyekukwaza.
Sisi tunaamini Mungu ana watu wake kila mahali, hata kwenye makanisa mengine, na hatuhukumu, kuhukumu ni kazi Mungu
 
Makambi faida yake ni kuleta umoja tu kati ya washiriki, zaidi ya hapo ni miradi ya upigaji kwa wachungaji, mchungaji anademand alale hotel ya 70000 per day wakati anashinikiza washiriki wakambike na mahema, ukimwambia yeye alale kwenye mahema anaruka mita 200....
Mbinguni mbali sana
 
Back
Top Bottom