Mudathir afundishwe namna ya kupiga mashuti huyu dogo ni chatu

OMOYOGWANE

JF-Expert Member
Dec 30, 2016
3,647
9,233
Pengine huenda ndio maana GAMOND hapend kumtumia huyu bwana mdogo tangu nimjue kila shuti analopiga huenda juu usawa wa paa la mkapa ila kiufundi namfananisha na chatu ambaye huwa anatabia ya kubana sehemu na kuvizia kitoweo kijisahau kisha kukivamia haraka na kukimezea huyu jamaa anakipaji cha kukaba na kupokonya mipira kwa haraka kama upepo
 
Umesema vyema. Jamaa hata hivo anaweza sana akicheza no 6. Kule mbele kwa akina Aziz Ki hapawezi. Shuti anapiga kama hana macho
 
Ni mchezaji wa kawaida tu sema mmeamua kumuimba sana. Mara zote huwa anakimbiakimbia tu na kujitahidi kukaba. Ni kiungo ambaye anapiga pasi nyuma na pembeni mara nyingi kuliko mbele, si dribbler mzuri, hajui kushoot, hajui kutengeneza nafasi za magori na si mzuri wa kupiga pasi.
 
Pengine huenda ndio maana GAMOND hapend kumtumia huyu bwana mdogo tangu nimjue kila shuti analopiga huenda juu usawa wa paa la mkapa ila kiufundi namfananisha na chatu ambaye huwa anatabia ya kubana sehemu na kuvizia kitoweo kijisahau kisha kukivamia haraka na kukimezea huyu jamaa anakipaji cha kukaba na kupokonya mipira kwa haraka kama upepo
Akicheza Mara kwa Mara atarekebisha namna ya kupiga mashuti .
Kuna mechi ya nbc hivi karibuni alifunga kwa shuti .
Kuna mechi ya Tp Mazembe nabi alimtumia namba 10 akafunga goli zuri sana kwa shuti .
 
na jana umeona?
 
Pengine huenda ndio maana GAMOND hapend kumtumia huyu bwana mdogo tangu nimjue kila shuti analopiga huenda juu usawa wa paa la mkapa ila kiufundi namfananisha na chatu ambaye huwa anatabia ya kubana sehemu na kuvizia kitoweo kijisahau kisha kukivamia haraka na kukimezea huyu jamaa anakipaji cha kukaba na kupokonya mipira kwa haraka kama upepo
kweli kama alivyonipenyeza jana nikashangaa Simu inapigwa nikajua tyr Dogo ashafanya yake...
 
Back
Top Bottom