Mtoto wa miaka 6 adaiwa kufariki baada ya umeme kukatika akifanyiwa upasuaji. Mkurugenzi asema hawana uwezo wa kufanya upasuaji wilayani humo

Mtumishiwetu

Senior Member
Jul 13, 2022
187
334
Kuna taarifa inasemekana mtoto mwenye umri unaokadiriwa kuwa kati ya miaka 6 hadi 8 amefariki dunia baada ya umeme kukatika katika Hospitali moja iliyoko Wilaya ya Mkinga Mkoa wa Tanga wakati mtoto huyo akifanyiwa operesheni.

Mtoto huyo inasemekana alikuwa anafanyiwa upasuaji mdogo kwenye Pua baada ya umeme kukatika akapoteza maisha inasemekana mzazi wa mtoto huyo ni Kiongozi wa Dini.

Tatizo la umeme sasa linagharamu maisha ya watu bila kificho huku Mbunge wa Jimbo la Mkinga ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati, Mhe Dastan Kitandula akiwa kimya wananchi wake jimboni wanakufa hospitalini kwa umeme kukatika.

Viongozi wa Mkoa wa Tanga, Wizara ya Afya fuatilieni kwa umakini taarifa hii wilayani Mkinga ili mpate ukweli na hatua ziweze kuchuliwa kwa wote waliohusika na uzembe huu.

Tunaimani kubwa na Ufuatiliaji na uwajibikaji wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Omari Mgumba, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu na Waziri wa OR- TAMISEMI, Angela Kairuki hivyo ukweli utajulikana haraka.

=====
Mkurugenzi MkingaM: MKINGA hatuna uwezo wa kufanya upasuaji

JamiiForums imefanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Wilaya ya Mkinga Mkoa wa Tanga ili kufahamu uhalisia wa tukio la kufariki kwa mtoto anayekadiriwa kuwa na miaka 6 hadi 8 kwa sababu ya kukatika kwa umeme, Mkurugenzi kakanusha kuwepo kwa Hospitali yenye uwezo wa kufanya upasuaji katika wilaya yake.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Mkinga, Zahara Msangi amesema: “Mkinga hatuna hospitali, tuna Zahanati na Vituo vya Afya, pia sidhani kama tuna kituo chenye uwezo wa kufanya oparesheni.

“Mkinga hatujawa na Hospitali ya Wilaya yenye uwezo wa kufanya operesheni kama hizo (ya pua), inawezekana aliyetoa hiyo taarifa amekosea kutaja jina la Wilaya.”
 
Back
Top Bottom