Mtatiro: Kaskazini wana Mkakati wa kwenda Ikulu

Siku zote siasa za udini, ukabila na ukanda zinaanzishwa na ccm. Lakini hatutorudi nyuma
 
Big up Julius Mtatiro nadhani kuna Watu wanaona hawawezi kushika Nchini bila kutugawa kwa ukanda na ukabila .....udini ....Kina wakati walisema cuf ni ya waislamu Siasa wanasema Kaskazini ....
 
Last edited by a moderator:
Hamna Kitu Hapa Ni Saund Tu, Mbowe, Mbatia, Sumaye, Lowasa, Slaa (kama Bado Yu Ukwawa) Nk. Wote Wakaskazn Na Chadema Waliwah Kupendekeza Kaskazini Ijitenge! Inatia Shaka Hapa Ukizingatia Na Sera Zenu Za Majimbo
 
Mtatiro naye aache ulofa Jimbo la ukonga ndo maana unawekewa Mizengwe na waroho wa madaraka

hili neno 'lofa' lilikuwepo siku nyingi sana,inaonekana kuna raia ndio mmeliskia jana kwa mara ya kwanza mnavyolishadadia..
 
Hamna Kitu Hapa Ni Saund Tu, Mbowe, Mbatia, Sumaye, Lowasa, Slaa (kama Bado Yu Ukwawa) Nk. Wote Wakaskazn Na Chadema Waliwah Kupendekeza Kaskazini Ijitenge! Inatia Shaka Hapa Ukizingatia Na Sera Zenu Za Majimbo

utaanzia wapi kujibu hizo hoja za Mtatiro..bora umeamua kubakia kin'gan'ganizi tuu..
 
kwa kauli za kipumbavu na za kilofa zilizosemwa jana na wanaccm pale jangwani nimeamini ccm ilishaondoka na nyerere. imebaki ccmmafisi. kubomoa nchi kwa kuwabagua watanzania sio kazi ili mradi tu ccm ishinde uchaguzi.ccm imekwisha.
 
Hamna Kitu Hapa Ni Saund Tu, Mbowe, Mbatia, Sumaye, Lowasa, Slaa (kama Bado Yu Ukwawa) Nk. Wote Wakaskazn Na Chadema Waliwah Kupendekeza Kaskazini Ijitenge! Inatia Shaka Hapa Ukizingatia Na Sera Zenu Za Majimbo

hii hofu ni ya nini? mbona watu hawajalalamika mawaziri wakuu wengi kutokea kaskazin? je ccm hili hawakuliona? nimeamini ccm ndo chanzo kikubwa cha kuligawa taifa letu...
 
lakin hata huku mtaani umeingia tunaona wachaga wanajitenga sasa na hii itawaharibia sana... ukanda si mzur hata kidogo
 
Ni rahisi sana kushabikiai siasa za udini na ukabila au ukanda kwa manufaa ya kisiasa kwa kuangalia mwisho wa pua lakini madhara ya ushabiki wa propaganda hizi ni makubwa kuliko vile inavyoweza kudhaniwa,hawa wanasiasa na wapambe wa aina hizi za siasa chafu wanafurahia na kuona wamemshinda au wamepata kete bora lakini hawajui mbegu wanayaopandikiza ina madhara kwa taifa letu, wanaangalia mahitaji yao ya sasa!

Jamani sisi sote ni watanzania tunahitaji Tanzania yenye maelewano, isiyo na chuki wa chembe ya udini na ukabila/ukanda.

Siasa na wanasiasa watapita lakini undugu,mshikamano na umoja wetu sio vitu vya kuchezea kamwe havipiti kama wanasiasa bali ni tunu za kuvusha mbali.

SHIME TUUNGANE BILA KUJALI ITIKADI ZA KISIASA TUKEMEE AINA HII YA PROPAGANDA.

TUKATAEE KWA NGUVU ZETU KUWA SEHEMU YA SIASA HIZI

chanzo cha yote hayo kisa ccm imebanww mwaka huu. sisi huku kusini hatutasikiliza chochote ilimradi ccm iondoke.
 
lakin hata huku mtaani umeingia tunaona wachaga wanajitenga sasa na hii itawaharibia sana... ukanda si mzur hata kidogo

mtaani hakuna hiyo issue.ccm wanatumia hiyo hoja ili kujaribu kudhoofisha ukawa. kisa mwaka huu wamebanwa. ccm ndo mabingwa wa kuwagawa watanzania...
 
unatafuta kick tu, wewe ni paka tu hakuna wa kukupigia simu-wakubwa wako tu wameambiwa ni wapumbafu na malofa sasa wewe una umashuhuli gani wa kupigiwa simu?
 
Watapambana lakini hawatashinda,hayo ni mateke ya mwisho ya ukataji wa roho kwa CCM
 
unatafuta kick tu, wewe ni paka tu hakuna wa kukupigia simu-wakubwa wako tu wameambiwa ni wapumbafu na malofa sasa wewe una umashuhuli gani wa kupigiwa simu?

Yani viongozi wa ACT mnaungana na CCM kutukana ?

SMH...
 
Kwani mtatiro naye unaweza kumweka miongoni mwa watu wenye akili timamu!
 
Kwa namna yoyote ile hata kama tunayataka sana madaraka na ni lazima kama baadhi ya watu wanavyojiaminisha, lakini tunakoelekea na hizi siasa za kutugawa Watanzania kikanda siyo afya kwa Taifa leo.

Siyo vyema kabisa kuendelea kushabikia na kuhuburi, ukanda,udini na ukabila, Wanasiasa tutumieni manavyoweza maana bado mnamtaji wa wajinga wengi, kwa maana mlitunyima elimu ya Uraia ila msitugawe kwa propoganda hizi za ukanda, msitupandikizie chuki hizi mioyoni mwetu.

Taifa hili niletu sote kila Raia ana changia pato kwa namna yake, katika mfuko mkuu wa hazina hakuna akaunti ya watu wa ukanda fulani wala wa dini fulani, kinachopatikana kinagawiwa sawa na kuleta maendeleo kwa kila Mtanzania bila kujali ni kabila au dini gani.

Vyama vyote vya siasa vinajiendesha kwa ruzuku ambazo ni kodi zetu Watanzania, mbona viongozi mnatumia majukwaa kutugawa? nikiongozi gani anaetambua chama chake kilichukua pesa ya ruzuku ya ukanda au ya kabila fulani? NI UPUUZI USIYO VUMILIKA HATA KIDOGO.

Mtu napohama chama kimoja kwenda kingine ni haki yake kikatiba sasa inakuwaje watu tunaminya demokrasia kiasi hiki, badala yake tunaigeuza na kuibatiza ni ukanda?

Wanasiasa na Watanzania sukumeni kete zote, lakini hizi za ukabila,udini na ukanda msijaribu kuzitumia kama upenyo wa kuwatimizia malengo yenu ya kisasa ni HATARI.

Binafsi nimeshwahi kukosa kazi kwa tabia hizi hizi za ukabila na sifa zote nilikuwa nazo, ila kuna rafiki yangu niliomba nae na alikuwa ni wa eneo moja na mkuu wa kitengo akapata kazi, mimi ni muhanga wa kansa hii ya ukanda na ukabila hivyo sitakuwa tayari kuendelea kuona wapuuzi wachache wakieneza propoganda za kijinga kama hizi...

#MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE.
 
Mtatiro umesomeka.
Swali: ivi isue ya segerea kuachiwa jimbo imeshakuwa solved.
Maana kura yangu ipo kwako. Nitoe wasiwasi
 
Habari haina mashiko hii, bila kuwasema hao alioongea nao ni upuuzi kuiamini hii habari.

Huu unaousema hapa ni ungedere sio ulofa tena. Unazijua sheria za kutoa details za mawasiliano binafsi kwa kuweka majina?
 
Back
Top Bottom