Muungano ukivunjika na Zanzibar itavunjika

Father of All

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
6,376
6,720
Kwa wanaojua kanuni za uharibifu, huwa hauachii mahali au kwenye kitu kimoja.

Nyerere aliwahi kuulinganisha na kula nyama ya binadamu. Ailaye haachi. Sijui ukweli wa dhana hii.

Hata hivyo, ukiwasikia wanaohanikiza tuvunje muungano, unapata wasiwasi nao.

Mfano, juzi mtu mmoja aitwaye Jussa alisikika akisema tuuvunje na kugawana mbao. Haya ni mawazo mafupi hasa kwa upande wa visiwani ambao watu wengi hujidanganya kuwa muungano ukivunjika watakuwa kama Dubai kwa vile wameonja harufu ya mafuta. Ni uchoyo na upofu mtupu.

Muungano ukivunjika, yafuatayo yanaweza kutokea:

Mosi, wapemba nao watataka kujitenga na waswahili weusi ili wawe karibu na ndugu zao waarabu ambao huwa wanawaabudia japo waarabu wanawaona kama watumwa wa kawaida.

Pili, Tanganyika italazimika kuwatimua wazenj wote ili warejee kwao na Zenj itajibu mapigo japo hatua hii itazua tatizo jingine.

Tatu, kama idadi ya Wazenji wote walioko bara watatimuliwa, Zanzibar haitakuwa na uwezo wa kuwatosheleza kimaisha hata kama ingekuwa na hayo mafuta ambayo haina uzoefu wa kuya-manage sawa na nchi nyingine za kiafrika.

Nne, Zenj itakumbwa na tishio la mapinduzi toka kwa migawanyiko yake ya asili baina ya waliofanya mapinduzi na waliopinduliwa ambavyo kimsingi, ndiyo sababu kuu iliyoisukuma kuungana na Bara.

Tano, Zenj itakuwa na tishio la usalama kutokana na kutokuwa na jeshi lake na vyombo vingine vya ulinzi. Hivyo, italazimika kuendelea kutegemea Tanganyika hata kama ni kinafiki.

Sita na mwisho, Zenj itatumia fedha nyingi kuagiza bidhaa toka Tanganyika katika fedha za kigeni jambo ambalo litaathiri vibaya uchumi wake.

Unaweza kuongeza madhara mengine na faida kama zipo.
 
Tanganyika ukabila si tatizo. Tatizo letu ni udini
Tanganyika ukitoa Zanzibar hakuna udini, patakuwa na ukbali. Kama ni udini hizi ishu zingeibuka kipind cha kikwete.

Haya mambo yote yapo kwa watu dhaifu labda kuleta udini na ukabila ndiyo point dhaifu ya mtu kufikiria kabisa.

Ninachoamini hata uchukue Singida ile uifanye kama nchi basi itakuwa mbali kimaendeleo na wala kama Zanzibar itaweza kuyumba kwanza kule vyakula bei juu tangu naanza kuijua Zanzibar.

Kingine suala la kufukuza watu hilo halipo kwa vile kuna ishu ya Uraia wapo maelfu ya Watanzania wapo South Africa , Marekani, Canada, Italy na nchi nyingine so aliwezi kuleta shida, mtu anaweza kuishi popote pale.
 
Hakutakuwa na madhara yoyote kwa Tanganyika iwapo muungano utavunjika
Kwani kuachana na wazanzibar kuna nini ndani ya muungano?

Mbona kuna jamii nyingi tu tunaishi nazo kama ndugu na hata hao Wazanzibar tupo nao na tunaishi nao kindugu.

Achana na wazanzibar tupo na waganda wengi mitaan mwanza, Arusha tupo na wakenya kwa wingi.

So ukabila kwa Tanganyika itakuwa ndoto labda tufanye bidii kuuleta.

Tatizo naliona kwa wenzetu upande wa pili maana uwezi kubisha jamaa wale ni wabaguzi, na kinachowatafuta ni kujitafsiri wao ni waarabu na kujiona wao wanaonewa na Tanganyika.

Mi naliona koti linazidi kuwa zito tulivueni.

Jamii ibaki na ushirikiano ila kila nchi ijitegemee
 
Kwa wanaojua kanuni za uharibifu, huwa hauachii mahali au kwenye kitu kimoja.

Nyerere aliwahi kuulinganisha na kula nyama ya binadamu. Ailaye haachi. Sijui ukweli wa dhana hii.

Hata hivyo, ukiwasikia wanaohanikiza tuvunje muungano, unapata wasiwasi nao.

Mfano, juzi mtu mmoja aitwaye Jussa alisikika akisema tuuvunje na kugawana mbao. Haya ni mawazo mafupi hasa kwa upande wa visiwani ambao watu wengi hujidanganya kuwa muungano ukivunjika watakuwa kama Dubai kwa vile wameonja harufu ya mafuta. Ni uchoyo na upofu mtupu.

Muungano ukivunjika, yafuatayo yanaweza kutokea:

Mosi, wapemba nao watataka kujitenga na waswahili weusi ili wawe karibu na ndugu zao waarabu ambao huwa wanawaabudia japo waarabu wanawaona kama watumwa wa kawaida.

Pili, Tanganyika italazimika kuwatimua wazenj wote ili warejee kwao na Zenj itajibu mapigo japo hatua hii itazua tatizo jingine.

Tatu, kama idadi ya Wazenji wote walioko bara watatimuliwa, Zanzibar haitakuwa na uwezo wa kuwatosheleza kimaisha hata kama ingekuwa na hayo mafuta ambayo haina uzoefu wa kuya-manage sawa na nchi nyingine za kiafrika.

Nne, Zenj itakumbwa na tishio la mapinduzi toka kwa migawanyiko yake ya asili baina ya waliofanya mapinduzi na waliopinduliwa ambavyo kimsingi, ndiyo sababu kuu iliyoisukuma kuungana na Bara.

Tano, Zenj itakuwa na tishio la usalama kutokana na kutokuwa na jeshi lake na vyombo vingine vya ulinzi. Hivyo, italazimika kuendelea kutegemea Tanganyika hata kama ni kinafiki.

Sita na mwisho, Zenj itatumia fedha nyingi kuagiza bidhaa toka Tanganyika katika fedha za kigeni jambo ambalo litaathiri vibaya uchumi wake.

Unaweza kuongeza madhara mengine na faida kama zipo.
Muungano haukupata baraka ya wenye nchi. Ni kama vile ndoa ya kulazimishwa. Lilikuwa ni takwa la Nyerere na Karume.

Pengine wananchi wangeshirikishwa, wangeweza kutoa maoni yao. Wananchi ndiyo wenye nchi. Wasikilizwe!

Kwani wenye nchi wanasemaje kuhusu Muungano?
 
Kwamba Tanganyika itabaki salama?
Wale wanaowachukia wazanzibari Kwa sababu ni waislam unafikiri chuki Yao itaishia Kwa wazanzibari?
Waislam wapo Zanzibar tu?

Aliekwambia Zanzibar vyakula vitapanda bei nani?lazima kununua Tanganyika?au Tanganyika ndo nchi pekee inazalisha vyakula duniani?

Aliekwambia nchi zikivunjika lazima Raia wafukuzwe nani??
Kila Mtanzania aliezaliwa baada ya mwaka 1964 huku Tanganyika ana haki ya kuchukua Uraia wa Tanganyika...
Zanzibar ..watapiga hatua kubwa Sana ...billa kuzuiwa na watanganyika
 
Kikwete kapitia Sana changamoto hizi, huna kumbukumbu tu.

Katukanwa Sana, na mara zote chuki za udini zinajificha kwa watu kujifanya wazalendo lakini linalofukuta moyoni ni jingine kabisa
Yaani duniani chuki ni kitu cha kawaida na ni changamoto pia...Ni kuishi nazo ndo maisha.
 
Back
Top Bottom