Mume wa Angela Kairuki achelewesha hati, Kutumbuliwa na Rais Magufuli?

Jamaa kuna wakati alitaka kujiuzulu baada ya ndoa yake "kuchezewa", ikatokea kuwa itakuwa scandal kwa jumba kubwa. Watu wa kitengo wakaaambiwa waichunguze ile Taasisi yao ya Hospital pale Mikicheni, inaonekana ina kashfa ya kukwepa kodi. Jamaa wakamtonya Balozi kuwa ukifurukuta tu aidha kujiuzulu au talaka wazee wa TKKR na TRA wanaweka kambi.

Basi yuko "ransom" ndiyo maana yuko kimya.
Shetani mbaya sana.
 
aisee kumbe alitupwa mbali ili goli libaki bila kipa.
.
tapatalk_1571394126445.jpeg
 
Hata Hawa Ghasia mumewe alitupwa kule India
WANAWAKOSESHA haki za binadamu, haki ya msingi kabisa ya mtu yeyote aliyefika miaka 18 ni " KUFANYA MAPENZI" sasa unapowatenganisha unamkosesha mtu haki yake ya kutia ama kutiwa
 
Naukumbuka ule waraka wa mfalme Daudi "Mweke Uria mstari wa mbele penye mapigano makali na kisha urudi nyuma, mwache auawe" Baada ya muda akazaliwa Suleiman! Aah Daudiii!
Dooooh! mfalme Daudi alijimwambafy, kumbe kuna mwamba zaidi yake akaishia kuweweseka miaka nenda rudi
 
Mume wa Angela kairuki , infact Angel ni Mpare, na waziri hapa Tanzania amefanya blander kwa kuchelewesha hati huku akishindwa kuendana na kasi za Jiwe


*IMEKUWAJE BALOZI MBELWA KAIRUKI AMECHELEWA KUWASILISHA HATI VIETNAM NA JE ANAHUSIKA KUIWAKILISHA TANZANIA VIETNAM?*

Balozi wa Tanzania, Beijing China Mheshimiwa Mbelwa Kairuki Jumatano tarehe 16/10/2019 aliwasilisha hati za utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Watu wa Vietnam Mheshimiwa Nguyen Phu Trong katika ikulu ya nchi hiyo jijini Hanoi, Vietnam.

Kumekuwa na maswali ya kutaka kufahamu kuwa je balozi Kairuki anaiwakilisha Tanzania nchini Vietnam pia? Je kama ni hivyo hakuna nchi nyingine ambazo anaiwakilisha Tanzania? Na kwa nini amechelewa kuwasilisha hati katika nchi hiyo ya Vietnam?

Jibu ni kweli kuwa Balozi Kairuki anaiwakilisha Tanzania Hanoi, Vietnam. Mbali na China na Vietnam kwa mujibu wa muongozo wa mabalozi wa Juni, 2008 Balozi Kairuki anaiwakilisha Tanzania nchini Laos, Cambodia, Mongolia, Thailand na Jamhuri ya Watu wa Korea maarufu kama Korea Kaskazini.

Kwa lugha ya kidiplomasia Balozi anaewakilisha nchi yake katika nchi zaidi ya moja huitwa Balozi mwenye Multiple Accreditation.

Kuhusiana na kuchelewa kuwasilisha hati, Uwanja wa Diplomasia umeona ni vema kutolea ufafanuzi juu ya utaratibu wa uwasilishwaji wa hati za mabalozi.

Mosi, kabla hatujaendelea ni vema tufahamu kwa nini nchi huamua kuwa na mwakilishi mmoja katika nchi zaidi ya moja (multiple accreditation) na pia kwa nini nchi huchagua kufungua balozi katika nchi fulani na kutofungua katika nchi nyingine?

Kuna sababu kama sits zinafanya nchi kuwa na balozi nyingi au chache au kuamua kuwa na mwakilishi mmoja katika nchi zaidi ya moja, nazo ni:

(1) Sababu za kihistoria

(2) Ukaribu wa kijiografia

(3) Sababu za kiuchumi

(4) Uwezo wa nchi kifedha (Kufungua balozi na kupeleka watendaji si jambo dogo hata kidogo)

(5) Muungano wa kisiasa (Mfano EAC, SADC n.k)

(6) Kutekeleza kanuni ya kulipa (Reciprocity) baada ya nchi nyingine kuwa imefungua ubalozi katika nchi yenu baada ya makubaliano (mutual consent) kama ilivyoelezwa kwenye ibara ya pili ya Mkataba wa Vienna wa mwaka 1961 unaohusu mahusiano ya Kidiplomasia.

Pili, kabla hatujatazama uwasilishwaji wa kati ni vema tufahamu pia mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao katika nchi zaidi ya moja (multiple accredited) hupatikana vipi.

Kama tulivyokwisha kueleza katika makala iliyomhusu Dkt. Benson Bana kwamba uteuzi wa mabalozi hufanyika kwa siri mno.

Kwa mabalozi wanaotarajiwa kuwakilisha nchi zao katika nchi zaidi ya moja jina la balozi mtarajiwa hutumwa huko wakati ule ule wa uteuzi wake na kusubiri majibu kutoka kwa nchi hizo husika.

Ndiyo maana ibara ya 4 (1) imesisitiza kuwa, "Nchi iliyomtuma balozi ni muhimu ijiridhishe kuwa nchi iliyotarajiwa kumpokea balozi imemkubali mteule huyo." Kitendo hiki kwa lugha ya kidiplomasia huitwa agremo/a.

Ibara hiyo hiyo ya 4 (2) imeweka onyo kuwa, "Nchi inayompokea Balozi haipaswi kueleza sababu za kumkataa mteule tajwa (Persona non grata)."

Baada ya kuwa mteule amekubaliwa na nchi hiyo/hizo nchi iliyomtuma balozi huyo inaweza kumpa jukumu balozi husika au kumpa kazi afisa mwingine wa juu kuwakilisha katika nchi zaidi ya moja isipokuwa kama kuna pingamizi kutoka kwa nchi mojawapo kati ya hizo [Ibara ya 5 (1)].

Ibara ya 5 (2) imeendela kueleza kuwa, "Kama nchi inayomtuma Balozi itampa jukumu balozi kuwakilisha nchi yake kwenye nchi moja au zaidi, inaweza kufungua ubalozi unaoongwa na Balozi wa Muda (Chargé d' Affairés ad interim) kuongoza ubalozi katika kila moja ya nchi hizo ambapo Balozi husika hana kiti chake cha kudumu.

Hapa mfano ni kwamba ikiipendeza nchi ya Tanzania, kwa kuwa kiti cha kudumu cha Balozi Kairuki kipo Beijing, China basi Tanzania inaweza kupeleka mabalozi wa muda nchini Vietnam, Laos, Cambodia, Mongolia, Thailand na Korea Kaskazini.

Hivyo ndiyo tafsiri ya Ibara ya 5 (2) kwa mujibu wa Mkataba wa Vienna wa mwaka 1961 unaoongoza mahusiano ya kidiplomasia baina ya nchi na nchi au nchi na taasisi za Kimataifa.

Baada ya kufahamu hayo, sasa ni vema kufahamu kwa kina juu ya utaratibu mzima wa uwasilishwaji wa hati za utambulisho wa mabalozi ili tuweze kuwa na ufahamu juu ya suala hili la kiitifaki.

Kwanza kabisa kabla ya kuendelea ni vema wote tukafahamu kuwa kwa utaratibu wa itifaki Balozi hawezi kutekeleza majukumu yake mpaka awe amewasilisha hati za utambulisho wake (Letter of Credence) sambamba na zile za kuitwa nyumbani kwa mtangulizi wake (Letter of Recall).

Hivyo basi kuwasilisha hati kwa Balozi ni kuanza kazi rasmi kwa Balozi.

Kwa uchache ni vema tukapata kufahamu mambo yanayojiri pindi Balozi anapowasili katika kituo chake cha kazi kwa kingereza "Post".

Mara baada ya kuwasili katika kituo chake cha kazi Balozi hutakiwa kuijulisha Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi iliyompokea kuwa amewasili rasmi.

Baada ya hapo Balozi atafanya taratibu za kuwasilisha nakala zake za utambulisho (Letter of Credence) na za kuitwa nyumbani kwa mtangulizi wake (Letter of Recall) haraka iwezekanavyo kwenye Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo.

Letter of Credence ambayo kwa Kiswahili tunaiita "Hati ya Utambulisho" huwa ni ujumuisho wa taarifa zote muhimu juu ya Balozi yakiwemo:

(1) Majina yake

(2) Umri wake

(3) Kiwango chake cha elimu ama weledi alio nao

(4) Mwanzo wa kuanza majukumu yake n.k

Kuna mambo kadhaa huweza kuchangia mabalozi kuchelewa kuwasilisha hati zao, mambo haya ni kama yafuatayo:

(1) Kuna nchi huwa hazipokei hati siku za Jumamosi ama Jumapili.

(2) Kuna nchi huwa hazipokei hati siku za matukio ya kiimani.

(3) Kuna nchi huwa hazipokei hati kipindi cha maombolezo.

(4) Kuna nchi huwa hazipokei hati siku za sikukuu

Kuna baadhi ya nchi huruhusu Balozi kuanza kutekeleza majukumu yake mara baada ya kuwa amewasilisha hati kwenye Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi husika.

Kutokana na kwamba Balozi hawezi kutekeleza majukumu yake pasina kuwasilisha hati zake kwa Mkuu wa Nchi. Balozi anapaswa kufahamu mazingira ya kule aendako mapema mara baada ya kupangiwa kwenda huko tangu akiwa nchini mwake. Hii husaidia kuepusha asikae muda mrefu bila ya kuwasilisha hati zake pindi anapowasili kwenye nchi aliyopangiwa.

Ifahamike pia kuwa Balozi hawezi kuelekea kwenye "post" yake pasina kuwasilisha hati zake kwa Mkuu wa Nchi husika.

Ili Balozi aweze kuwasilisha hati zake, kitengo cha Itifaki cha nchi iliyompokea Balozi husika huujulisha Ubalozi nchi iliyomtuma Balozi (Sending State) juu ya siku maalumu kwa Balozi husika kuwasilisha hati zake.

Tunapaswa kufahamu kuwa kila nchi huwa na utaratibu wake wa kuandaa sherehe za uwasilishwaji wa hati za utambulisho wa Balozi.

Utaratibu wa uwasilishwaji hati huweza kutofautiana kutokana na mila, desturi, utamaduni ama imani za nchi iliyompokea Balozi.

Kwa msingi huo Balozi husika na wafanyakazi wa Ubalozi wake wanapaswa kufuata utaratibu uliowekwa na nchi iliyompokea katika kuhudhuria sherehe ya uwasilishaji hati.

Baada ya kuwasilisha hati kwa Balozi, Ubalozi hushauriwa kuandaa sherehe ndogo katika Ubalozi au nyumbani kwa Balozi kuashiria mwanzo rasmi wa majukumu ya Balozi.

Kwa mantiki ya maelezo haya, pindi balozi awasilishapo hati zake huwa ameanza rasmi majukumu yake katika nchi iliyompokea (Receiving State)

Balozi hupaswa kuwatembelea mabalozi wenzake kwa kuanzia kwa Balozi kiongozi (Dean of Diplomatic Corps) na kuendelea na wengine kwa kufuata utaratibu wa kiitifaki wa "aliyekuwa wa kwanza kufika katika post husika huwa ndiye mkubwa kwa mwenzake" yaani Order of Precedence.

Kuwatembelea mabalozi wenzake na kuhudhuria mikutano inayoandaliwa na mabalozi wenzake humsaidia Balozi kujifunza mambo mengi juu ya namna ya kutekeleza majukumu yake ndani ya nchi hiyo.

Kwa ufupi hivyo ndivyo ambavyo neno "Balozi kuwasilisha hati za utambulisho" linavyotafsiriwa kidiplomasia na pia kidiplomasia hizo ndizo sababu zinazoweza kuwa zimepelekea Balozi Mbelwa Kairuki kuchelewa kuwasilisha pale Ikulu ya Hanoi, Vietnam.

Abbas Mwalimu.
Mbona mnakuwa wajinga sana yani maelezo marefu mda wa kusoma yote hayo tutatoa wapi?
 
Moja ya njia ya kuyapata maarifa ni kusoma...

Thread ikiwandefu waweza subscribe halafu ukawa waisoma taratibu
Humu jf tunapiga porojo Sasa ukiandika thesis Nani kakwambia Yuko shuleni?
 
Mbelwa ni jina la Kizigua,Kairuki ni jina lenye asili ya Kenya,hii imekaaje?Tupe ufafanuzi tafadhali.And then imekuaje familia moja iule kiasi hicho,ni coincidence tu kwa kuwa they deserve it, au kuna jambo.Nauliza tu kutaka kujua,maana mimi sio punguani.Na huyu Anjela mbona kafanana sana na Waziri Mkuu mmoja wa zamani,ni yale yale ya waswahili kwamba binadamu wako wawili wawili au?
Mkuu yote mberwa na kairuki ni majina ya kihaya wa huko bukoba vijijin.


Kariuki ndo kikenya
 
Hiv ni kweli mberwa kairuki ndiye Mme wa Angela?


Kairuki ni jina linalotumiwa na wahaya wengi kuna Yule abayemiliki hospital ya kairuki
 
Jamaa kuna wakati alitaka kujiuzulu baada ya ndoa yake "kuchezewa", ikatokea kuwa itakuwa scandal kwa jumba kubwa. Watu wa kitengo wakaaambiwa waichunguze ile Taasisi yao ya Hospital pale Mikicheni, inaonekana ina kashfa ya kukwepa kodi. Jamaa wakamtonya Balozi kuwa ukifurukuta tu aidha kujiuzulu au talaka wazee wa TKKR na TRA wanaweka kambi.

Basi yuko "ransom" ndiyo maana yuko kimya.
Mtume!!! Nahisi kama tunamsingizia kwani huyo Eve hakuwa na utashi wa kukataa kwa maana anamilikiwa na Adam au mi ndo sielewi!!!!
 
Hiv ni kweli mberwa kairuki ndiye Mme wa Angela?


Kairuki ni jina linalotumiwa na wahaya wengi kuna Yule abayemiliki hospital ya kairuki
Jamani nadhani Wahaya hawana Mbelwa wala Mberwa wana Buberwa.Nadhani watu wanachanganya.
 
Back
Top Bottom