Wallahi ningekuwa na mimba nikajifungua mtoto wa kiume angeshapata jina "Muntadar al-Zeidi" lakini no sweat hata mjukuu lazima nitampa jina .. kumbukumbu nzuri .. kweli kamdharau maana kiatu hata maliwatoni kinafika .. this one is added on my list of heroes
Hahahahahaa angekuwepo mtume mwamedi hapa aya ingeshuka
Ila kichaka kweli kamanda umeona alivyokwepa naamini wangekuwa viongozi wetu lazima angetoka ngeu
Nilifikiria hili pia nami, nikaimagine kama viatu vile angerushiwa fisadi Mkapa! Am sure saa hizi angekuwa anauguza ngeu tu na kuskilizia maumivu! Mtambi ule na magoti mabovu ukichanganya na zero fitness afu juu yake uongezee makonyagi ya kila siku??? NO CHANCE!
Heya Kana-Ka-Nsungu long time mkuu, where were you mkuu? Hata hivyo karibu sana jamvini
Njimba
Bush might be a lame duck lakini kwenye hii ducking nampa +5 kumaintain his coolness under fire now that is a commander in chief.
Kikwete alipandishwa jukwaani na kuketishwa kwenye kigoda. Wakati shughuli hiyo ikiendelea, ndipo kijana aliyekuwa amevalia mgolole mweusi, alipomvamia Kikwete na kuukumbatia mguu wake wa kulia akitaka kumdondosha chini kutoka jukwaani alipokuwa ameketi kwenye kigoda!
Kutokana na ushupavu wake, Kikwete aliweza kujinasua kutoka mikononi mwa yule kijana, na wakati huo huo ndipo kijana huyo aliposhukiwa na kundi la zaidi ya askari 30 waliokuwa wamezunguka jukwaa alilokuwepo Kikwete.
Kusema kweli, kitendo hicho kilitokea katika muda wa sekunde chache, kiasi kwamba wapo baadhi ya watu waliokuwemo uwanjani humo hawakujua nini kilichokuwa kimetendeka.
source;Kutoka Geita hadi Mahenge bila kulala
RAIS George W. Bush juzi alikumbana na mushkeli mkubwa wakati wa ziara yake ya kuaga nchini Iraq wakati mwandishi mmoja alipomrushia kiatu mara mbili katika mkutano na waandishi wa habari huku akimwita "mbwa" kwa kutumia maneno ya Kiarabu.
Mara zote mbili, Bush alimudu kukwepa kiatu katika tukio hilo lililotokea wakati rais huyo wa Marekani anayemaliza muda wake akizungumza na waandishi akiwa amesimama pamoja na mwenyeji wake, Nuri al-Maliki, ambaye ni waziri mkuu wa Iraq.
Mwandishi huyo alikuwa na shabaha lakini alirusha juu kidogo ya Bush, aliyeinama mara zote mbili, kwa mita 4.5 na hivyo kushindwa kuupata vizuri uso wa kiongozi huyo wa taifa kubwa duniani.
Kiatu cha kwanza kilipita juu ya kichwa cha Bush na cha pili kilimbabatiza mwandishi aliyekuwa jirani yake na hivyo kumkosa Bush, huku Waziri Maliki aliyekuwa pembeni yake akionekana kufedheheka na Bush akitabasamu.
"Hiyo hainikeri," alisema Bush huku akimsihi kila mmoja kutulia wakati walinzi wake na wana usalama wakimshughulikia mwandishi huyo.
Alipoulizwa kuhusu tukio hilo muda mfupi baadaye, Bush alifanya mazaha akisema: "Sikujisikia kutishika hata kidogo."
Waandishi wengine wa Iraq waliomba radhi kwa niaba ya mwandishi mwenzao aliyefanya shambulio hilo.
Mrushaji wa viatu hivyo, aliyetambulika kama Muntadhar al-Zaidi, mwandishi raia wa Iraq anayeripoti kwenye televisheni ya al-Baghdadia yenye makao yake makuu nchini Misri-- alisikika akisema kwa Kiarabu: "Hii ndiyo kwa heri ... mbwa wee!"
Akiwa amekunjwa sakafuni na watu wa usalama, alikuwa akipiga kelele akisema: "Uliua Wairaqi!"
Mwandishi huyo Al-Zaidi aliondolewa kwenye chumba hicho kilichokuwa na ulinzi mkali. Wakati al-Zaidi alikuwa akiendelea kupiga kelele kwenye chumba kingine, Bush alisema: "Hicho kilikuwa kiatu cha saizi 10 kilichorushwa kwangu, mnaweza kutaka kujua."
Kumrushia kitu mtu, au kukaa kwa jinsi ambayo soli ya kiatu inaelekea kwa mtu mwingine, huchukuliwa kama matusi kwa Waislamu.
Televisheni ya Al-Baghdadia ilitoa taarifa Jumapili ikitaka al-Zaidi aachiwe huru.
Al-Zaidi alisikika sana ulimwenguni Novemba mwaka 2007 wakati alipotekwa wakati akielekea kazini katikati ya Baghdad. Aliachiwa huru siku tatu baadaye.
Bush alirushiwa kiatu hicho wakati akisifia kusainiwa kwa mkataba wa amani na Iraq mbele ya waandishi.
"Kwa hiyo kuna kitu gani kama mtu ananirushia kiatu?" Bush alimwambia mwandishi akijibu swali kuhusu tukio hilo.
"Ngoja niwaambie kuhusu mtu aliyerusha kiatu chake. Ni njia mojawapo ya kutaka umaarufu. Ni kama kwenda kwenye mkutano wa kisiasa na kufanya watu wakuzomee. Ni kama kuendesha gari mitaani na kusababisha watu wasikupungie mkono wakichanua vidole vyote vitano. ...
"Hawa waandishi hapa walikerwa sana. Walisema ... huyu mwandishi hawakilishi watu wa Iraq, lakini hayo ndiyo yanayotokea kwenye jamii zilizo huru ambako watu hujaribu kufanya wengine wawaangalie."
Baadaye Bush aliendelea na mazungumzo yake ya mkataba wa amani, ambao yeye na al-Maliki walikuwa wakijiandaa kusaini, akiusifia kama ni "mafanikio makubwa", lakini akionya kuwa "kuna kazi kubwa zaidi ya kufanya".
Lakini al-Zaidi alikuwa akihojiwa kama kuna mtu yeyote aliyemlipa ili amrushie Bush kiatu na alikuwa akipimwa kama alitumia dawa za kulevya au alikunywa pombe, kwa mujibu wa afisa aliyekataa kutaja jina lake.
Mwandishi huyo wa dhehebu la Shiite ambaye umri wake ni kwenye miaka ya ishirini, alikuwa ameshikiliwa kwenye ofisi za makao makuu ya Waziri Mkuu.
Hiyo ni mara ya mwisho kwa Bush kwenda eneo hilo la vita kabla ya Rais Mteule Barack Obama kuchukua ofisi Januari
Reuters reports that Muntadhar al-Zeidi will be given an award by a Libyan charity group called Wa Attassimou.
"Waatassimou group has taken the decision to give Muntazer al-Zaidi the courage award ... because what he did represents a victory for human rights across the world," the group, headed by Aicha Gaddafi, said in a statement.
The group said the Iraqi authorities should honour the journalist for his actions.
Zaidi, accused by the Iraqi government of a "barbaric and ignominious act" will be tried on charges of insulting the Iraqi state, said the Iraqi prime minister's media advisor, Yasin Majeed.
Journalist Muntadhar al-Zeidi, who was kidnapped by militants last year, was being held by Iraqi security Monday and interrogated about whether anybody paid him to throw his shoes at Bush during a press conference the previous day in Baghdad, said an Iraqi official.
He was also being tested for alcohol and drugs, and his shoes were being held as evidence, said the official, speaking on condition of anonymity because he was not authorized to talk to the media.
Showing the sole of your shoe to someone in the Arab world is a sign of extreme disrespect, and throwing your shoes is even worse. Iraqis whacked a statue of Saddam with their shoes after U.S. Marines toppled it to the ground following the 2003 invasion.