Mvua yaua watu 3 Mkoani Mara na kusababisha barabara kutopitika

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,282
091a2c0dc10f822a1b0a36633cd0c20c

Serengeti. Mvua kubwa iliyonyesha mkoani Mara nchini Tanzania imesababisha maafa ikiwamo vifo vya watu watatu wakiwamo watoto wawili wa familia moja na uharibifu wa miundombinu.

Pamoja na watoto hao, mwili wa dereva bodaboda aliyesombwa na maji wakati akivuka katika eneo la Issenye wilayani Serengeti mkoani Mara umepatikana

Diwani wa Issenye Ally Nyarobi amesema mvua iliyonyesha imesababisha daraja la Nyiberekera kukatika na dreva bodaboda alilazimisha kupita leo asubuhi Alhamisi ya Desemba 26, 2019 na kusombwa na maji yaliyosababisha kifo chake.

Mkuu wa wilaya ya Serengeti, Nurdin Babu amesema mwili wa dereva huo umepatikana hatua chache toka eneo alilozama na jina lake halijafahamika.

Amesema kwa mvua iliyonyesha usiku wa kuamkia leo Alhamisi imesababisha maafa hayo na baadhi ya madaraja kubomoka.

Babu amesema mvua hiyo imesababisha pia vifo vya watoto wawili wa familia moja na mmoja kujeruhiwa baada ya nyumba walimokuwa wamelala kujaa maji kisha kubomoka eneo la Issenye wilayani humo.

Amesema miili ya watoto hao imepelekwa kituo cha afya Nyamuswa wilaya ya Bunda mkoani humo wakati taratibu za mazishi zikiendelea.

Diwani wa Issenye (CCM), Ally Nyarobi amesema watoto hao ni wa Hagai Kongoye wenye umri wa miaka 10 na mwingine minne.

Mvua hizo zimesababisha barabara za kutoka Mugumu kwenda Arusha kupitia Fort Ikoma na Makunduzi kutopitika baada ya kukatika daraja na nyingine maji kujaa hadi juu.

"Barabara ya Natta Makundusi nayo haipitiki maana maji yamefunika daraja, magari ya kwenda Arusha au kutoka ikiwamo mabasi hayawezi kupita mpaka maji yapungue," amesema Babu

Amesema amewasiliana na Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroad) kuhusu suala hilo na wamemwahidi kufika haraka wilayani hapo ili kushughulikia daraja la Fort Ikoma liweze kupitika.

Kaimu Meneja wa Tanroad, Reginald Massawe amesema wamelazimika kutuma wataalam wao barabara zote za wilaya ya Serengeti ili kusaidia kurekebisha magari yaweze kuvuka kwenda na kutoka Arusha.

Mwananchi
 
Daaa masika hiyo ilichelewa kunya sasa inaelekea kuisha na majanga juu...
 
Huyo wa bodaboda nimesikia jirani yangu akimuongelea, wanadai alikua chakari na pikipiki ilikua imebeba watu wengine ila yeye peke ndio Allah kamuita.
 
Kumbe Mods ndo mnaharibu,kule kwenye facebook mmeweka picha gani ?
Yani mnajichanganya.
 
091a2c0dc10f822a1b0a36633cd0c20c

Serengeti. Mvua kubwa iliyonyesha mkoani Mara nchini Tanzania imesababisha maafa ikiwamo vifo vya watu watatu wakiwamo watoto wawili wa familia moja na uharibifu wa miundombinu.

Pamoja na watoto hao, mwili wa dereva bodaboda aliyesombwa na maji wakati akivuka katika eneo la Issenye wilayani Serengeti mkoani Mara umepatikana

Diwani wa Issenye Ally Nyarobi amesema mvua iliyonyesha imesababisha daraja la Nyiberekera kukatika na dreva bodaboda alilazimisha kupita leo asubuhi Alhamisi ya Desemba 26, 2019 na kusombwa na maji yaliyosababisha kifo chake.

Mkuu wa wilaya ya Serengeti, Nurdin Babu amesema mwili wa dereva huo umepatikana hatua chache toka eneo alilozama na jina lake halijafahamika.

Amesema kwa mvua iliyonyesha usiku wa kuamkia leo Alhamisi imesababisha maafa hayo na baadhi ya madaraja kubomoka.

Babu amesema mvua hiyo imesababisha pia vifo vya watoto wawili wa familia moja na mmoja kujeruhiwa baada ya nyumba walimokuwa wamelala kujaa maji kisha kubomoka eneo la Issenye wilayani humo.

Amesema miili ya watoto hao imepelekwa kituo cha afya Nyamuswa wilaya ya Bunda mkoani humo wakati taratibu za mazishi zikiendelea.

Diwani wa Issenye (CCM), Ally Nyarobi amesema watoto hao ni wa Hagai Kongoye wenye umri wa miaka 10 na mwingine minne.

Mvua hizo zimesababisha barabara za kutoka Mugumu kwenda Arusha kupitia Fort Ikoma na Makunduzi kutopitika baada ya kukatika daraja na nyingine maji kujaa hadi juu.

"Barabara ya Natta Makundusi nayo haipitiki maana maji yamefunika daraja, magari ya kwenda Arusha au kutoka ikiwamo mabasi hayawezi kupita mpaka maji yapungue," amesema Babu

Amesema amewasiliana na Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroad) kuhusu suala hilo na wamemwahidi kufika haraka wilayani hapo ili kushughulikia daraja la Fort Ikoma liweze kupitika.

Kaimu Meneja wa Tanroad, Reginald Massawe amesema wamelazimika kutuma wataalam wao barabara zote za wilaya ya Serengeti ili kusaidia kurekebisha magari yaweze kuvuka kwenda na kutoka Arusha.

Mwananchi
Mkuu wa wilaya ya Serengeti,mkurugenzi wa Halmashauri ya Serengeti, mbunge wa wilaya ya Serengeti, meneja wa Tanroad mkoa wa Mara hawamasidii Mh Rais kuwakomboa na kuwasaidia wananchi wa wilaya ya Serengeti hata kidogo. Nafasi zao laiti zingekuwa wazi bila kupewa mtu yeyote nadhani kusingekuwa na madhara. Wilaya ya Serengeti tunakuomba Mh Rais atembelee hiyo wilaya,Hali ni mbaya sana sana,hskumi maji,hakuna umeme,hskuna barabara,hakuna shule za kutosha wanafunzi,hakuna hospital ,hakuna chakula watu wanakufa njaa hakuna vyakula,wananchi hawana nyumba za kuishi, hakuna faida ya uwepo kwa Serengeti national park kwa wananchi wa eneo Hilo, wanyama pori wanauwa watu hakuna ofisi ya wanyamapori, Sasa unakuwa kwamba wananchi wa Serengeti walilaaniwa kitu smbacho si kweli.Hali ya wilaya ya Serengeti utadhani haipo kwenye ramani ya Tanzania.Tunamuomba Mh Rais atembelee wilaya ya Serengeti, nyang'wale,Bukombe, nzera, simanjiro, kilosa,rufiji,makete,kongwa ajionee hali ulivyo.
 
Watani wangu wa Mara wa Sasa hivi wamelegea Sana

Yaani mvua Hadi inaua watu wameshindwa kuitokea na mapanga waikate Kate iache kusumbua watu?

Mvua inanyesha hivyo Akina Mura mnaiangalia tu
 
Back
Top Bottom