Mwakyembe Arukiwa Na Wasomi

Yeye alikataa kwa sababu taratibu hazikufuatwa, lakini baadaye kama mnakumbuka Hosea ilibidi aende bungeni kuwa na mazungumzona spika na hapo aliwasilisha barua ya kuitaarifu ofisi ya spika juu ya suala hilo na baada ya hapo spika alitoa waraka kwa wabunge walio takiwa kuhojiwa.

Kwa mujibu wa kanuni za bunge mbunge hawezi kupingana na waraka uliotolewa na spika, kwa mh. mwakyembe ilibidi ahojiwe ktk mazingira hayo na si vinginevyo.
Hizi pumba.
Mbona juzi kwenye Kongamano pale chuo kikuu baado analalamika kuwa si haki wabunge kuhojiwa?.Sasa kanuni gani za bunge?
 
Hao wasomi kuna jambo hawataki kuwa wawazi, ishu hapa siyo kuhojiwa

Ishu hapa ni Mwakyembe kutamka kuwa JK nafaa

Mwakyembe akibanwa kwenye kona anasema atafumua yote ya richmond ambao kayabakiza

na kila mtu anajua aliloogopa kusema mwakyembe na kamati ni uhusika wa Jk kwenye richmond!

Leo same mwakyembe ansema JK nafaa, hajatulia huyu
 
Mapepe na masifa bila busara ndio sifa yake Mwaki

Anajidai anajua sheria angekataa kuhojiwa tungejua anamaanisha anachosema

Mwizi, opportunist, hana jipya...tofauti yake ni kwamba hakupata cheo akipata atakuwa even more worse..lol
 
Hao wasomi kuna jambo hawataki kuwa wawazi, ishu hapa siyo kuhojiwa
Ishu hapa ni Mwakyembe kutamka kuwa JK nafaa

Mwakyembe akibanwa kwenye kona anasema atafumua yote ya richmond ambao kayabakiza na kila mtu anajua aliloogopa kusema mwakyembe na kamati ni uhusika wa Jk kwenye richmond !
Leo same mwakyembe ansema JK nafaa, hajatulia huyu

Mwakyembe ni typical example ya usanii at its best - mtaji mkuu wa CCM katika kuzidi kuwapumbaza wadanganyika. Yaonekana usanii ndiyo sera pekee inayotekelezwa kikamilifu na serikali kwa baraka za hili zimwi CCM - toka mjumbe wa nyumba kumi, mbunge, waziri hadi mkuu wa kaya mwenyewe. Hapa ndipo nawachoka wote wanaojitokeza kulalamikia uongozi wa nchi na wakati huo huo kumsifia Jemadari Mkuu ! Wanadai Kiongozi wetu ni dhaifu lakini kila wanapopata kibano, pona yao ni kukimbilia kumpaka mafuta huyo huyo kiongozi dhaifu.
Usanii huzaa udhaifu, Udhaifu huzaa unafiki, Unafiki huzaa ulafi, Ulafi huzaa ulaghai na Ulaghai huzaa UFISADI ! Masikini Tanzania !

Gazeti la karamagi haliwezi kumchafua mtu makini kama mwakyembe hata mtoto mdogo anajua kati ya karamagi na dk nani zaidi.
 
Dk aliwaambia waweke mdahalo wa wazi na baada ya mdahalo wapite pale kariakoo kwa mguu mtaani waone kama hawata vuliwa na nguo za ndani......

Tena karamagi watachukua miwani kwanza.
 
Usanii huzaa udhaifu, Udhaifu huzaa unafiki, Unafiki huzaa ulafi, Ulafi huzaa ulaghai na Ulaghai huzaa UFISADI ! Masikini Tanzania

MHHHHH.VERY TRUE.
 
Mwakembe hawezi kushindana na vyombo vya dola!
Unafanya mchezo nini? Kamuulize Mramba na Grayson Mgonja (yule alie kuwa katibu mkuu wizara ya fedha!) .Hawa watakuwa na experience nzuri na mamlaka ya dola!
 
wasomi wasema: Dk. Mwakyembe ni mpotoshaji

mwandishi wetu

mbunge wa jimbo la kyela kupitia chama cha mapinduzi (ccm), dk. Harrison mwakyembe, ametajwa kuwa ni miongoni mwa watu wapotoshaji nchini huku akijificha kwa kofia ya kubobea katika taaluma ya sheria.

hali hiyo imebainishwa na watu mbalimbali hivi karibuni kufuatia kitendo chake cha kusalimu amri na kuhojiwa na taasisi ya kuzuia na kupamba na rushwa nchini (takukuru) kutokana na kashfa ya kupokea posho mara mbili kwa kazi moja.

dk. Mwakyembe pamoja na baadhi ya wabunge wa jamhuri ya muungano wa tanzania , akiwemo mbunge wa kishapu, mkoani shinyanga, fred mpendazoe ambaye naye awali aligoma kuhojiwa, hatimaye alikubali kuhojiwa na taasisi hiyo nyeti ya serikali.

baadhi ya wasomi ambao waliongea na mwandishi wetu kwa masharti ya kutotajwa majina yao gazetini walisema kuwa kusalimu amri kwa dk. Mwakyembe na mwenzake na hatimaye kuhojiwa na takukuru kumechukuliwa na baadhi ya watu kuwa ni hatua ya kiume na kukomaa kisiasa kwa wabunge hao ambayo ilikuwa ikitarajiwa na wengi nchini.

hata hivyo, baadhi yao wamemtaja msomi huyo wa sheria kuwa ni mpotoshaji kwani ameshindwa kuwa na msimamo katika mambo yake.

“awali alisema kuwa hawezi kuhojiwa kwa sakata la kupokea posho mara mbili kwa kazi moja kwa kuwa ana kinga ya kisheria, baadaye aliambiwa kuwa asipokubali angekamatwa na kuhojiwa kwa nguvu… anabadilika na kukubali, hii ina maana gani kama si upotoshaji,” alihoji mwanafunzi wa udaktari chuo kikuu cha tiba cha muhimbili, jijini dar es salaam.

alisema kuwa kujua sheria haina maana kuwa hawezi kufanya uhalifu, hivyo inavyoonekana ni kuwa alikuwa akifanya makusudi kuchukua posho mara mbili huku akijua kuwa kufanya hivyo ni kosa kisheria.

hata hivyo, daktari huyo mwanafunzi alisema kuwa kila shughuli anayofanya dk. Mwakyembe anakuwa na lengo fulani, kwani sakata la kampuni ya kufua umeme wa dharura ya richmond ambayo yeye alikuwa mwenyekiti wa kamati ya kuchunguza mkataba wake, anaona kama inampa kinga asisemwe.

hata hivyo, mwalimu mmoja wa chuo cha usimamizi wa fedha (ifm) cha jijini dar es salaam alisema kuwa, kukataa kuhojiwa kwa dk. Mwakyembe kumemuondolea heshima yake mbele ya umma.

” kama kuna rushwa mahakamani na polisi, basi wanaofanya makosa wakatae kukamatwa na polisi na wakatae kuhukumiwa na majaji?” alihoji msomi huyo na kuongeza kuwa huu ni upotoshaji mkubwa.

hata hivyo, baadhi ya watu wanashangaa kwanini alikubali kuhojiwa.

“ni kweli kuwa dk. Mwakyembe angeendelea kugoma kuhojiwa, mwisho wa siku angejikuta akivunjiwa heshima yake kwa kuhojiwa kwa nguvu na hatimaye kupelekwa mahakamani kwa kukataa amri halali ya taasisi hiyo iliyopewa meno na bunge lenyewe,” alisema mmoja wa watu waliohojiwa na mwandishi wetu.

akaongeza: “baada ya hapo ndipo ushujaa wake ungemtokea puani kwani aibu ya kuhojiwa isingelingana na aibu ya kupelekwa mahakamani na kuhukumiwa kwa kukaidi amri ya halali ya serikali, kosa ambalo mwenyewe analitambua kisheria.”

hata hivyo, kukubali kuhojiwa kwa dk. Mwakyembe ambaye aliapa kuwa asingehojiwa kamwe huku akidai kuwa kufanya hivyo ni kuwadhililisha wabunge, kumemwaibisha na heshima yake kuporomoka.

heshima yake imeshuka kwa vile anafahamika na mara kwa mara amekuwa akijitangaza kuwa ni mtu wa kanuni, hivyo swali hapa ni vipi alisimamia hoja ambayo asingeweza kuiendeleza.

wachunguzi wa mambo ya kisiasa wanasema kwamba, dk. Mwakyembe ni mwanasheria, tena aliyebobea katika nyanja hiyo, hivyo anategemewa kuwa kila anachokisema anakuwa ameshakitafakari mara kadhaa kwa kuangalia madhara na athari zake mbele ya umma.

aidha, wamesema kauli ya mbunge huyo kuwa hawezi kuhojiwa kwa kuwa kufanya hivyo ni kukiuka sheria bila shaka ameitoa kwenye vitabu, kwa maana hiyo inaonekana kuwa vitabu vyake vya sheria alivyovisoma vilimdanganya au alikosea kuvisoma na kumwelekeza kuwa hapaswi kuhojiwa.

mbunge huyo wa kyela, aliwahi kusema kuwa kuwahoji wabunge maana yake ni kukiuka sheria inayohusu kinga, madaraka na haki ya wabunge, bila shaka hoja hiyo ameijenga kupitia mtazamo wa kisheria zaidi.

si hivyo tu, dk. Mwakyembe alidai kuwa taratibu hazikufuatwa kwani aliitwa kutaka kuhojiwa kwa simu badala ya wito maalum wa barua.

dk. Mwakyembe hakuishia hapo, alizidi kusema kuwa hatua hiyo ilichukuliwa kwa nia ya kufunika kashfa ya mkataba tata wa kampuni ya kufua umeme ya richmond .

kimsingi ni kuwa, wito ni wito tu, uitwe kwa kukonywezwa, kuitwa kwa barua, kwa mdomo, kwa simu au kupitia barua pepe, unabaki kuwa wito, kwani kinachotazamwa hapa ni taarifa ya kukutaka ufike sehemu fulani.

hata hivyo, hatua ya kutakiwa kuhojiwa na kashfa ya mkataba wa kampuni ya richmond , ni mambo mawili tofauti ambayo kimsingi yasingestahili kuwekwa pamoja kama alivyojaribu kufanya dk. Mwakyembe.

hatimaye, sheria imechukua mkondo wake, dk. Mwakyembe kahojiwa, japo kwa shingo upande, lakini kuhojiwa ni kuhojiwa tu. Ingekuwa ni jambo la aibu kwa serikali kushindwa kumchukulia hatua mvunjifu wa sheria.

hata hivyo, kitendo cha dk. Mwakyembe kugeuka jiwe na kukubali kuhojiwa, kinaweza kuwashangaza wengi waliomuona mbunge huyo ni shujaa kutokana na hoja zake za kupinga asihojiwe huku akisema kuwa hatua hiyo ilikuwa na ajenda ya siri.

baada ya kuhojiwa sasa dk. Mwakyembe ameibuka kwenye gazeti moja la kiingereza na kutangaza kuwa alikubali kuhojiwa baada ya takukuru kubadilisha taratibu za mahojiano ambayo awali yalikuwa yakienda kinyume na katiba na sheria za nchi.

wakati dk. Mwakyembe anasema hivyo, mpendazoe yeye akasema kuwa hayakuwa mahojiano, bali yalikuwa mazungumzo tu. Ni mazungumzo gani hayo na takukuru?

hayo ni mambo ya kushangaza ambayo hayapaswi kujirudia kwa wabunge wetu, kwani wanapaswa kuwa mfano wa tabia na mwenendo mzuri unaozingatia weledi na si kukurupuka na kutoa matamshi mazito na yenye utata ambayo baadaye wanakuja kuyajutia.

hili la matamshi mazuri yenye kufurahisha watu linamkumba pia spika wa bunge samwel sitta, ambaye aliwahi kujitokeza na kuwakingia kifua wabunge kuwa kuwahoji ni kuwadhalilisha, wakati yeye ndiye aliyetaka waheshimiwa hao wahojiwe.

hii ina maana kuwa spika sitta hakuwa mkweli, aliwahadaa wabunge huku akijua kuwa yeye ndiye aliwasha moto huo bungeni baada ya kutakiwa kufanya hivyo na viongozi wa serikali.

tuhuma za wabunge kuwa wanapokea posho mara mbili kwa kazi moja zilifikishwa takukuru na ofisi ya bunge la jamhuri ya tanzania aprili 26, mwaka huu.

kufuatia hali hiyo, waziri mkuu mizengo pinda alikaririwa akisema kuwa wabunge wanapaswa kuhojiwa kwani agizo hilo linatoka katika ofisi ya rais na si kwingineko.

hata hivyo, kila jambo halikosi mtibuaji, kwani suala hilo lilikuja kutibuliwa na spika mwenyewe aliposema kuwa watu wanawaonea wivu wabunge ambapo aliwataka wajiandae kuingia katika ulingo wa siasa na kugombea ubunge mwakani.

hata hivyo, spika sitta alisema kuwa wabunge wataendelea kupokea fedha hizo mara mbili kwa kuwa ni takrima.

wabunge waliokwishahojiwa na kamati hiyo hadi sasa ni pamoja na james lembeli (kahama), chrisant mzindakaya (kwela), fred mpendazoe (kishapu), aloyce kimaro (vunjo) na anthony diallo (ilemela).

hakuna sababu hata moja ya watanzania kujichanganya kwani takukuru imekusudia kutekeleza wajibu wake na hakuna aliye juu ya sheria.

hata hivyo, sheria na kanuni za malipo ya posho zinasema mtumishi, mtu au asasi haiwezi kulipwa zaidi ya mara moja kwa ajili ya kazi hiyo hiyo.

sasa hawa wabunge wanalipwa posho za kujikimu (subsistence allowance) na ofisi za bunge, lakini wakienda kwenye taasisi au mashirika ya umma au serikali za mitaa wanalipwa tena posho za kujikimu kwa shughuli hiyo hiyo ambayo bunge imeshawalipa.

inaelezwa kwamba, wabunge wanapotembelea asasi, taasisi na mashirika ya umma anapaswa kupewa chakula, maji ya kunywa, vinywaji baridi au baada ya kikao kufanyiwa hafla.

mchambuzi mmoja wa masuala ya kisiasa nchini aliwahi kusema kuwa watanzania kila tunapotaka kufanya suala la maendeleo, huwa kuna urasimu unatokea, hivyo hadi unapokamilisha taratibu zake kunakuwa hakuna maana tena.

dk. Mwakyembe alikataa kuhojiwa na takukuru kama baadhi ya wabuge wengine walivyohojiwa na taasisi hiyo kwa madai kuwa hizo ni mbinu za kutaka kuwaziba midomo wabunge.

katika mahojiano yake na vyombo vya habari hivi karibuni dk. Mwakyembe alikaririwa akisema kuwa, takukuru inawapigia simu wabunge mmoja mmoja na kuwahoji kwa takriban zaidi ya saa tatu.

alisema kuwa hilo ni kosa na ni kinyume cha sheria kwani mahojiano hayo hayawekwi kwenye maandishi.

chanzo: taifa tanzania, desemba 18, 2009
nimeinasa kwenye mtandao wa kwanzajamii.com

hii ni kazi ya mafisadi wa kiiran
 
Dk aliwaambia waweke mdahalo wa wazi na baada ya mdahalo wapite pale kariakoo kwa mguu mtaani waone kama hawata vuliwa na nguo za ndani.......

Unapoona msomi wa ngazi ya uzamivu katika masuala ya sheria anapigia debe "mahakama za mitaani" ama MOB JUSTICE ni lazima ujiulize mara mbilimbli tunakoelekea....

Nakumbuka wakati nipo mlimani mwaka wa kwanza nikisome shahada ya sayansi ya siasa nilikuwa mhudhuriaji mzuri wa mihadhara ya Dr Mwakyembe katika kitivo cha sheria. Ukitoa mbwembwe na tuhuma za unyanyasaji wa baadhi ya wanafunzi zikihusishwa na mapungufu ya kijamii alikuwa mwalimu mzuri sana aliyekuwa akijua nini anafundisha. nilihakikisha kuwa nahudhuria darasa lake hata kama haikuwa kozi niliyojiandikisha na mengi nilisoma kuhusiana na CRIMINAL LAWS.

Hata hivyo sisahau siku ile alipokuwa katika kipindi kimoja cha luninga akiwa pamoja na Marehemu Prof Haroub Othman na Kipanga mwengine wa kitivo cha sheria Prof Palamaganda Kabudi kuhusiana na mauaji ya wazanzibari ya mwezi Januari 2001. Kwa wazi, kejeli, majivuno, chuki na furaha yake ya kuona damu ya wazanzibari ikimwagika.Kwa kweli sitasahau siku ile na mara baada ya hapo akazawadiwa ubunge wa Afrika Mashariki.

Hayo na mengine mengi aliyokuwa akiyafanya wakati wa kampeni ya 2005 ambayo yalimfanya hata JK na mtandao kuapa kutompa nafasi ya uwaziri aliyokuwa akiiamini kuwa anapaswa kuwa nayo kutokana na usomi wake yamenifanye niwe na mtazamo wa kuwa Mwakyembe ni LEARNED POLITICAL MERCINARY period....Ni hatari zaidi ya kina Charles Charles na wenziwe.

Ingawa yeye ni msomi mkubwa amekuwa akifanya siasa zisizo tofauti na MEDIOCRES waliojaa humo bungeni. Inashangaza kuona kuwa kwa usomi wake na exposure aliyonayo bado ameamua kutumikia ajenda moja tu ya RICHMOND katika miaka mitatu yote sasa. Wakati ana uwezo wa kuibua, kujenga na kufanikisha ajenda nyingi kubwa na zenye kuhitajika zaidi kwa mustakabali wa nchi yetu zaidi ya hii HOMA YA LOWASSA NA ROSTAM. Tanzania ni zaidi ya uvundo wa kina ROSTAM, LOWASSA, RICHMOND, DOWANS na katika watu wanaopaswa kulitambua hilo Mwakyembe ni mmoja wapo. Inachosha kusikia neno moja tu RICHMOND kutoka kinyani kwa Msomi wa Level yake ambaye tunategemea mengi makubwa kutoka kwake.

Akiwa kama msomi Mwakyembe anapaswa kubadilika na kuwa zaidi ya hizi petty politics zenye kulenga nguvu za kisiasa tu kuliko maslahi makubwa ya taifa letu linaloelekea kuzama. Msomi mkubwa kama Mwakyembe anapaswa kujipembua kutoka katika hii kansa ya petty, emotional and politics of the belly, ili kuonyesha tija ya kuwa na wasomi katika siasa. Akiendelea na style yake ya sasa ni wazi atakuwa anawasaidia madui wa USOMI katika siasa na hivyo kuendeleza MEDIOCRE POLITICS....

Mwakyembe ni aibu kwa wasomi kama alivyo HARVARD BOY Andrew Chenge....NI wazi kuwa Mwakyembe hajaweza kujikusanyia VIJISENTI sio kwa sababu anaamini katika principles and values lakini he is waiting and scheming for HIS TURN TO EAT....

omarilyas
 
Dk aliwaambia waweke mdahalo wa wazi na baada ya mdahalo wapite pale kariakoo kwa mguu mtaani waone kama hawata vuliwa na nguo za ndani......

Tena karamagi watachukua miwani kwanza.
.

Ndugu Magezi.
Kweli unajua kuandika pumba.na nafikiri wewe ni pumba pia.
 
Mkuu Omarilyas,

1.Akikusikia MASANILO na MWAAFRIKA kuhusu hii post yako,nafikiri mtapigana ngumi.

2.Wao ni Maswahiba wa Mwakyembe na wameamua kwa pamoja kuwa yeye ni kiongozi bora.Ata akiongea pumba,basi zidumu!.

3.MASANILO yeye amesema atashuka na magari mawili ya kampeni,moja limeandikwa MZEE MWANAKIJIJI na lingine limeandikwa INVISIBLE.

4.MASANILO yeye amesema ,ni lazima mwakyembe arudi bungeni mwakani na anajiandaa kwenda kyela kuongeza nguvu na magari yake hayo mawili.

5.MWAAFRIKA naye amesema atakwenda kumpa tafu swahiba wake huyo msanii.Sikonge naye amesema atakwenda , duh . Kweli kyela kutakuwa na mpambano mkali sana mwakani.

5.Na mimi nikipata nauli ya kunitoa Mwanza nitakwenda.
 
Back
Top Bottom