Tetesi: Mtume Mwamposa anakusanya zaidi ya Jumla Million 50 kwa ibada zote kwenye wiki 1

Nshomile wa Muleba

JF-Expert Member
Dec 5, 2015
2,165
5,551
Jambo Jambo?

Watu wanaweza kudhani pengine ni hadithi ya kusadikika lakini la hasha,Ni kweli baada ya kupokea taarifa hizi kwa mmoja wa viongozi wanaohusika na kuhesabu mtonyo.Iko hivi;

Nina Mama mdogo wangu mtu wa makamo tu (Sister mdogo kwa bi mkubwa tumbo 1) ni muumini wa Mwamposa kwa zaidi ya miaka 6 sasa kiufupi yeye ni “ZOMBIE” wa Mtume Mwamposa(Haambiwi lolote huyu juu ya mtume huyu), Alibahatika kupata nafasi za uongozi kutokana na uaminifu wake wa muda mrefu kwenye dhehebu hilo la inuka uangaze.

Sasa Majuma mawili yaliyopita nilikuwa dar es salaam kwaajili ya kucheki familia yangu na kabla sijageuka Kahama, niliaamua nipitie nyumbani kwake kumsabahi mana nilikuwa na siku nyingi hatujaonana,Nikafika na kuzugazuga hapa na pale huku tukipiga soga za hapa na pale, Wakati tukiendela na soga hizo simu ya ma mdogo ikaita (nadhani alikuwa kiongozi mwenzake wa dhehebu la mwamposa) na alipokea na kuanza kuongea maswala ya kanisa.

Lakini katikati ya maongezi yao marefu nikasikia anasema kuwa alijaza kwenye kitabu cha kumbukumbu kiasi cha Million 19 na ushee ibada ya kwanza jumapili, million 16 na ushee ibada ya tatu, Million 8 na ushee maombi ya jumatatu na million 5 na ushee maombi ya jumanne, zote zikiwa za WIKI ILIYOPITA na niliweza kuyakariri kwasababu alikuwa anarudiarudia kumuelewesha huyo anayeongea naye.

Hapo hatujapiga hesabu miamala ya simu ya kila siku kwenye maombi ya KOMBOA FAMILIA pamoja na miamala ya benki.
-Bado mauzo ya mafuta ya upako
-Bado mauzo ya vitabu vyake
-Bado mauzo ya stika zake
-Bado mauzo makaratasi ya kuandika maombi
-Bado mauzo ya maji ya upako
-Bado mauzo ya Jarida/Gazeti zake.

Oh my Goodness this guy is a Billionaire by simply exploiting the fools.

Hivi jamani mtu huyu ana uwezo wa kukusanya million zaidi ya 200 kwa mwezi ambapo kwa mwaka ni zaidi ya BILLION 2.4 ambzao hazilipiwi hata 100 mbovu ya kodi.

Na alivyomjanja hajengi kanisa bali anajenga asset zake mfano Ana hoteli yake mbeya, ana mjengo/ghorofa wake Dar na mwingine Mbeya, ana mashamba makubwa ya kisasa ya parachichi, ana magari kibao, basi la YUTONG 1, coaster 2, Hiace nyeusi za kubeba sadaka 4(imagine mtu ana gari maalum za kubebea sadaka), ana V8 3 , Radio stations nchi nzima pamoja na Tv station zote i mean zote ziko Registered under his Dominion ila upande wa pili zikiwa chini ya jina lake na mambo mengine mengine.Na hizo ndo zinajulikana zipo ambazo hatuzijui hazipo hapa.

DATA HIZI NIMEPEWA NA NDUGU HUYU ANAYESALI ZAIDI YA MIAKA 6 KWA MTUME MWAMPOSA.

THE IS THE MOST/HIGHEST GROWING BUSINESS/INVESTMENT WITH MINIMAL CAPITAL INVESTMENT BUT HAS BURSTING PROFIT IN OUR COUNTRY, THE GUY NEEDS SOME CREDIT/RECOGNITION FROM THE GOVERMNENT SERIOUSLY.

APEWE TUZO YA INNOVATION!!!

IMG_7798.jpg

Nshomile
kwasasa Kahama,Tanzania
 
Huyo ni mmoja wako wengine nao wanapiga hela kwa jina la bwana
 
Back
Top Bottom