TIMING
JF-Expert Member
- Apr 12, 2008
- 24,892
- 11,289
Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe
Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, amegeuka mbogo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza eneo la Kivukoni jijini Dar es Salaam na kuelezwa asilimia kubwa ya mapato yanayopatikana yanatumika kuendesha kivuko hicho.
Dk. Mwakyembe aligeuka mbogo baada ya Mkuu wa Kivuko cha Kigamboni, Mhandisi John Gama, kueleza kwamba mapato ya kivuko hicho kwa mwezi ni Sh 221,173,230 wakati matumizi ni wastani wa Sh. 223,314,481 kwa kipindi hicho.
Gama alieleza pia kwamba gharama kubwa ni ununuzi wa mafuta ambayo ni Sh. Milioni 102 kwa mwezi.
Taarifa hiyo ilimfanya Naibu Waziri huyo kuonyesha kutoridhishwa na hali ya mapato na matumizi na kueleza kwamba idadi ya watu na magari ambayo yanatumia vivuko kila siku hailingani
SOURCE: NIPASHE
Ushauri kwako Harry...
anza na temesa leadership... wanalea ana hao suprvisors, umeondoka huku watu wanamega kisela:tape: