Mtikila atupwa rumande! Demokrasia itapatikana?

- Mtikila amewekwa Rumande kwa kuvunja masharti ya sheria ya dhamana yake na nothing else, nothing to do na kesi ambayo hajahukumiwa, angekua amehukumiwa then kweli tungeelewa kesi ni ya kijinga jinga, na hasa baada ya kuangaalia sheria inasema nini na kumuita Rais wa jamhuri gaidi.

Es!

well said Mkuu FMES!!! kesi ikiwa mahakamni hatuna sababu ya ku-conclude mara upinzani wanafungwa demokrasia iko wapi.... na sidhani ni busara kuanza kulaumu!!!

Mtikila angetimiza masharti ya dhamani basi angetoka asubirie kesi yake na maamuzi ya mahakama.

so far he is still innocent until proved guilt!!
 
Wapigania haki siku zote wawe tayari kupitia njia hii kwa kila sababu, iwe ina sound vizuri kwenye masikio ya maadui au la. Kwa kila sababu wote mnaopigania haki ndiko muwe tayari kupitia. Na njia hii haitawahi kuwa ya mtikila pekee maana wengi wamepitia njia hii na sababu zilikuwepo na sababu hazitakosa. Lakini ole wake adui atakapojiliwa....... kiburi kitakoma.
Siku moja mtakumbuka maneno haya.
 
Siasa ndiyo hizo!! aliyeshikilia dola si mwenzako. Mtikila ajichunge, na aepuke kutusi walio katika enzi!!
 
Ukichunguza sana sheria imefuata mkondo wake ila huyu Mchungaji alikiuka vifungu vya sheria.Sijui alifanya hivyo kwa kudhamiria au ndiyo katika kutaka kuandika historia?
 
Ikiwa magazeti yanafungiwa, na wapinzani wanarushwa jela.

Demokrasia itapatikana?


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam leo imemfutia dhamana Mwenyekiti wa Chama cha Democratic (DP), Mchungaji Christopher Mtikila.

Mtikila anakabiliwa na tuhuma za kumwita Rais Jakaya Kikwete gaidi.

Mwanasiasa huyo amekiuka masharti ya dhamana yake hivyo amerudishwa rumande.

Hakimu Mkazi Waliarwande Lema alisema amechukua uamuzi huo baada ya mtuhumiwa kushindwa kufika mahakamani hapo kwa muda muafaka.

Kwa mujibu wa hakimu huyo,ni mara ya pili sasa Mtikila amekuwa akichelewa mahakamani hapo bila kutoa taarifa zozote kwa wadhamini wake kama masharti ya dhamana yanavyoelekeza.

Mtikila amedai mahakamani kuwa alikuwa anaumwa na kuongeza kuwa taarifa za kuumwa kwake alimpatia Wakili wake ambaye naye alidai mwanawe anaumwa na hivyo mahakama kushindwa kupata taarifa zake.

“Ni mara ya pili sasa umekuwa ukirudia kosa hili bila kutoa taarifa zozote kwa wadhamini wako hivyo ninakufutia dhamana utarudi rumande hadi Januari 25, mwaka huu kesi yako itakapoletwa kwa ajili ya kusikiliza maelezo ya awali,” alihitimisha Hakimu Lema.

Januari 4, mwaka jana, mtuhumiwa hakufika mahakamani hapo ambapo upande wa mashitaka uliiomba mahakama hiyo kutoa kibali cha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kutokana na kutofika kusikiliza kesi inayomkabili bila kutoa taarifa yoyote wala maombi ya kumfanya ashindwe kufika mahakamani.

Hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo, Victoria Nongwa hakutoa kibali cha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo licha ya kuombwa na upande wa mashitaka.

Januari 6, mwaka jana, Mtikila aliwasilisha barua ya kuiomba msamaha mahakama hiyo, akieleza kuwa alikuwa akimhangaikia ndugu yake ambaye amepooza na kudai kuwa aliwatuma wadhamini wake kutoa taarifa hiyo lakini hawakufanya hivyo.

Inadaiwa kuwa,Oktoba 21, 2007, maeneo ya Ilala katika Shirika la Nyumba (NHC) la Taifa, Mtikila alitoa maneno ya dharau na kujenga chuki dhidi ya Serikali ya Rais.

Katika shitaka la pili, Mtikila anadaiwa kutoa lugha ya uchochezi akidai: “Ahadi zote za Rais Jakaya Kikwete siku zote zinaongozwa na imani yake ya dini tena kutekeleza malengo yake ya kusilimisha nchi”

Mtikila alikana mashitaka hayo na alikuwa nje kwa dhamana.

Chanzo: HabariLeo

Demokrasia ni Mtikila na Kulikoni tu?
 
May be yule nyoka aliyemgonga siku ile kule Zimbabwe alilegeza some brain attachment za Mtikila, vituko vyake vimeanza!
 
Wana JF, kheri ya mwaka mpya. Nilijiunga na jukwaa hili muhimu, majuma mchache yaliyopita, lakini bado nilikuwa sijawasiliana nanyi rasmi kwa vile nilikuwa kwanza nikipitia michango yenu, makala, na habari nyingi za kusisimua. Shukrani nyingi kwa michango yenu muhimu na ya kuelimishana.

Ningelipenda kusema chochote kuhusu mashtaka yanayomkabili Mchungaji Mtikila. Katika demokrasia ya kweli, watu hawashtakiwi kwa kuwaita viongozi walio madarakani 'gaidi'.

Siku za nyuma nilishuhudia Rais George Bush Jr, akiitwa 'gaidi' kwa kujihusisha kwake katika vita vya Iraq; na, ingawaje baadhi ya watu waliomwita hivi ni Wamarekani, hawakufunguliwa mashtaka yoyote.

Dhahiri, lugha aliyoitumia Mchungaji Mtikila haikuwa na diplomasia. Lakini huwezi kutegemea watu katika jamii ya kisiasa kuwa na mtizamo wa namna moja; au hata malezi yanayolandana, kwa vile jamii nzima haitoki familia moja.

Kutumia au kutotumia diplomasia katika mawasiliano baina yetu katika jamii, ni jambo la hiyari tu, ambalo haliwezi kulazimishwa kwa nguvu za kisheria. Nina hakika kifungu cha sheria kilichotumika kumfungulia mashtaka Mchungaji Mtikila, hakiendi sambamba na wakati tuliomo hivi sasa, wa demokrasia.

Isitoshe, Rais akiitwa 'gaidi', tamko kama hili, hakika, alimfanyi Rais kuwa 'gaidi' hata kidogo.

Nje ya hilo, tamko kama hilo halimjengei chuki Rais kwa wananchi, kama chuki haipo. Badala yake, inawashangaza walio wengi kumshtaki Mchungaji Mtikila kwa kosa la 'kumtukana' Rais wakati mafisadi-papa wanaendelea kulindwa na uongozi wa kisiasa uliopo hivi sasa madarakani.

Hata mtoto mdogo, anaweza kubaini kuwa ili la mwisho linaweza kumjengea chuki Rais na wananchi wake kuliko 'matusi' ya Mchungaji Mtikila.

Kuwa Rais, kunahitaji uvumilivu wa hali ya juu sana kutokana na madaraka mengi katiba inayomlimbikizia Rais. Ni uvumilivu wa namna hiyo methali ya 'Mkubwa ni jaa' inayolenga kuimarisha.

Aidha, serikali inamshitaki Mchungaji Mtikila kama fundisho kwetu wote kwamba, viongozi wetu wateule wanastahili wakusifiwa na kutukuzwa daima, jambo ambalo hata hivyo haliendi sambamba na dhana ya demokrasia tunayokusudia kujenga.

Kama madhumuni ya kumshitaki Mchungaji Mtikila yamejificha nyuma ya pazia hili, basi kama alivyonena MCHUKIA UFISADI 'Wapigania haki siku zote wawe tayari kupitia njia hii...' (ya kutupwa gerezani kutokana na kesi ambazo chanzo chake ni siasa). Hili si jambo zuri katika karne ya ishirini na moja au kwa mshikamano wa Taifa letu.
 
tuache sheria ichukue mkondo wake akuna aliye juu ya sheria but ifanye ivyo kwa mafisadi na walosaini mikataba mibovu
 
ametumwa kuwahubiria wafungwa habari njema, ili baada ya uchaguzi, raisi mteule akiwatoa kwa msamaha, basi wawe wanamjua yesu na kuacha maovu,
maana wengi wa wafungwa dar es salaamu ni wale wanaodai Yesu si Mungu huku wakiwaibia watu simu zao hasa maeneo ya mwananyamala, keko, tandika, buguruni,tandale , hawa ni kina mudi guy, mudi boy, side boy, j4, dulayo, dul one, dula, sheby, sheby one sheby guy
 
tuache sheria ichukue mkondo wake akuna aliye juu ya sheria but ifanye ivyo kwa mafisadi na walosaini mikataba mibovu


Mafisadi wako juu ya sheria. Hata mkibisha ndivyo ilivyo.
Wa Richmond walishawekwa hata rumande? zaidi ya Gea tu who was just a front. wengine je? na kesi hata ya Gea imekaaje? achana na propaganda za rangi ya njano na kijani.
 
mtikila ni mkorofi sana

hapana siyo mkorofi ni mtafutaji tu kama watafutaji wengine, ndiyo maana ni mchungaji, mwenyekiti wa chama cha dp. Mpigania haki za wanyonge, mwanasiasa n.k.

Ila sijui kanisa lake linaitwaje na liko wapi.
Uko kote anatafuta maslahi, ndiyo maana ra alishawahi kumnunua. Mtikila alikataa kununuliwa na ra, siku ra alipokuja na vocha yenye sahihi yake mtikila akalala mbele.
Kwa mtizamo wangu namuona kama mtafutaji zaidi.
 
Back
Top Bottom