UZUSHI Muigizaji Jackie Chan avaa fulana yenye picha ya Muhoozi Kainerugaba, mtoto wa Rais Museveni

Baada ya tathmini, tumebaini kuwa taarifa hii ni ya uzushi
Muigizaji Jackie Chan ameonekana akiwa amevaa fulana yenye picha ya Muhoozi kainerugaba, Mtoto wa Rais Museveni.
Screening+Sony+Pictures+Karate+Kid+OEMISEXj4NTx.jpg
 
Tunachokijua
Picha ya mwigizaji na mtayarishaji filamu maarufu wa nchini China Jackie Chan akiwa amevalia fulana iliyochapishwa picha ya Muhoozi Kainerugaba, mtoto wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni, imekuwa ikisambaa katika mitandao ya kijamii. Maandishi chini ya picha yanasomeka kwa Kiingereza: "Rais Ajaye".

Picha hii inadhamiria kuonesha kuwa Jackie Chan anamuunga mkono Kainerugaba kama mrithi wa baba yake, Rais Museveni, ambaye amekuwa madarakani tangu 1986.

Katika picha, Jackie Chan anaonekana akiwa na Jaden Smith ambaye ni mwimbaji, na mwigizaji wa Marekani mwenye umri wa miaka 24 sasa. Chan na Smith waliigiza pamoja katika The Karate Kid, filamu iliyotoka mwaka 2010.

Google Reverse Image Search inaonesha kuwa picha hiyo imehaririwa kwa lengo la kupotosha umma. Katika picha halisi fulana ya Jackie Chan ni nyeupe, isiyo na picha ya Kainerugaba.

muhoozi-jpg.2400285

Picha isiyo halisi ya Jackie Chan
Picha halisi inaonesha kuwa ilipigwa tarehe 26 Mei, 2010, na inawaonesha Jackie Chan na Jaden Smith wakiwa katika zulia jekundu kwenye tamasha la Kick it with Karate Kid Street huko jijini Dallas, katika jimbo la Texas Marekani.

screening-sony-pictures-karate-kid-oemisexj4ntx-jpg.2400287

Picha halisi ya Jackie Chan
Hivyo basi, picha inayomuonesha Jackie Chan akiwa amevaa fulana yenye picha ya Muhoozi Kainerugaba kama rais ajaye wa Uganda, ni ya upotoshaji.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom