Mtoto kukosa Kimeo/Kilimi

JimCarrey

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
214
124
Habari wadau..? Mim ninamtoto ametimiza mwaka siku chache zilizopita, mwanangu anatatizo la kugoma kula, najua mtasema ni kawaida ila I wish mngepata nafasi ya kumuona maana wapo waliosema ni kawaida ila baada ya kumuona wakakubali kua anautofauti.... Maana anapambana, hachoki na ananguvu za ajabu wakati wa kula,unaweza mpa uji asimeze kijiko kata kimoja na akashinda hivyo kuanzia asubuh mpaka mama ake Atoke kazini ndo anyonye, na akinyonya dakila3 hazifiki anaacha..... Sasa mke wangu amesafiri na mtoto huko walikokwenda kunasehemu walimpeleka wakamgundua kua Hana kilimi/kimeo, wanadai ndio sababu Hana afya nzuri, swali langu ni je, wapo watoto wasiozaliwa na kilimi..???? Na je, ni kilimi kinachomfanya agome kula kabisa..???? Inawezekana kuendelea na maisha bila hicho kilimi bila kuathiri chochote...???
Naomba kuwasilisha

NB: Huko waliko wanadai amepewa dawa ya kuotesha hicho kilimi
 
Back
Top Bottom