Mwaka 2023 ndio Unaisha, je ni nani aliyeathiri maisha yako?

Megalodon

JF-Expert Member
Apr 9, 2021
2,256
4,099
Kuathiri kunaweza kuwa kwa Uzuri au kwa Ubaya.

Wengine wamejifunza uchawi JF na kwasasa ni waganga na wanapata Ugali.

Wengine wamepoteza watu wakaribu, njoo hapa muombee dua njema huko aliko

Wengine wamekuwa diagnosed na HIV, Kansa, ini, figo pole na njoo utuambie ilikuaje na unapata matibabu vema.

Wengine wamebadili imani zao, njoo utuambie nini kimetokea

Wengine wametoa divorce au wapo katika harakati za kutoa divorce , tuambie kwanini mmeshindwa kunusuru ndoa yenu

Harmonize katika hustle zake za maisha, hawezi kumsahau Diamond Platnumz… , Konde Boy njoo umshukuru Platnumz hapa mwambie neno zuri

Kuna wale wametapeliwa mazima, njoo uweke neno

Kuna wale ambao walipewa ahadi za kuolewa….. au kuoa : jamaa au binti kaingia mitini

Kuna wale vijana ambao wamemaliza zao chuo kutoka familia za kayumba wana hustle na bahasha mtaani, watesi wanajitokeza na kusema vijana jiajirini na mfikiri nje ya box huku wao wapo kwenye kiti cha kuajiriwa, njoo mwambie kitu watesi wako selfish creatures

Wale wote wanaochukizwa na kukatika kwa umeme mara kwa mara, hali yakuwa miaka 3 nyuma wa TZ walisahau hilo jambo, njoo uwaulize mwamba aliwezaje.

Waliochukizwa na inflation ya mafuta, dola, vyakula kupanda bei, nauli kupanda, tozo, barabara zilizokuwa kwenye ujenzi zimegeuka kuwa magofu hakuna kinachofanyika ili hali miaka 3 nyuma things were so perfect ….. njoo hapa waambie kitu watesi wako.

Kuna wale ambao wamekopa bank mahela hela , kichwa kinaenda race , njoo useme neno.

Kama pia unakereka na mwenendo JF kufuta futa nyuzi na kupiga watu ban ambao wanatoa opinions zao , njoo hapa waambie watesi wako na kwamba tutaanzisha JF nyingine itakayotoa uhuru wa kujieleza na kutoa maoni binafsi hata kama hayo maoni ni msumari kwa watawala.

Nawatakia heri ya mwaka mpya



Influencer ,
Ottawa, Canada.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom