Mtwara: Mama amchoma Mtoto baada ya kula Ugali Nyama uliohifadhiwa kwa ajili ya Bibi yake

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,282
Mtwara. Mtoto Akashe Wahabi (8) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la pili Shule ya Msingi Naliendele ameunguzwa mkono na mama yake mzazi Muwaza Abeid( 29) kwa madai ya kuiba ugali na nyama.

Ofisa ufuatiliaji na tathmini wa kituo cha msaada wa sheria Mtwara Manispaa, Judith Chitanda amelieleza Mwananchi Digital leo Julai 19, 2021 kuwa mtoto huyo aliunguzwa Julai 3, mwaka huu kisha mama yake akamficha ndani huku akimpa matibabu ya kienyeji.

"Nilipata taarifa za mtoto huyu kuunguzwa Julai 18, mwaka huu kidonda kikiwa na siku 16 na hakiko katika hali nzuri," amesema Judith.

Ameeleza kuwa baada ya kumuhoji mama Akashe ameeleza kuwa siku ya tukio mtoto alikula ugali na nyama ambao alikua amewekewa bibi yake aliyekuwa ameenda shamba.

Amesema bibi aliporudi hakukuta chakula walipouliza ndipo Akashe alikiri kuwa yeye ndie aliyekula chakula cha bibi yake.

Baada ya kukiri mama alimfunga mtoto mikono yake yote miwili kwa kutumia majani ya mnazi.

Baada ya kumfunga akachukua moto na kuanza kumtishia ndipo mtoto alipoanguka na majani ya mnazi yaliposhika moto na kumuunguza mkono wa kulia.

Mama Akashe ambaye muda wote alikuwa akilia ameomba jamii imsamehe kwa vile hakutegemea kwamba mtoto wake anaweza kuungua kiasi hicho.

"Najuta mimi sikutegemea kabisa kwamba mtoto wangu anaweza kuungua hivi, sikudhamiria kumuumiza hivi mtoto wangu ni mtundu mno na amekuwa akidokoa dokoa hata hela,"

Amesema siku ya tukio mtoto huyo alitoka kwa shangazi yake akiwa ameshakula chakula cha mchana lakini kwa vile mtoto wake ana tabia za udokozi aliamua kudokoa chakula.

Mwananchi
 
Matukio ya ukatili yamezidi Sana
Lazima jamii ichukue hatua za dhati
Kweli yamekithiri mapema Julai mwaka huu katika mtaa wetu Kuna mama alimfungia mtoto wa miaka 10 kwenye kisalfeti kwa muda wa siku 3.
Kwa kweli tukio hili lilitusikitisha.Sisi tulichukua hatua kwa kuzitaarifu mamlaka husika na tunafuatilia kwa karibu kujua nini kinaendelea.
 
Mtwara. Mtoto Akashe Wahabi (8) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la pili Shule ya Msingi Naliendele ameunguzwa mkono na mama yake mzazi Muwaza Abeid( 29) kwa madai ya kuiba ugali na nyama.

Ofisa ufuatiliaji na tathmini wa kituo cha msaada wa sheria Mtwara Manispaa, Judith Chitanda amelieleza Mwananchi Digital leo Julai 19, 2021 kuwa mtoto huyo aliunguzwa Julai 3, mwaka huu kisha mama yake akamficha ndani huku akimpa matibabu ya kienyeji.

"Nilipata taarifa za mtoto huyu kuunguzwa Julai 18, mwaka huu kidonda kikiwa na siku 16 na hakiko katika hali nzuri," amesema Judith.

Ameeleza kuwa baada ya kumuhoji mama Akashe ameeleza kuwa siku ya tukio mtoto alikula ugali na nyama ambao alikua amewekewa bibi yake aliyekuwa ameenda shamba.

Amesema bibi aliporudi hakukuta chakula walipouliza ndipo Akashe alikiri kuwa yeye ndie aliyekula chakula cha bibi yake.

Baada ya kukiri mama alimfunga mtoto mikono yake yote miwili kwa kutumia majani ya mnazi.

Baada ya kumfunga akachukua moto na kuanza kumtishia ndipo mtoto alipoanguka na majani ya mnazi yaliposhika moto na kumuunguza mkono wa kulia.

Mama Akashe ambaye muda wote alikuwa akilia ameomba jamii imsamehe kwa vile hakutegemea kwamba mtoto wake anaweza kuungua kiasi hicho.

"Najuta mimi sikutegemea kabisa kwamba mtoto wangu anaweza kuungua hivi, sikudhamiria kumuumiza hivi mtoto wangu ni mtundu mno na amekuwa akidokoa dokoa hata hela,"

Amesema siku ya tukio mtoto huyo alitoka kwa shangazi yake akiwa ameshakula chakula cha mchana lakini kwa vile mtoto wake ana tabia za udokozi aliamua kudokoa chakula.

Mwananchi
Umaskini!!
 
Mkoa wa Mtwara ni miongoni mwa mikoa yenye Umasikini ulio topea !!
tukio kama hilo ni dalili ya umasikini ulio kithiri. kuna umasikini wa kipato na chakula.
 
Jambo hilo limechagizwa na ufukara, japo huyo mama kafanya jambo la kinyama ila ukiangalia kwa umakini utagundua kuwa bibi ndiye anayehudumia familia, huyo mama pengine alitaka kumuadhibu mtoto ili kuonyesha kwa mfadhili wake ( bibi) kuwa naye amechukizwa sana na tabia iliyooneshwa na mwanae, sasa katika kutaka kumfurahisha mfadhili wake na pengine kutuliza hasira za mfadhili, mama akaenda mbali zaidi na kufanya alichofanya.
Ufukara mbaya sana unaweza kusababisha mtu akafanya jambo la kipuuzi ambalo litaumiza wengine au kushusha thamani ya utu wake kama mwanadamu, binafsi nimemsamehe huyo mama, namwombea nae aweze kujitegemea. Pia sisi wanaume tunatakiwa kuzijali na kuzitunza familia zetu na sio kuwavika majukumu watu wengine, kwa upande mwingine baba wa mtoto huyo angekuwa anaitunza familia hiyo sidhani kama lingetokea jambo hilo, Mungu atupe uwezo wa kupata familia na nguvu ya kuzihudumia.​
 
Alikuwa katika harakati za kumtishia,pole mama mtoto ndio hivyo kashaungua...
 
Ukimpatia mtoto chakula cha kushiba vizuri hawezi kuwa mdokozi kwa asilimia kubwa. Labda I've tabia za kurithi tu
 
Back
Top Bottom