Mtoto mchanga aokotwa Sinza 'C' karibu na ilipo Mahakama ya Mwanzo akiwa ametelekezwa na Mama yake

Dotto Mnzava

R I P
Mar 6, 2014
865
427
Wakuu wimbi la Dada zetu/wanawake kutupa watoto wachanga na wengine kuwaua na kuwanyofoa macho bado linaendelea kujitokeza katika maeneo yetu ambapo leo kuna kuna tukio limetokea mda mfupi uliopita ambapo Mtoto mwenye jinsia ya kike anayekadiriwa kuwa na umri wa mwezi mmoja ameokotw aakiwa ametupwa na Mama yake (hajatambulika jina mara moja) katika eneo la Mahakama ya Mwanzo Sinza 'C' Jijini Dar es Salaam (Mtoto hajafa) ila amejeruhiwa kwa kiasi kidogo usoni na mbwa waliokuwa wanaranda randa nje ya eneo hilo.

Tukio hilo limetokea leo Machi 29, 2015 saa 21:30 usiku ambapo mashuhuda wa tukio wanaeleza kuwa walikiona kichanga hicho kikiwa kimetupwa nje ya geti la nyumba namba 22 inayomilikiwa na Steven Lesika ambapo kugundulika kwa tukio hilo kumekuja baada ya ya wapita njia kusikia kichanga hicho kikilia ndipo walipoto taarifa kwa mwenye nyumba.

attachment.php

Mwenye nyumba baada ya kupewa taarifa aliripoti kwa Balozi wa eneo hilo, Lucia Kaunda. Balozi aliwaandikia barua wasamaria wema ili wampeleke kwenye Kituo cha Polisi Mabatini na kufunguliwa faili lenye namba KJN/RB/3237/015.

Wasamaria wema waliochukua jukumu la kumuokoa mtoto huyo wamepewa hati ya matibabu, maarufu kwa jina la PF3, wasamaria hao hao wameambiwa na Polisi wampeleke Hospititali ya Mwananyamala.

Naambatanisha picha za tukio, kwa pamoja tuungane kuwapa elimu watu wanaokuwa na roho ngumu kwasababu mbalimbali ikiwemo ugumu wa maisha hali inayowapelekea kuwatupa watoto wao/kuwatekeleza.


attachment.php



Mashuda wa tukio hilo wakiwa katika harakati za kumepeke mtoto huyo kwenye Kituo cha Polisi Mabatini aliwa amebabwa na Hortensia Mmbando


attachment.php

 

Attachments

  • Msamaria.jpg
    Msamaria.jpg
    30.5 KB · Views: 4,630
  • Mashuhuda.jpg
    Mashuhuda.jpg
    26 KB · Views: 3,788
  • Sinza.jpg
    Sinza.jpg
    25.4 KB · Views: 3,632
Haya mambo yanaenda viseversa sana..dah nina ndugu yangu ametafuta sana mtoto miaka mitano bila mafanikio
 
Hivi hapa ina maana kazi ya kumlea huyu mtoto anaibeba nani?


Nafikiri itakuwa ni Ustawi wa Jamii, japokuwa jana niliwapa kampani hadi pale Polisi Mabatini baada ya kuchukuiwa maelezo waliambiwa wampeleke Mwananyamala Hospitali kwa ajili ya kupatiwa huduma sasa sijajua kuwa yeye anaweza kuamua kumhudumia au atawakabidhi akina nani.....
 
Nafikiri itakuwa ni Ustawi wa Jamii, japokuwa jana niliwapa kampani hadi pale Polisi Mabatini baada ya kuchukuiwa maelezo waliambiwa wampeleke Mwananyamala Hospitali kwa ajili ya kupatiwa huduma sasa sijajua kuwa yeye anaweza kuamua kumhudumia au atawakabidhi akina nani.....

Yaani hawa wanawake wanaowatupa watoto wanatakiwa wapewe adhabu kali sana maana wanawapa watu wengine kazi zisizotegemewa.
 
Mkuu Meljons sijui kama kwa hii Tanzania yetu hili jambo linaweza kufanikiwa kirahisi.....nasema hivyo kwamaana kuna masuala ya kumuangalia na yule aliyempa ujauzito.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Meljons sijui kama kwa hii Tanzania yetu hili jambo linaweza kufanikiwa kirahisi.....nasema hivyo kwamaana kuna masuala ya kumuangalia na yule aliyempa ujauzito.

Ni kweli na sababu kubwa ya haya ni baba wa mtoto anapokimbia mimba na mtoto pia. Sasa huku kwetu tatizo la kusolve kwanza ni ngono zembe zinazosababisha mimba zisizotarajiwa. Tunawalaumu hawa wanawake tu wana roho mbaya angali hata baba wa mtoto anajua mtoto wake ametupwa na hashtuki. Itatuchukua muda sana kufika tunapostahili kufika.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom