Mwabukusi atangaza mapambano tena "Tunakwenda barabarani"

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,321
24,228
21 August 2023
Mbeya, Tanzania

MASHARTI HARAMU YA DHAMANA NIMEYAKATAA, NITAKWENDA POPOTE NA SITARIPOTI KITUO CHA POLISI KWA SABABU KUKAMATWA KWANGU NI KINYUME CHA SHERIA


View: https://m.youtube.com/watch?v=2DkDqk8bMPQ

Akiongea kwa mara ya kwanza toka achiwe kwa dhamana ya Polisi wakili msomi Boniface Mwabukusi ... tarehe 28 August na kuendelea sitaripoti tena kituo cha polisi.

===
Akiongea na vyombo vya habari baada ya kuachiwa na polisi, wakili Boniface Mwabukusi amesema atafanya maandamano kupinga mkataba wa bandari kama haki yake ya kikatiba. Hii itakuwa ni hatua ya pili katika kueleza kuwa baadhi ya vifungu vya mkataba wa bandari.

Mwabukusi amesema kesi ya bandari ambayo imekwisha tolewa hukumu haikuwa yake. Yeye alikuwa anafanya kazi yake ya uwakili katika kesi ile. Yeye suala lake litakuwa ni maandamano ambayo ni haki ya kikatiba katika uhuru wa kujieleza.

Aidha, amezungumzia kuhusu kukamatwa kwake na kuachiwa, huku akisema kuwa masharti aliyopewa ameyakataa. Baada ya kuachiwa alitakiwa kuripoti mara kwa mara kituoni suala ambalo amelikataa, pia alitakiwa kuwa katika kizuizi cha kutoenda baadhi ya maeneo, naye amesema ataenda kokote anapotaka.

Pia amewashauri waliomuwekea dhamana waandike barua ya kujiondoa kama wadhamini ili ikibidi arudi rumande
 
Mdude Nyagali -, Hatukubali kifungo cha nje kupitia dhamana ya polisi. Kupigwa marufuku kusafiri ni kinyume cha sheria kufuatana na hukumu aliyotoa jaji Lugakingira JA,wa mahakama ya rufaa ya Tanzania ....
Hongera Sana wazalendo God bless you
 
Back
Top Bottom