Muhimbili: Mwandishi ajifanya mgonjwa, nusura apasuliwe tumbo

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
  • Posted by GLOBAL on October 22, 2013 at 8:00am

MWANDISHI1.jpg

Na Mwandishi Wetu

HUDUMA za afya nchini Tanzania ni wasiwasi jumlisha majanga, wapo madaktari wasio waaminifu wanaocheza na maisha ya wagonjwa, miili ya Watanzania ikichokonolewa na kupasuliwa bila sababu.

Dk.HusseinMwinyi.jpg

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi.

Kitengo cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) cha gazeti hili, kilipata malalamiko kwamba kwenye hospitali nyingi binafsi, wapo wanaopewa magonjwa ambayo hawana ili wapunwe pesa bure. OFM kilipofanyia kazi tatizo hilo, kilijiridhisha pasipo chembe ya shaka kwamba mchezo huo upo na umeenea kwa kiwango kikubwa, kwani hata mwandishi wetu aliyejifanya mgonjwa ili kubaini ‘uhuni' huo, nusura apasuliwe tumbo.

Awali, mama wa Kitanzania, Mary-Stella Maulid alitoa malalamiko yake OFM: "Sikuwa na tatizo la appendix (appendicitis au kidole tumbo), pale … (anataja jina la hospitali moja binafsi Dar es Salaam), waliniambia nina appendix.

"Waliniambia natakiwa kufanyiwa oparesheni haraka. Nilimpigia simu mume wangu, akaja pale hospitali, akanipeleka Muhimbili (hospitali ya taifa), alisema haziamini hospitali binafsi kwa oparesheni.

"Pale Muhimbili nikapimwa tena lakini majibu yalipotoka yalionesha sikuwa na appendix, isipokuwa nilikuwa na matatizo katika mfuko wa uzazi, nikapelekwa kwa mtaalamu wa mambo ya uzazi (gynecologist) ambaye alinisaidia sana.

OFM KAZINI

Oktoba 16, mwaka huu, OFM ilimtuma mwandishi wa kike kwenda katika hospitali iliyotajwa na Mary-Stella ili kujiridhisha, hali ilikuwa hivi;
Mwandishi akijifanya anaumwa sana, alikuwa akitembea kwa kuinama, akilalamikia maumivu ya tumbo.

Saa 4:45 asubuhi alifika hospitalini hapo, akapokelewa na muuguzi mwanamke mwenye umri wa makamo ambaye alimsaidia kumpeleka mapokezi ambako rekodi zake ziliandikwa kisha akapewa kadi yenye namba ya faili lake.
Baada ya hatua hiyo, mgonjwa-mwandishi alisaidiwa kupelekwa kwenye chumba cha daktari ambako baada ya kujieleza, daktari aliagiza akafanyiwe kipimo cha Ultrasound ambacho gharama yake ni shilingi 30,000 kwa bei ya hospitalini hapo.
Kabla ya kuingia chumba cha ultrasound, mwandishi-mgonjwa, alitakiwa kunywa maji kiasi kisichopungua lita moja, baada ya kutekeleza hilo, aliingizwa kwenye kipimo.

UTANI UKAANZA

Majibu ya ultrasound katika hospitali hiyo, yalionesha kwamba mwandishi wetu hana tatizo la appendix lakini daktari akasema: "Utakuwa na tatizo la appendix, ultrasound haioneshi lakini ngoja nikupime zaidi."
Daktari huyo (jina linahifadhiwa) akaanza kufanya kazi ‘manyuali', akimshika mwandishi-mgonjwa kwa mikono, akipapasa sehemu ya tumbo kwa chini kisha akaibuka na jibu: "Ni appendix kabisa, inabidi tukufanyie oparesheni."
Aidha, daktari alimtaka mwandishi-mgonjwa atoe shilingi 600,000 ili afanyiwe oparesheni ya kuondoa kidole tumbo.
Hata hivyo, mwandishi-mgonjwa alisema hana fedha, kwa hiyo akaomba apewe muda na angerudi siku iliyofuata ambapo daktari akiwa na macho makavu, alimruhusu.

MWANDISHI MPAKA MUHIMBILI

Kwa mtindo uleule, mwandishi wetu akijifanya hawezi kutembea vizuri, alikwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili, Oktoba 17, mwaka huu na kufanikiwa kuonana na daktari (jina kapuni).
Daktari huyo baada ya kumsikiliza mgonjwa, alimwambia arudi Oktoba 28, mwaka huu (yaani siku 11 baadaye) ndipo atafanyiwa ultrasound.
Katika cheti cha mwandishi wetu, daktari alimwambia kuwa siku hiyo arudi na maji lita moja, tishu (makaratasi) na afike hospitali saa 2.00 asubuhi.

MWANDISHI AKUNA KICHWA

Majibu ya daktari Muhimbili yalimfanya ajiulize: "Mtu unaumwa tumbo hata kutembea huwezi, unaambiwa urudi nyumbani mpaka Oktoba 28, yaani siku 11 baadaye, je, appendix ikipasuka nikifa?"
Mwandishi aliwaza na kuwazua kisha akaenda Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu Muhimbili (Moi) ambako alipokelewa na kupimwa ultrasound chapchapu kwa gharama ya shilingi 40,000.
Majibu ya Moi kama yanavyoonekana ukurasa wa kwanza, ilibainika hana appendix na daktari alishauri afanyiwe CT Scan ili kama kuna tatizo lingine tumboni lionekane.

NINI CHA KUJIFUNZA?

Hali ni mbaya nchini hususan kwenye Jiji la Dar es Salaam kwa sasa, ni wazi kwamba kama Mtanzania asipokuwa mwangalifu, anaweza kufanyiwa oparesheni bila sababu ili mradi watu wapate pesa!
Uchunguzi wetu umebaini kuwa wetu wengi katika hospitali binafsi wanaingiwa na tamaa mbaya ya fedha, kiasi cha kucheza na maisha ya watu.

"Wengi wameshafanyiwa oparesheni wakati haikuhitajika wafanyiwe. Mtu anachanwa tumbo halafu anashonwa, anaambiwa amekatwa appendix wakati siyo kweli, kuna utapeli mwingi katika baadhi ya hospitali binafsi," alisema Mary-Stella.
Wakati Watanzania wakitendewa hayo, hali halisi inaonesha kwamba serikali yao haijui chochote.
Uchunguzi zaidi unaonesha kuwa hospitali binafsi zimekosa udhibiti kiasi kwamba zinachaji bei kubwa utadhani huduma za afya ni anasa na siyo mahitaji ya lazima kwa binadamu.

Imebainika kuwa katika baadhi ya hospitali binafsi, madaktari wake ambao mara nyingi ni waajiriwa wa muda (part-time), wamekuwa wakitumiwa na wamiliki wa hospitali hizo kuwakamua wagonjwa fedha nyingi katika vipimo na matibabu yasiyo ya lazima ili kuingiza fedha.
"Hali ni mbaya sana, imefikia madaktari wanamwandikia mgonjwa vipimo vingi bila sababu lengo likiwa ni kumfanya alipe fedha nyingi ili mradi wao wamechukua sehemu ya malipo hayo," alisema Anania Bella wa Sinza Mori, Dar es Salaam.
Aidha, OFM imebaini kuwa hata pale daktari anapofahamu mgonjwa wake ana ugonjwa fulani mfano, malaria, badala ya kupima kwanza damu ili ijulikane, atamwandikia lundo la vipimo kama widal test (typhoid), kipimo kikubwa cha damu (full blood picture) na mkojo, ili mradi alipe pesa nyingi.

Muuguzi mmoja wa Muhimbili mwenye moyo wa uzalendo (jina tunalo) alisema: "Kinachosikitisha zaidi ni pale mgonjwa anapokuwa anaumwa tumbo, ataandikiwa vipimo vingi vikubwa vya gharama kubwa kama ultrasound ambayo hugharimu shilingi 20,000 mpaka 50,000, CT-Scan shilingi 300,000 na MRI (magnetic resonance imaging) shilingi 450,000."
Aliongeza kuwa hali huwa mbaya zaidi pale mgonjwa huyo anapolipiwa na bima, kwani gharama hufanywa karibu mara mbili ya bei anayotozwa mgonjwa anayelipa taslimu sababu inayolipa ni serikali.
"Kwa huu mwendo na kama serikali haitafanyia kazi hili, huko mbeleni tunaweza kushuhudia NHIF (Mfuko wa Bima ya Taifa) ikifilisika.

"Tujiulize, kwa nini kama mgonjwa anaumwa tumbo ili kumpunguzia gharama usimfanyie kwanza ultrasound, usipopata jibu ndipo umfanyie CT-Scan nayo isipoonesha majibu ndipo umfanyie MRI?" anahoji muuguzi huyo.
Taarifa za kusikitisha zaidi zimedai kwamba baadhi ya hospitali jijini zimekuwa zikiwalazimisha wagonjwa kufanyiwa oparesheni hasa za uzazi ambazo hutozwa hadi shilingi milioni mbili ili tu ziingize pesa, wakati wahusika wanaweza kujifungua kwa njia ya kawaida.

MAJANGA MENGINE

Gazeti hili linazo taarifa pia kwamba vifaa katika hospitali za serikali huharibika mara kwa mara kwa sababu ya hujuma ili wagonjwa waende hospitali binafsi.
Nesi aliyejitaja kwa jina la Subi wa hospitali moja binafsi inayomilikiwa na watu wenye asili ya Bara la Asia, alisema: "Huoni siku hizi watu maskini wanakuja hapa kupima? Muhimbili, Mwananyamala na hata Amana wanawaambia waje huku.
"Daktari ambaye anamleta mgonjwa kupima huku anapata kamisheni. Vilevile tambua kwamba madaktari haohao wa hizo hospitali ndiyo hufanya hapa na kwenye hospitali nyingine binafsi kwa part-time," alisema Subi.

SERIKALI INASEMAJE?

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi, (pichani) alipoulizwa kuhusu skendo hii alijibu: "Hayo mambo siwezi kujibu sasa, labda mpaka mniandikie maswali halafu niwasiliane na vitengo vinavyohusika."

MWANDISHI:
Mheshimiwa, kuna hili hata la bei, hizi hospitali binafsi mbona zinachaji bei kubwa utafikiri kutibiwa ni anasa?
DK. MWINYI: Hilo pia siwezi kujibu, kuna vitengo vinavyohusika.

MWANDISHI:
Wewe ni waziri mwenye dhamana, je, huna mpango wa kuweka sheria ya udhibiti wa bei kwenye hospitali binafsi? Mbona Ewura wanadhibiti bei za mafuta japo ni soko huria?
DK. MWINYI: Niandikie maswali halafu niletee nitashughulikia.

MWANDISHI:
Na hawa Watanzania si wataendelea kupasuliwa na kutibiwa magonjwa ambayo hawaumwi kwa sababu watu wanataka pesa?
DK. MWINYI: Haya mambo yapo katika vitengo, nitayajibu kwa pamoja baada ya kunipa maswali na kuwaita wahusika.

Sitetei quacks.

Lakini pia.

Madaktari wanajifanya wanajua kuliko wanavyojua dunia nzima, si Tanzania tu.

Na kuna a whole branch of (western) medicine that lost the ideas battles a couple of hundred years ago that is not even taken seriously.

Wamarekani kwa mfano (I live in America and follow them a lot, so you will excuse my constant American references, plus they are some sort of trendsetters so it is not wholly unwarranted) Wamarekani wana matatizo sana katika huduma zao za afya, na moja ya matatizo haya ni la madaktari kutaka kufanya tests na procedures zisizo na lazima.

Tofauti ni kwamba wao wana mfumo wa sheria na muamko wa jamii kuhusu sheria hizi kiasi kwamba daktari akikosea anaweza kushtakiwa na kulipishwa hela nyingi au hata kukatazwa kuendeleza udaktari wake (revocation of license).

Which is a double edged sword, since it tends to make them edgy and have them hedge their chances with a lot of insurance costs which drive up health care costs.

Sisi unaweza kuua watu day in day out ukaendelea kudunda.

On the whole, naona investigative journalism, however crude, inaanza ku take shape.
 
Hii study yenu ni hovyo. Mojawapo ya 'tools' zinazomwezesha daktari kufikia decision ni dalili. Sasa wewe umeonyesha dalili zote ziwe feki au si feki za maumivu yanayofanana na mtu mwenye appendicitis, then Dr akataka akufanyie operesheni then unamlaumu. Huyo mwandishi amezoea kwenda kwa waganga wa kichawi ambapo diagnosis inasaidiwa na mizimu. Hospitalini dalili na vipimo ndio vinatumika. Inawezekana operesheni aliyotaka Dr ni explorative laparotomy ambapo katika upasuaji angejua hasa ni nini kinakupa maumivu hadi huwezi kutembea...
 
Hii ni point nzuri sana. Hata mimi nimeifikiria, nikaiona kama mapungufu kwa upande wa waandishi.

Unapompa daktari habari ambazo si sahihi, huwezi kutegemea kwamba tiba itokayo kwake iwe sahihi.

Ndiyo maana ulimwengu mzima sasa hivi, madaktari wanaondoka kutoka kwenye tiba inayotegemea maelezo ya mgonjwa. Kuumwa kwa kichwa kwa namna moja kunaweza kuelezewa tofauti na watu wawili tofauti, unaweza kuuliza "kichwa kinauma sana au kidogo? mbele au upande?" na ukapewa majibu tofauti na watu wawili tofauti wanaoumwa sawa.Wengine kile kitendo cha kuulizwa na daktari tu kinaharibu uwezo wao wa kuelezea hali vizuri.

Kwa hiyo huduma za afya za kisasa zinaondoka katika kutegemea maelezo ya mgonjwa na kuelekea zaidi katika uchunguzi wa vipimo zaidi.

Nakumbuka Upanga kulikuwa na mama mmoja wa kihindi, alikuwa na matatizo ya akili mengi tu, lakini mojawapo lilikuwa "hypochondria". Huyu mama alikuwa akiitwa Rabia, basi watoto walikuwa wanamsema "Rabia chaafu" akisikia hivyo analia.

Rabia muda wowote alikuwa anajisikia kwenda hospitali na kupigwa sindano. Hajisikii raha bila kupigwa sindano. Kwa sababu kila mara anaamini yeye ni mgonjwa na akipigwa sindano itamsaidia. Sasa huyu ni extreme case. We all all susceptible to a certain degree of hypochondia. Ni kazi ya madaktari kujua ni nani anaumwa kweli na kuhitaji dawa (achilia mbali sindano na operesheni) na nani ana matatizo ya saikolojia tu.

Hapa ndipo vipimo vinapokuja. Daktari ameapa above all, kutoka Hippocratic oath to Declaration of Geneva kutoleta tatizo pale ambapo hakuna tatizo.

Sasa ikiwa mtu hana tatizo, umempima ukaona hana tatizo, hizi habari nyingine zinatoka wapi?

Ni uroho wa pesa tu kutaka kumkata mtu asiye na tatizo ili alipe?

Au ni quackery ya kutofuata vipimo na kufanya modern medicine yenye vipimo vya kisayansi iwe sawa na impulsive medieval bleeding?
 
Huyu mwandishi angepasuliwa tu.>75% ya ugonjwa ni kwa maelezo ya mgonjwa,kumwangalia na kumshika.Hivyo vipimo ulivyotaja ni visaidizi tu.Vijijini/wilayani hakuna vipimo ulivyovitaja au hakuna wataalam wake,madaktari wanategemea maelezo ya mgonjwa.Hakuna ramli hospitalini.Mwandishi amezoea kwa sangoma.
 
Hii study yenu ni hovyo. Mojawapo ya 'tools' zinazomwezesha daktari kufikia decision ni dalili. Sasa wewe umeonyesha dalili zote ziwe feki au si feki za maumivu yanayofanana na mtu mwenye appendicitis, then Dr akataka akufanyie operesheni then unamlaumu. Huyo mwandishi amezoea kwenda kwa waganga wa kichawi ambapo diagnosis inasaidiwa na mizimu. Hospitalini dalili na vipimo ndio vinatumika. Inawezekana operesheni aliyotaka Dr ni explorative laparotomy ambapo katika upasuaji angejua hasa ni nini kinakupa maumivu hadi huwezi kutembea...

Kipimo husika c kimetumiwa? Kwa nn utumie fikra zako zaid?
 
Sioni makosa kwa madaktari wote wawili. Huyu mwandishi anafikiri kwamba madaktari wana rely kwenye kipimo cha aina moja tu. Daktari wa muhimbili was very clever. Alishtuka kuwa anapewa maelezo fake na ndo maana aliona kuwa ampe mgonjwa siku kadhaa kwanza ili aone kama tatizo linaendelea ndo aanze mchakato wa tiba.
 
Duu hili gazeti la kijinga sana. Sasa wamemtuma mwandishi akatoe tarifa za uwongo kwa daktari?

Hawa madaktari wana akili sana, wote wmekuja na majibu sawa bada yaa kuona dalili sawa. Usifikiri daktari hutegemea vipimo tuu, hata dalili ni clue kubwa ya kujua mgonjwa ana tatizo gan.
 
Dalili hazipimiki?

Stop clowning.

Siku hizi watu wanapima hata ubongo, wanaanza kuacha kuangalia "dalili" katika magonjwa ya akili.

Itakuwa hiyo habari ya appendicitis? Which is not much a difference from glorified dentistry.
 
Hii study yenu ni hovyo. Mojawapo ya 'tools' zinazomwezesha daktari kufikia decision ni dalili. Sasa wewe umeonyesha dalili zote ziwe feki au si feki za maumivu yanayofanana na mtu mwenye appendicitis, then Dr akataka akufanyie operesheni then unamlaumu. Huyo mwandishi amezoea kwenda kwa waganga wa kichawi ambapo diagnosis inasaidiwa na mizimu. Hospitalini dalili na vipimo ndio vinatumika. Inawezekana operesheni aliyotaka Dr ni explorative laparotomy ambapo katika upasuaji angejua hasa ni nini kinakupa maumivu hadi huwezi kutembea...

Kwa maelezo yako kama wewe ni Daktari, basi ni sawa ukiitwa Dr. Majanga. Yaani ukiwa na dalili zote lakini kipimo hakionyeshi, basi chukua kisu pasua, funua na katakata mwili ili kuutafuta ugonjwa! Huu ni zaidi ya uganga wa jadi.

Ila huko ndo Tanzania tulikofika, bora tubinafsishe Uraisi kwa wachina, kwa sababu uchakachuaji umeanzia kwa Urais, wabunge, mawaziri na elimu feki, madokta feki, mapolisi feki, usalama wa taifa feki, walimu feki, madereva feki, na sisi wananchi ni feki tu kwa sababu tunafanyiwa ufeki hatuchukui hatua za maana!
 
Sio siri mwandishi mchunguzi ana mapungufu kichwani, appendicitis inatambuliwa kwa maumivu aliyonayo mgonjwa na signs wakati wa kumpima. Sasa kama mtu anaona dalili zote ni appendicitis hawezi kutegemea ultrasound ambayo siku zote haiioni appendix asilimia zote. Angeenda anafeki amevunjika mguu wakati haujavunjika kama angewekewa POP tungesema kweli, lakini kwa soft tissues hakuna cha uhakika.
 
jamani appendicitis kwa ultra sound ni ngumu kuonekana na inahitaji expert radiologist kugundua unless iwe ni appendicular abscess so mara nyingi sign and symptoms ndo zinatumika kufika diagnosis.hilo la malaria kumbuka symptom zake ni sawa na infection zingine ndo maana unapimwa b/s,widal n.k.kumbuka ukipimwa malaria peke yake ikaonekana neg then upime widal then mkojo ni time wasting na utaishia kukaa hospitali siku nzima na utalalamika umecheleweshewa huduma.kuhusu vipimo vyenye gharama nakubaliana na huyo nesi aliyesema uanze na ultrasound then ct kama u/s haijaonesha tatizo.watanzania wengi hawaaziamini govt hosp but they are really good na gharama za uhakika kuluko private.
 
SOMENI ALAMA ZA NYAKATI MWISHO WA DUNIA HUO!!! Hapendwi mtu bali pesa!
 
Hii study yenu ni hovyo. Mojawapo ya 'tools' zinazomwezesha daktari kufikia decision ni dalili. Sasa wewe umeonyesha dalili zote ziwe feki au si feki za maumivu yanayofanana na mtu mwenye appendicitis, then Dr akataka akufanyie operesheni then unamlaumu. Huyo mwandishi amezoea kwenda kwa waganga wa kichawi ambapo diagnosis inasaidiwa na mizimu. Hospitalini dalili na vipimo ndio vinatumika. Inawezekana operesheni aliyotaka Dr ni explorative laparotomy ambapo katika upasuaji angejua hasa ni nini kinakupa maumivu hadi huwezi kutembea...

Lakini akikuta hamna tatizo la appendicitis atamwambia mgonjwa ukweli?

Mbona yule aliyefanya operesheni ya Kichwa aliandika na report kabisa kwamba tatizo wameliona na limetibiwa badala ya kuandika kwamba amefanya operation ila hakukuta hilo tatizo.
 
jamani appendicitis kwa ultra sound ni ngumu kuonekana na inahitaji expert radiologist kugundua unless iwe ni appendicular abscess so mara nyingi sign and symptoms ndo zinatumika kufika diagnosis.hilo la malaria kumbuka symptom zake ni sawa na infection zingine ndo maana unapimwa b/s,widal n.k.kumbuka ukipimwa malaria peke yake ikaonekana neg then upime widal then mkojo ni time wasting na utaishia kukaa hospitali siku nzima na utalalamika umecheleweshewa huduma.kuhusu vipimo vyenye gharama nakubaliana na huyo nesi aliyesema uanze na ultrasound then ct kama u/s haijaonesha tatizo.watanzania wengi hawaaziamini govt hosp but they are really good na gharama za uhakika kuluko private.

Hatanzania hawapendi kwenda private hospitals ndugu yangu tatizo huko serikalini sometimes Yes sometimes NO.

Kwanini niende Muhimbili nikapoteze muda wakati najua kipimo cha ultra sound wataniambia niende Regency?
 
Kwa maelezo yako kama wewe ni Daktari, basi ni sawa ukiitwa Dr. Majanga. Yaani ukiwa na dalili zote lakini kipimo hakionyeshi, basi chukua kisu pasua, funua na katakata mwili ili kuutafuta ugonjwa! Huu ni zaidi ya uganga wa jadi.

Ila huko ndo Tanzania tulikofika, bora tubinafsishe Uraisi kwa wachina, kwa sababu uchakachuaji umeanzia kwa Urais, wabunge, mawaziri na elimu feki, madokta feki, mapolisi feki, usalama wa taifa feki, walimu feki, madereva feki, na sisi wananchi ni feki tu kwa sababu tunafanyiwa ufeki hatuchukui hatua za maana!
Tatizo ni kwamba tunajadili issue ya kitaalam kishabiki au kisiasa!
As far as I know, sometyms dr anaweza decide kufanya explorative laparatomy (upasuaji kutafuta tatizo) kama anaona majibu ya vipimo ni inconclusive ukilinganisha na complain ya mgonjwa! So daktari alikua sahihi, swali ni kwamba huyo muandishi wa tukio hili anaufaham hata kidogo kuhusu medicine? Kama hafahamu basi ni mpuuzi kabisa na atutolee ujinga wake hapa
 
Back
Top Bottom