Mwakyembe aelezea suala la mabehewa feki, ajibu yaliyoandikwa Nipashe

Mwakyembe sio mgeni kwenye mambo ya kashfa, ni janja-janja nyingine inayotumia elimu na siasa kupata opportunities, alinguruma sana wakati wa sakata la Richmond kumbe na yeye alikua na kampuni ya umeme, kila aendapo lazma hukumbana au hukumbwa na vurugu, complaints and the like... hii kitu siyo coincidence, KUNA KITU!!

Na siku zote huwa mjanja sana wa kusingizia UCHAGUZI ETC.

Kama sikosei, huyu jamaa pia alishawahi kutolewa kwenye magazeti over 10 years ago akiwa kabanwa na watemi aliwaingilia mboga yao

Anyway, sidhani kama atashinda ubunge mwaka huu... he has to be careful, maana akishindwa basi yatafumuka mengi na hataamini kitakachomkuta
 
Hii Taarifa haikupaswa kutolewa na Wizara ya Afrika mashariki

Ilipaswa kutolewa na Mwakyembe in Person

Haya ni matumizi mabaya ya Ofisi ya Umma

Tuhuma zimeelekezwa kwake personaly

Hakupaswa hata kutumia heading ya Wizara ya Afrika mashariki

Hupaswi kutumia ofisi ya Umma kujitetea kwa mambo yako binafsi mfano Ubadhirifu wako

Hapa patamu. Hebu tupe, japo kwa mukhtasari, ubadhirifu wake.
 
Mwakembe ni mnafiki sana huyu na sita kama mapacha wezi halafu wanajiita wazalendo uzuri unafiki haujifichi wacha mzimu wa unafiki wake umtafune akome kabisa
 
hujaelewa kitu

hizo kashfa zote hazijatolewa kwa wizara

ni za kwake binafsi

wizara hazijatuhumiwa hapo...ni mwakyembe...si sawa kutumia jina la wizara kujitetea binafsi

hoja za wapambe wa lowassa wanaodai damu ya mwakyembe kwa udi na uvumba zinaonekana! Hapa wanalazimisha richmond no.2 itokee. Kwa jinsi tunavyomjua mwakyembe, mtahangaika sana bila mafanikio. Bwana freeland hapo anasubiri mshiko wa mamvi, atamg'ang'ania mwakyembe wee bila hoja!
 
Mwakyembe sio mgeni kwenye mambo ya kashfa, ni janja-janja nyingine inayotumia elimu na siasa kupata opportunities, alinguruma sana wakati wa sakata la Richmond kumbe na yeye alikua na kampuni ya umeme, kila aendapo lazma hukumbana au hukumbwa na vurugu, complaints and the like... hii kitu siyo coincidence, KUNA KITU!!

Friends of Lowassa wanazoza! Zoza mwanangu zoza, kuna mshiko!

Na siku zote huwa mjanja sana wa kusingizia UCHAGUZI ETC.

Kama sikosei, huyu jamaa pia alishawahi kutolewa kwenye magazeti over 10 years ago akiwa kabanwa na watemi aliwaingilia mboga yao

Anyway, sidhani kama atashinda ubunge mwaka huu... he has to be careful, maana akishindwa basi yatafumuka mengi na hataamini kitakachomkuta
Friends of Lowassa wanazoza! Zoza mwanangu zoza, kuna mshiko!
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
WIZARA YA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI
HABARI YA UPOTOSHWAJI ILIYOANDIKWA NA GAZETI LA NIPASHE KUNIHUSISHA NA KASHFA YA MABEHEWA FEKI YA TRL

JOTO la uchaguzi mkuu limezidi kupanda baada ya Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Harrison Mwakyembe kusema tuhuma zinazotolewa dhidi yake ni porojo na uzushi kuelekea kipindi hiki cha uchaguzi. Mwakyembe alisema baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikiandika kuhusu mabehewa ya TRL na kumhusisha yeye wakati alikwisha agiza hatua za kuchukuliwa kwa wahusika tangu waziri wa uchukuzi.

Imeandika habari yenye kichwa cha habari “Mwakyembe atajwa Kashfa ya TRL”. Napenda kutoa ufafanuzi kuwa habari hiyo iliyoandikwa ni uzushi mtupu wa kutaka kunichafua. Nachelea kusema habari hii ni uzushi na porojo za kisiasa haswa katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kwa kunihusisha kwenye mchakato wa zabuni ya TRL ambao Waziri hana mamlaka nao kikanuni na kisheria.

Kama Waziri mwenye dhamana na Wizara baada ya kupokea malalamiko kuhusu mabehewa yaliyonunuliwa na TRL kutokuwa na viwango vinavyokubalika, nilichukua hatua za awali za kuunda tume ambayo ilanza mara moja kuchunguza suala hili ili kujiridhisha na kutafuta ukweli wa jambo hilo. Baada ya kupokea taarifa ya awali ya uchunguzi uliofanywa na tume hiyo, nilichukua uamuzi wa kuiagiza Bodi ya Wakurugenzi ya TRL kuivunja Bodi ya Zabuni.

Baada ya bodi hiyo zabuni kuvunjwa, niliagiza Bodi ya Wakurugenzi ya TRL iwasimamishe kazi maafisa waandamizi wote wa TRL waliohusika katika mchakato wa manunuzi wa mabehewa hayo ili kupisha uchunguzi uliokuwa ukiendelea kufanywa na tume. Aidha, niliiagiza Wizara na Bodi ya Wakurugenzi ya TRL kuiomba Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)ifanye uchunguzi wa kina wa mkasa mzima, kazi ambayo nafahamu inaendelea kufanyika hadi sasa.

Kwa msingi huo habari iliyoandikwa kwenye gazeti hilo (NIPASHE) vyombo hivyo (si hili) ya kunihusisha na kashfa ya sakata hilo imenishtua na kunishangaza kwa kuwa kama ningekuwa nahusika kwa namna moja au nyingine nisingeweza kuchukua hatua nilizozieleza hapo juu. Gazeti la NIPASHE pia limehusisha suala la mabadiliko ya Baraza la Mawaziri yalyofanywa na Mhe. Rais, ambayo mimi nimehamishiwa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwamba ni kwa sababu ya kuniepusha na kadhia ya kashfa hiyo ya ununuzi wa mabehewa feki.

Hilo ni jambo la kushangaza na uelewa mdogo wa mwandishi wa kutoelewa namna Serikali inavyofanya kazi. Uamuzi wa kunihamisha Wizara umefanywa na Rais kwa sababu tofauti kabisa na hizo za kusadikika zilizoandikwa na gazeti la NIPASHE. Kama Rais aliona nina dosari, hakuwa na sababu kabisa kuniteua kumsaidia kuendesha Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) katika kipindi hiki ambacho nchi yetu imepata fursa ya kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya. Hivi karibuni Mhe.

Waziri Mkuu, alifanya ziara katika Mkoa wa Mbeya na wakati akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Kyela, Waziri Mkuu alitoa ufanunuzi mzuri wa uamuzi uliochukuliwa na Mhe. Rais wa kuniamisha kutoka Wizara ya Uchukuzi kwenda Wizara ya Ushirikano wa Afrika Mashariki, maelezo ambayo sina haja ya kurudia kuyaeleza kwa sababu yalishatolewa kwenye vyombo vya habari.

Nimalizie kwa kusema kuwa Watanzania tuamke kwani hakuna dosari yoyote ya mimi kuhamishiwa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Kupelekwa kwangu Afrika ya Mashariki ambako nilianzia Ubunge, ni mkakati mzuri tu wenye tija. Wenye nia njema na nchi yetu wataafiki”. Naomba ifahamike kwamba sehemu kubwa ya nguvu ya fedha ya washiriki wetu wa maendeleo sasa inapitia kwenye Jumuiya za kanda kama Jumuiya ya Afrika Mashariki ambayo kwa sasa Mhe. Rais ni Mwenyekiti wa Marais wa Jumuiya na mimi ni Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri.

Hivi sasa niko njiani natokea Marekani ambako niliongoza ujumbe mkubwa wa Mawaziri wan nchi tano (5) za Jumuiya ya Afrika Mashariki kujadiliana na Serikali ya Marekani, pamoja na mambo mengine, kuongeza muda wa sheria inayozipa fursa nchi za EAC kupeleka bidhaa za biashara Marekani bila ushuru (AGOA).

Dkt. Harrison G. Mwakyembe (Mb)

WAZIRI WA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI

9 Machi, 2015

Angemjibu rafiki yake wa zamani bwana Sita ndiyo anayemshughulikia.... Hayo yote anayosema mbona ni uwongo, hakuna kitu kama hicho kinachoendelea ndani ya TRL...
 
kiutawala mwakyembe hajaonyesha maana ya kuwa na phd ya sheria.tuhuma si kwa wizara bali ni yeye kutokuwajibika na kuwa mbadhrifu.haya si mambo ya wizara kumjibia mwakyembe ,bali yeye mwenyewe.huko ndo kuwajibika (accountability).
kutumia kinga ya wizara kuzungumza na jamii au umma kwa kutumia wizara kimsingi haya matumizi mabaya ya madaraka.
hata kama kahamishiwa wizara hiyo ku uzembe au ubadhirifu,mwenye wajibu wakumsemea si yeye baki ni mamlaka yake ya uteuzi nayo nayo ni rais.
yeye ajibu kama yeye na si wizara kumjibia kisa anafanya wizara hiyo.
Ukisoma taarifa hii unagundua kama Tanzania kuna wababe...na huyu anayetuhumiwa ni mmoja wao maana anatumia wizara kama ndiye yeye mwenyewe maana taarifa hii haioneshi kuandikwa na mtu mwingine ila yeye mwenyewe...ndiyo maana anatumia maneno sasa hivi nimetoka badala ya msemaji wa wizara kusema kwa sasa hivi waziri ametoka ...kwa hiyo ni matumizi mabaya ya ofisi nakubaliana na mlalamikaji mmoja humu jamii forum. Tuzoea kujua mambo yetu na ya kazi yawe ya kazi kweli maana kama yupo msemaji wa wizara aachiwe kazi hiyo hata kama atapewa maelekezo toka kwa huyo aliyeamua kujisemea
 
nchi hii suala la uwajibikaji limekuwa gumu sana, mtu ndiye una kauli ya mwisho kwenye wizara unajivua vipi lawama mambo yanapoharibika? Mbona yakiwa mazuri mnajichukulia sifa nzuri za utendaji!!

Mshikaji soma vizuri hoja ya Mwakyembe! Hapa ni sheria ya manunuzi yenye vyombo vyake mahsusi vya uwajibikaji. Kama Mwakyembe angeingilia mchakato huo kama alivyofanya Lowassa kwenye Richmond basi angewajibika. Hapa ni hoja tu si hisia na kwikwi za inda na visasi.
 
Mwakyembe sio mgeni kwenye mambo ya kashfa, ni janja-janja nyingine inayotumia elimu na siasa kupata opportunities, alinguruma sana wakati wa sakata la Richmond kumbe na yeye alikua na kampuni ya umeme, kila aendapo lazma hukumbana au hukumbwa na vurugu, complaints and the like... hii kitu siyo coincidence, KUNA kitu
Na siku zote huwa mjanja sana wa kusingizia UCHAGUZI ETC.

Kama sikosei, huyu jamaa pia alishawahi kutolewa kwenye magazeti over 10 years ago akiwa kabanwa na watemi aliwaingilia mboga yao

Anyway, sidhani kama atashinda ubunge mwaka huu... he has to be careful, maana akishindwa basi yatafumuka mengi na hataamini kitakachomkuta[/QUOTE

Brother au sister, nakuhakikishia kuwa jamaa huyu Mwakyembe atashinda ubunge kwa kishindo kwa kuwa nyie akina Mwangumhulu, Mwakalyelye, Mwamasuku, Mwakipesile nk wa Kyela mnadhani kumshinda Mwakyembe ni kumshambulia kwa jazba kwenye JamiiForums. Nendeni Kyela, changieni maendeleo badala ya michango hii ya kichizichizi!
 
Binafsi simkubali kabisa Mwakyembe kwa kuwa ni mnafiki
sana. Ni mwanaCCM mjanjamjanja, Opportunistic, mpenda sifa za haraka haraka nk.

KASORO ZA TAMKO LAKE:
1/Hoja inamgusa yeye lakini anatumia wizara Afrika Mashariki kujibu why? Tena anatoa tamko akiwa safarini(nje ya wizara) ikiashiria muhusika ni yeye mwenyewe na watendaji wa wizara hawajahusishwa kabisa. Haya ndio matumizi mabaya ya madaraka.

2/Mwakyembe anadai hahusiki na utaratibu wa Zabuni za TRL halafu hapo hapo anasema aliunda Tume kuchunguza zabuni hiyo!! Anakataa nini na anakubali nini?

3/Hata kama ni kweli labda alikuwa na dhamira njema ya kuunda tume, kwanini hakusimamisha kwanza viongozi wakuu wa TRL ili kupisha uchunguzi?
Mbona mpaka leo hiyo report ya tume haijaletwa hadharani?

4/Rais Kikwete ndio aliyemhamisha kutoka Uchukuzi kuja EAC, iweje Pinda ndio atolee ufafanuzi wa uteuzi wake? Pinda ana ubia na Kikwete kwenye kiti cha urais? Toka lini serikali au rais Kikwete amekuwa na utaratibu wa kutoa sababu binafsi za uteuzi wake?

5/Kwanini Kikwete amwone Mwakyembe anafaa sasa kuwa EAC na sio wakati ule 2010 anamteua? Anataka kusema Sitta alishindwa au angeshindwa kuimudu EAC ndio maana akapelekwa yeye?

Mimi naamini kabisa kwa hili Mwakyembe anahusika 100% na kuunda tume ilikuwa ni kunawa mikono ili asihusishwe au kulizika kinyemela hili suala. Otherwise utuambie nani ni mhusika mkuu wa hii zabuni au alitolewa
Pale ili wahusika walindwe.
 
Mwakembe ni mnafiki sana huyu na sita kama mapacha wezi halafu wanajiita wazalendo uzuri unafiki haujifichi wacha mzimu wa unafiki wake umtafune akome kabisa

Mwakyembe amechanganyikiwa Kyela hawataki hata kumuona. Hajafanya chochote Kyela mwisho wake kisiasa umefika
 
Mwakyembe sio mgeni kwenye mambo ya kashfa, ni janja-janja nyingine inayotumia elimu na siasa kupata opportunities, alinguruma sana wakati wa sakata la Richmond kumbe na yeye alikua na kampuni ya umeme, kila aendapo lazma hukumbana au hukumbwa na vurugu, complaints and the like... hii kitu siyo coincidence, KUNA kitu
Na siku zote huwa mjanja sana wa kusingizia UCHAGUZI ETC.

Kama sikosei, huyu jamaa pia alishawahi kutolewa kwenye magazeti over 10 years ago akiwa kabanwa na watemi aliwaingilia mboga yao

Anyway, sidhani kama atashinda ubunge mwaka huu... he has to be careful, maana akishindwa basi yatafumuka mengi na hataamini kitakachomkuta[/QUOTE

Brother au sister, nakuhakikishia kuwa jamaa huyu Mwakyembe atashinda ubunge kwa kishindo kwa kuwa nyie akina Mwangumhulu, Mwakalyelye, Mwamasuku, Mwakipesile nk wa Kyela mnadhani kumshinda Mwakyembe ni kumshambulia kwa jazba kwenye JamiiForums. Nendeni Kyela, changieni maendeleo badala ya michango hii ya kichizichizi!

teh teh teh teh... chadema wanachukua jimbo

tunajua wafuasi wake mtakuja kama siafu... karibuni
 
Binafsi simkubali kabisa Mwakyembe kwa kuwa ni mnafiki
sana. Ni mwanaCCM mjanjamjanja, Opportunistic, mpenda sifa za haraka haraka nk.

KASORO ZA TAMKO LAKE:
1/Hoja inamgusa yeye binafsi lakini anatumia wizara Afrika Mashariki kujibu why? Haya ndio matumizi mabaya ya madaraka.

2/Mwakyembe anadai hahusiki na utaratibu wa Zabuni za TRL halafu hapo hapo anasema aliunda Tume kuchunguza zabuni hiyo!! Anakataa nini na anakubali nini?

3/Hata kama ni kweli labda alikuwa na dhamira njema ya kuunda tume, kwanini hakusimamisha kwanza viongozi wakuu wa TRL ili kupisha uchunguzi?
Mbona mpaka leo hiyo report ya tume haijaletwa hadharani?

4/Rais Kikwete ndio aliyemhamisha kutoka Uchukuzi kuja EAC, iweje Pinda ndio atolee ufafanuzi wa uteuzi wake? Pinda ana ubia na Kikwete kwenye kiti cha urais? Toka lini serikali au rais Kikwete amekuwa na utaratibu wa kutoa sababu binafsi za uteuzi wake?

5/Kwanini Kikwete amwone Mwakyembe anafaa sasa kuwa EAC na sio wakati ule 2010 anamteua? Anataka kusema Sitta alishindwa au angeshindwa kuimudu EAC ndio maana akapelekwa yeye?

Mimi naamini kabisa kwa hili Mwakyembe anahusika 100% na kuunda tume ilikuwa ni kunawa mikono ili asihusishwe au kulizika kinyemela hili suala. Otherwise utuambie nani ni mhusika mkuu wa hii zabuni au alitolewa
Pale ili wahusika walindwe.
nenda kafyonze urojo huwezi jua umuhimu wa mwakyembe EAC mpaka kwanza ujue ame-specialize kwenye nini! hii topic ni kubwa sana kwako..
 
nenda kafyonze urojo huwezi jua umuhimu wa mwakyembe EAC mpaka kwanza ujue ame-specialize kwenye nini! hii topic ni kubwa sana kwako..

Geza Ulole usitake kujifanya unawajua wakati hujui chochote. Ni vizuri ukajibu hoja za msingi kuliko kubwabwaja hapa JF.

Mwakyembe ni Mwanasheria kitaaluma na alituma muda wake mwingi akiwa Lecturer. Nimemfahamu muda mrefu hata kabla hajaingia kwenye mikiki ya kisiasa kipindi hicho nikiwa naye UDSM wakati
anafundisha.

Dr.Mwakyembe hana role yoyote ya maana EAC kwa kuwa hakuna utaalamu wowote wa maana unaohitajika ili kuongoza wizara hiyo zaidi ya kutalii na kupiga blah blah tu. Ni moja wizara mpya, ndogo na changa sana. Ilipaswa kuwa ni Idara tu ndani ya wizara mama ya Mambo ya nje.
 
Last edited by a moderator:
Huko ndio alikotoa pesa za kununua kiwanja cha bilioni moja kule Bahari beach.

Adhabu ni hapa hapa duniani, kumwonea Lowassa yanamkuta na yeye.

Nimeambiwa hata kule kwao hawamtaki tena, ubunge bye bye.
 
Geza Ulole usitake kujifanya unawajua wakati hujui chochote. Ni vizuri ukajibu hoja za msingi kuliko kubwabwaja hapa JF.

Mwakyembe ni Mwanasheria kitaaluma na alituma muda wake mwingi akiwa Lecturer. Nimemfahamu muda mrefu hata kabla hajaingia kwenye mikiki ya kisiasa kipindi hicho nikiwa naye UDSM wakati
anafundisha.

Dr.Mwakyembe hana role yoyote ya maana EAC kwa kuwa hakuna utaalamu wowote wa maana unaohitajika ili kuongoza wizara hiyo zaidi ya kutalii na kupiga blah blah tu. Ni moja wizara mpya, ndogo na changa sana. Ilipaswa kuwa ni Idara tu ndani ya wizara mama ya Mambo ya nje.
so EPA negotiation na trade agreements zinahitaji zoba kushughulikia sio?
 
Back
Top Bottom