Mtego wa kisheria katika kile kinachoitwa mkataba wa bandari

shida ya hawa watu, huwa wanajifanya hawasikii, wanaingia mikataba ya madudu weee, wanajua wanatupoteza ila kwa maslahi yao wanaendelea tu kwa kufumba macho. wakimaliza utawala wao wanapokaribia kufa, wanaandika kitabu halafu wanajuta kwa waliyoyafanya kwamba kweli yale malalamishi tuliyalalamikia wakatudharau tulikuwa sahihi. wanakufa, wanatuachia msala na kizazi kijacho,na hawatakiwi kuwajibishwa. kuna siku sheria ibadilishwe wanyongwe, kwasababu wanajua wanafanya jambo baya lakini wanaendelea kulifanya kwasababu hawawezi kuwajibishwa.
Katiba Mpya ndio mwarobaini mkuu lkn Sasa kuipata inabidi watanzania kweli tujitoe kwa nguvu zote
 
..hicho kipengele kimenitatiza sana.

..kama ni lazima kiwepo, basi na sisi tudai kwamba DP wakitaka kuwekeza ktk bandari za Mombasa, Beira, na kwingine kwenye ushindani na bandari yetu tuelezwe / tujulishwe.
Kweli kabisa ndio maana tunasema mkataba huu unatufunga miguu,mikono na mdomo kwa nini tuukubali? Hv viongozi wetu wamelogwa?
 
PAMOJA na yote mkuu sidhani kama nchi nyingine alipowekeza huyu DP world Kuna mkataba wa hovo kama huu, kiukweli Hawa waarabu wametudhau sana, hebu fikiri Kuna kipengele kinasema shughuli au fursa zozote za kibandari na maeneo mengine zitakapojitokeza sisi Tanzania tutapaswa kuwajulisha wao hili ni tusi kubwa sana
Djibout kipendele iko waliwekewa na ilipokuna fursa wakataka kuitumia DP world alizuia. Jamaa wakavunja mkataba, DPW akaenda washitaki. Ipo video kabisa aljazeera inaelezea ilo swala. Ni ajabu kuona wabunge wetu hawaoni. Wao wamekomaa kuona Bint anabonyeza kontena linashuka utafikiri hayo ndio maslahi ya taifa
 
Mimi sio mwanasheria lkn ninatumia akili ya kawaida kuhoji na kutafakari mambo, tunaposema bandari zimeuzwa tuna maanisha kweli, nimeusoma mkataba huu kwa umakini mkubwa. Pamoja na mambo mengine mengi nitajikita katika
maneno muhimu sana yafuatayo:
Intergovernmental agreement (IGA)na Host government agreement (HGA)

Kwa kuzingatia maelezo yaliyopo kwenye mkataba,

Kwamba IGA ni makubaliano ya jumla/ makubwa au mama kati ya nchi na nchi japo sisi tumeingia makubaliano kati JMT na kampuni ya Dubai sijui yanaitwaje haya makubaliano.

HGA ni makubaliano madogo madogo ya miradi yatakayo kuwa ndani au chini ya IGA.

Sasa hoja yangu ni nini hapa?.
IGA hakuna ukomo yaani ni milele mpaka bahari na maziwa yetu yatakapo kauka lkn tunaambiwa HGA kutakuwa na ukomo maana yake ni hata pale HGA zitakapofikia ukomo tutalazimishwa/lazimika kuendelea na Hawa DPW hata wakivurunda, wakishindwa kutimiza masharti kwani hatutakuwa na uwezo wa kusitisha au kuvunja IGA Hivyo tutakuwa mateka WA milele.

Huu ni mkataba wa kilaghai kama Ile walikuwa wanaingia babu zetu kipindi cha utumwa na ukoloni bila kujua, tofauti kwamba Karne hii watawala wetu wanaingia kwa kujua kabisa.

Watanganyika tuamke tumeuzwa!
View attachment 2663427
Mungu ametuona CCM-CHUKUA CHAKO MAPEMA wamesha chukua chao ndiyo maana hwakubali wamesha kula matango poli
 
Lisu hana issue usimpe mileage za bure. Ni mmoja wa wanufaika wa IGA
Kwahiyo CCM hautakuwepo? Kubinafsisha bandari ni moja ya kukosa akili, kukosa mbinu na serikali ni dhaifu. Mkataba wa kishenzy sana.
CCM wamebakiza wauze nchi wakimbie
 
Mimi sio mwanasheria lkn ninatumia akili ya kawaida kuhoji na kutafakari mambo, tunaposema bandari zimeuzwa tuna maanisha kweli, nimeusoma mkataba huu kwa umakini mkubwa. Pamoja na mambo mengine mengi nitajikita katika
maneno muhimu sana yafuatayo:
Intergovernmental agreement (IGA)na Host government agreement (HGA)

Kwa kuzingatia maelezo yaliyopo kwenye mkataba,

Kwamba IGA ni makubaliano ya jumla/ makubwa au mama kati ya nchi na nchi japo sisi tumeingia makubaliano kati JMT na kampuni ya Dubai sijui yanaitwaje haya makubaliano.

HGA ni makubaliano madogo madogo ya miradi yatakayo kuwa ndani au chini ya IGA.

Sasa hoja yangu ni nini hapa?.
IGA hakuna ukomo yaani ni milele mpaka bahari na maziwa yetu yatakapo kauka lkn tunaambiwa HGA kutakuwa na ukomo maana yake ni hata pale HGA zitakapofikia ukomo tutalazimishwa/lazimika kuendelea na Hawa DPW hata wakivurunda, wakishindwa kutimiza masharti kwani hatutakuwa na uwezo wa kusitisha au kuvunja IGA Hivyo tutakuwa mateka WA milele.

Huu ni mkataba wa kilaghai kama Ile walikuwa wanaingia babu zetu kipindi cha utumwa na ukoloni bila kujua, tofauti kwamba Karne hii watawala wetu wanaingia kwa kujua kabisa.

Watanganyika tuamke tumeuzwa!
View attachment 2663427
Naunga mkono hoja
 
Back
Top Bottom