Dr. Chapa Kiuno
JF-Expert Member
- Sep 11, 2009
- 443
- 18
Mtoto wa kiume wa miaka 9 abadili jinsia kuwa mwanamke
Tuesday, September 22, 2009 3:55 AM
Baada ya mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 12 kubadili jinsia kuwa mwanamke nchini Uingereza mtoto mwingine wa kiume mwenye umri wa miaka 9 na yeye amebadili jinsia kuwa mwanamke.
Baada ya taarifa za mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 12 kuanza elimu ya sekondari akiwa amebadili jinsia yake kutolewa kwenye vyombo vya habari wiki iliyopita na kuzua mtafaruku nchini Uingereza, mtoto mwingine wa kiume mwenye umri wa miaka tisa amerudi kwenye shule yake ya msingi kutoka likizo akiwa amebadili jinsia kuwa mwanamke.
Tukio hilo pia kama lile la awali limetokea kwenye mji mmoja kusini mwa Uingereza.
Wanafunzi katika shule ya msingi anayosoma mtoto huyo wa miaka 9 waliambiwa kuwa mwanafunzi mwenzao wa kiume amehama shule na nafasi yake imechukuliwa na mwanafunzi mwingine wa kike.
Lakini wanafunzi wanaomjua vizuri mtoto huyo walirudi majumbani mwao na kuanza kuwauliza maswali wazazi wao kwanini mwenzao ameamua kuvaa nguo za kike.
"Mwanangu alirudi toka shuleni na kuniuliza kwanini rafiki yake mmoja amekuwa msichana, mwanzoni nilidhani anatania lakini aliendelea kunisumbua kwa swali hilo na kunifanya nitie shaka inaweza kuwa kweli", alisema mzazi wa mtoto mmoja katika shule hiyo.
Hata hivyo baada ya kuona wanafunzi wamegundua kuwa mwanafunzi huyo ndio yule yule wa awali ma wala hakuhama shule, walimu waliwakusanya wanafunzi wote na kuwataarifu kuwa mwanafunzi mwenzao amebadili jinsia amekuwa mwanamke na waliwataka wanafunzi wote waanze kutumia jina lake jipya la kike ambalo lilibandikwa kwenye ubao wa matangazo wa darasa lake.
Wazazi wa wanafunzi katika shule hiyo ya msingi walikasirishwa na hatua ya mwalimu mkuu wa shule hiyo kuwapa taarifa hiyo watoto wao kabla ya kujadiliana nao kwanza.
"Sijui nitajibu vipi maswali ya mwanangu wa kiume, ni mdogo sana na hajui chochote kuhusiana na masuala ya jinsia", alilalamika mmoja wa wazazi wa mwanafunzi wa shule hiyo.
"Sijui nitasemaje kama na yeye akisema kuwa anataka kubadili jinsia kuwa kama rafiki yake", alilalamika mzazi huyo.
Kitendo cha mtoto wa miaka tisa kubadili jinsia kuwa mwanamke kimechochea moto kwenye mjadala mkali uliozuka baada ya taarifa za mtoto wa miaka 12 kubadili jinsia kutolewa katikati ya wiki iliyopita.
Taarifa hiyo ilisababisha wazazi wa mtoto huyo kupewa ulinzi kutokana na vitisho vya kuuliwa walivyokuwa wakitumiwa na watu wasiojulikana wanaopinga kitendo hicho.