Mungu yupo

Suhendra

JF-Expert Member
Nov 25, 2023
1,074
2,461
Kuna jambo limenisukuma sana kuandika huu Uzi.

Mambo ambayo yanaendelea kuhusu uwepo wa Mungu.

Kuna baadhi ya watu wa amini hakuna mungu nk.

Ni ingie kwenye point.

Uwepo wa mungu una dhihirika kwa alama zake na viumbe vyake.

Hebu tutafakari kama hakuna mungu nani alieumba bahari, jua, mbingu, binadamu, wanyama hivi vitu vimetokea vipi kama hakuna alieviimba.

Leo hii hata ukimchukuwa mtoto mdogo wa miaka mitatu ukamuuliza nani kaumba mbingu atakujibu mungu.

Vipi mtu mzima mwenye akili timamu unashindwa kutambua hilo.

Yapo mambo mengi sana yana thibitisha uwepo wa mungu naweza kesha kuelezea kiufupi, Tufahamu mungu yupo na yeye ndo ametuumba sisi ili tumuabudu yeye tu.
 
Kama vilivyo complex hivi vyote vyenye high order hivi ulivyovitaja, bahari, jua, watu, wanyama, ni lazima viwe vimeumbwa na higher intelligence, basi complexity haiwezi kutokea bila kuumbwa na higher intelligence.

Sasa, hapo hapo linakuja swali, kwa kanuni hiyo hiyo ya kwamba kilicho complex hakiwezi kuwepo tu, ni lazima kiwe kimeumbwa, hata Mungu wako naye atahitaji kuwa ameumbwa, na aliyemuumba naye atahitaji kuwa na muumba, hivyo hivyo, bila mwisho.

Kwa hiyo, ukisema kuwa bahari, jua, watu ni lazima vimeumbwa, kwa sababu complexity haiwezi kutokea tu, kimsingi hapo unasema Mungu hayupo, labda hujaelewa tu kwamba unajenga hoja kwamba Mungu hayupo.

Ni hivi.

Ama, hivi vitu complex ni lazima viwe vimeumbwa, ama si lazima.

Kama si lazima viwe vimeumbwa, hapo Mungu hahitajiki, kwa sababu kama ulivyosema, unatumia dhana ya kwamba Mungu kaumba kudhihirisha Mungu yupo. Kama vitu hivi si lazima viwe vimeumbwa, basi Mungu hahitajiki.

Kama ni lazima viwe vimeumbwa, basi huyo unayemuita Mungu naye ni lazima awe kaumbwa, na kama ni lazima awe kaumbwa, huyo si Mungu.

Sijui hata kama una uwezo wa kuelewa hizi hoja.
 
Acha mengine yoote, hapo kwenye JUA

Unajua nimekuwa nikitafakari umuhimu wa Jua ni mkubwa sanaaa, bila jua hatupati maji kwsbb ya Evaporation, Transpiration n.k

Bila jua hatupati chakula kwsbb mmea hutengeneza chakula kukiwa na mwanga wa jua

Jua inafanya mifupa ya viumbe vyote vyny skeletons viwe strong

Joto la jua linaneutralize climate yetu

Aliyeumba au kutengeneza jua ni nani? Aliyeweka Ozone Layer ni nani?
 
Kwa nini swali lako linakuwa "aliye...?".

Huoni kuwa swali lako linalenga kwenye jibu unalolitaka tayari? Huoni swali yako lina bias, kasumba ya kwamba kuna "aliyeumba"?

Sayansi imeshaelezea vizuri kabisa jinsi jua lilivyotokea. Na maelezo hayo hayamuhutaji Mungu.

Wewe umesoma nini kuhusu maelezo ya kisayansi kuhusu jua lilivyotokea?

Tunasoma haya mambo au tunashangaa tu na kusema hii ni kazi ya Mungu?

Mbona vitu vyote vipo mtandaoni? Tatizo ni nini, ni hiki Kiingereza?

Formation​

The Sun formed about 4.6 billion years ago in a giant, spinning cloud of gas and dust called the solar nebula. As the nebula collapsed under its own gravity, it spun faster and flattened into a disk. Most of the nebula's material was pulled toward the center to form our Sun, which accounts for 99.8% of our solar system’s mass. Much of the remaining material formed the planets and other objects that now orbit the Sun. (The rest of the leftover gas and dust was blown away by the young Sun's early solar wind.)
 
Kuna jambo limenisukuma sana kuandika huu Uzi.
Mambo ambayo yanaendelea kuhusu uwepo wa mungu.
Kuna baadhi ya watu wa amini hakuna mungu nk.

Ni ingie kwenye point
Uwepo wa mungu una dhihirika kwa alama zake na viumbe vyake.

Hebu tutafakari kama hakuna mungu nani alieumba bahari, jua, mbingu, binadamu, wanyama hivi vitu vimetokea vipi kama hakuna alieviimba.

Leo hii hata ukimchukuwa mtoto mdogo wa miaka mitatu ukamuuliza nani kaumba mbingu atakujibu mungu.

Vipi mtu mzima mwenye akili timamu unashindwa kutambua hilo.

Yapo mambo mengi sana yana thibitisha uwepo wa mungu naweza kesha kuelezea kiufupi, Tufahamu mungu yupo na yeye ndo ametuumba sisi ili tumuabudu yeye tu.
Sawa umejibu kama mtoto wa miaka 3
 
Nnachoamini Mimi,

Hakuna kiumbe asiyeamini Hakuna Mungu, Bali kila kiumbe kina Mungu wake kinaemuamini, wengine mnaita "miungu"

Tatizo linakuja pale mnapotaka kutuaminisha kwamba Mungu wenu wa kwenye biblia na qurani kua ndio Mungu sahii.

Hao wengine mmewabatiza majina mabaya mabaya TU Kama majini,mizimu,miungu, misukule,frimasoni,mapepo n.k
 
Kama vilivyo complex hivi vyote vyenye high order hivi ulivyovitaja, bahari,jua, watu, wanyama, ni lazima viwe vimeumbwa na higher intelligence, basi complexity haiwezi kutokea bila kuumbwa na higher intelligence.

Sasa, hapo hapo linakuja swali, kwa kanuni hiyo hiyo ya kwamba kilicho complex hakiwezi kuwepo tu, ni lazima kiwe kimeumbwa, hata Mungu wako naye atahitaji juwa aneumbwa, na aliyemuumba naye atahitaji kuwa na muumba, hivyo hivyo, bila mwisho.

Kwa hiyo, ukisema kuwa bahari, jua, watu ni lazima vimeumbwa, kwa sababu complexity haiwezi kutokea tu, kimsingi hapo unasema Mungu hayupo, labda hujaelewa tu kwamba unajenga hoja kwamba Mungu hayupo.

Ni hivi.

Ama, hivi vitu complex ni lazima viwe vimeumbwa, ama si lazima.

Kama si lazima viwe vimeumbwa, hapo Mungu hahitajiki, kwa sababu kama ulivyosema, unatumia dhana ya kwamba Mungu kaumba kudhihirisha Mungu yupo. Kama vitu hivi si lazima viwe vimeumbwa, basi Mungu hahitajiki.

Kama ni lazima viwe vimeumbwa, basi huyo unayemuita Mungu naye ni lazima awe kaumbwa, na kama ni lazima awe kaumbwa, huyo si Mungu.

Sijui hata kama una uwezo wa kuelewa hizi hoja.
Kuna kitu kidogo tu bado huja kielewa vyote ulivyo sema ni sawa, mungu ninae mzungumzia hapa yupo juu ya kila kitu hadi unacho kifikiria hasaivi
 
Back
Top Bottom