Mtoto kulala mchana

Adm

Senior Member
Sep 19, 2010
149
45
Familia nyingi kati ya zile ambazo nimebahatika kuzitembelea. Kama familia hiyo kuna watoto wenye umri kuanzia miaka 3 up to 5,pindi wanapomaliza kula chakula cha mchana utaona baba au mama anawaambia watoto wakalale. Swali langu ni kwamba KUNA SABABU GANI YA MSINGI KUWALAZIMISHA WATOTO WALALE MCHANA. Wahusika au wenye ufahamu na hili naomba wanisaidie
 
nenda google utajua faida zake,kiduchu tu ni kukuza ufahamu wa mtoto, mtoto anapolala mchana ubongo hukua vizuri, na isitoshe hata kwa akili ya kawaida mtoto chini ya miaka 7 hawezi kuwa macho saa 12,kama huna mtoto bado jifunze sasa,
 
Mtoto anakua vizuri, ubongo unakua vizuri pia. Experience niliyonayo mtoto asipolala mchana, usiku anasumbua sana atakula kwa shida na wakati mwingine hawezi kula kabisa. Lakini akilala mchana, jioni anakuwa fresh hasumbui na kesho yake asubuhi kuamka kwenda shule anakuwa hana shida kabisa tofauti na yule ambaye hajalala mchana.
 
Back
Top Bottom