Mtei: Uongozi wa Rais Magufuli ni kama wa Mwl. Nyerere

Ukizeeka sana akili zinarudi utoto...Mzee Mtei akili zake zimerudi utotoni

Nyie washabiki mna laana......, Slaa mlianza kumkashifu alipotofautiana na mipango ya kubadilisha gear angani.... Lipumba hivyo hivyo, sasa Mzee Mtei tena mwenye hati miliki ya chama katoa Maoni yake mmeamza kumtukana kisa tu yameenda kinyume kidogo na mnavyotaka..!!!! Kingunge ambaye Ni Mzee kuliko Mtei aliongea lugha mnavyotaka kuisikia ... Yeye Ni "hero " machoni penu ...! Seriously mnahitaji ukombozi wa fikra.... Hamjui mnataka nini .......
 
Michango mingi ya bandiko hili ni lawama kwa serikali ya Magufuli kwamba anapora demokrasia pamoja na sifa kede alizomwagiwa na Mzee Mtei. Kigezo ati ni bunge kutokuoneshwa "live".

Wanalalamikia hilo ni wanasiasa uchwara na wanaharakati. Huu ni wakati wa vitendo vya kimaendeleo na siyo kuoneshwa/kuona, kusikia au kusoma udaku na vitendo vya hovyo na uchochezi.

TAFAKARI CHUKUA HATUA
 
Leo wa kijani wataweka kambi uzi huu hawaondoki, na kule CDM ukitaka kujua unafiki wa jamaa wa kambi ile hutasikia huyu mzee akiitwa kwa majina mabaya au kuambiwa msaliti,angekuwa Zitto ndio kayasema haya ungeona kambi ya Mjerumani hapa povu lao,
kuwaamini wanasiasa wa kibongo sawa na kubeba maji kwenye ungo
 
Hayo ni mawazo yake.ila mimi nasema kati ya marais wote huyu ndio hana vision

Unabishana Na Mwasisi wa Chama? Tatizo mmehama kwenye malengo Na misingi ya Chama waliojiwekea waasisi wa Chama... matokeo yake mmemeza ndoano imekaa kooni haiendi mbele wala hairudi nyuma....!
 
Toeni ujinga hapa
Kama Kuna positive actions however few tutasifia lakini kwa huyu dikteta wenu hakuna mengi ya kujisifu
Je hali ya maisha imekuwa bora kwa MTz wa kawida?
Nini cha kujisifu miezi tisa yangu ashike madaraka?
Achemi utani anaposema atawasaidia wanyonge kama Mwalimu Ni kuwatimua UDOM?
Ni kuwapandishia bei ya sukari?
Ni kumpa wadhifa Mrema?
Ni nini?
Acheni mzaha na maisha ya wa Tz na Mhima wenu

Unaanzaje kumwita Mzee Mtei mjinga?
 
Back
Top Bottom