Mtendaji kizimbani kwa rushwa ya 250,000/

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
OFISA Mtendaji wa Kata ya Challa katika Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa, Priver Mwasile amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Nkasi akikabiliwa na shtaka la kuomba na kupokea rushwa ya Sh 250,000 kutoka kwa mtu anayetuhumiwa kuingiza mifugo katika vyanzo vya maji.

Imedaiwa na Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Ferdnand Nsakuzi mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Nkasi, Manase Goroba, kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo Aprili 16 ya mwaka huu majira ya mchana katika Kata hiyo ya Challa.

Nsakuzi aieleza Mahakama hiyo kuwa siku ya tukio, mshtakiwa huyo alimshawishi Ngika Yegele aliyekuwa na kesi katika Mahakama ya Mwanzo Challa ampatie kiasi cha Sh 250,000 ili aweze kumsaidia katika kesi iliyokuwa ikimkabili ya kukutwa akiwa analisha mifugo yake katika vyanzo vya maji.

Kwamba, Yegele alikubali, ndipo alipotoa taarifa katika ofisi za Takukuru iliyoandaa mtego uliofanikisha kumnasa Mwasile baada ya kukutwa akipokea kiasi hicho cha fedha kutoka kwa mtuhumiwa.

Hata hivyo, Mwansele amekana shitaka hilo jambo lililosababisha Hakimu Goroba kuahirisha kesi hadi Juni 9 mwaka huu itakapotajwa tena.

HabariLeo | Mtendaji kizimbani kwa rushwa ya 250,000/

Laiti ingekuwa Bongo kama Nchi zingine za Dunia ukipokea Rushwa unahukumiwa Kifo basi ninafikiri hapo kwetu hili Tatizo Sugu lingeondoka Tatizo la Rushwa hapo kwetu limekuwa kama Ugonjwa wa Kensa (Cancer Disease) Ugonjwa usiopona Namuomba Mzee J Kikwete Tatizo la Rushwa alitafutie Dawa la kuliponyesha haraka iwezekanavyo nalichukia sana hilo tatizo.
 
Back
Top Bottom