Muswaada wa Baraza la Vijana Tanzania umeigwa(Copy and Paste)kutoka Kenya

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
10,131
35,164
Toka siku ya jana ndani ya bunge la Tanzania kulikuwa na mjadala kuhusu kuundwa kwa baraza la vijana nchini Tanzania. Wabunge kadhaa walisikika wakichangia kwa kuukosoa Muswaada huo kwa kuwa karibu wote umeigwa(Copy and Paste) kutoka Kenya huku ukiacha mambo ya msingi yanayohusu mazingira halisi ya vijana wa Kitanzania.

Serikali ya Tanzania kupitia kwa Naibu waziri wa Vijana, habari na michezo Juma Nkamia leo wakati wa majumuisho wa hoja alisema kuwa, ni kweli Muswaada huo kwa sehemu Kubwa umeigwa (Copy and Paste) kutoka Kenya.

Nini Uzuri na ubovu wa sheria ya uundwaji wa baraza la vijana la Kenya kiutekelezaji, kwa kuwa soon Tanzania will experience the same?
 
  • Thanks
Reactions: Gor

Hivi ni ule wa Binafsi uliowasilishwa na Mh Mnyika, Mbunge wa Ubungo au ni mwingine? Maana nilishangaa kuona hata Mbunge huyo akiukosoa!
 
Ni kweli kabisa,,,, copy and paste ndugu zetu wakenya walishaona mwanga siku nyingi sisi bado tupo gizani.
Tujikakamue wenxetu
 
Hahhahhaaa...kuna kipengele kinazungumzia kwamba "BARAZA SIO CHOMBO KINACHOFUNGAMANA NA CHAMA CHOCHOTE". Lakini moja ya kanuni zake zinatamka kwamba waziri mkuu ndie atakaemchagua mwenyekiti wa baraza na ndiye atakayeratibu matumizi ya fedha ya baraza.

Swali: kwani waziri mkuu sio mwanasiasa?

Na kama ni baraza la vijana kwanini mwenyekiti ateuliwe na waziri mkuu badala ya kuchaguliwa kutokana na mikutano na vikao vya baraza?
Hapo nakosa majibu jamani
 
Hivi ni ule wa Binafsi uliowasilishwa na Mh Mnyika, Mbunge wa Ubungo au ni mwingine? Maana nilishangaa kuona hata Mbunge huyo akiukosoa![/QUOTE

Mnyika alipeleka wazo ambalo alilipata baada ya kukaa na vijana.. vijana waliandika vitu vingi kuhusiana na baraza lao.... lakini cha kustajabisha serikali lichukua wazo na kwenda kutengeneza huko upuuzi wakidhani vijana watakubali tuuuh
 
Toka lini ccm wameanza kutumia akili katika utendaji wao wa kazi na ubunifu wa sera endelezi? Kila siku ni consultants kutoka nje ya nchi kwa gharama ya mamilioni. Sitoshangaa kusikia hiyo copy and paste imetu-cost mabilioni pia.
They will never stop. They always look for something that's not the top priority.
 
Hivi ni ule wa Binafsi uliowasilishwa na Mh Mnyika, Mbunge wa Ubungo au ni mwingine? Maana nilishangaa kuona hata Mbunge huyo akiukosoa![/QUOTE

Mnyika alipeleka wazo ambalo alilipata baada ya kukaa na vijana.. vijana waliandika vitu vingi kuhusiana na baraza lao.... lakini cha kustajabisha serikali lichukua wazo na kwenda kutengeneza huko upuuzi wakidhani vijana watakubali tuuuh

Muswada wa Mnyika ulishasomwa mara ya kwanza bungeni. Kinachonitatiza ni kwa nini serikali ipeleke Muswada mwingine bila kuendelea ule wa Mnyika! Au ni Muswada ule ule yakiwemo mabadiliko ya Serikali?
 
Back
Top Bottom