Mtandao wa vibali bandia vya uhamiaji mkoa wa arusha waingia sura mpya

Juliani Mumbi

Member
Mar 1, 2012
10
3
Mtandao wa utoaji vibali bandia katika mkoa wa Arusha umeingia sura mpya baada ya kinara wa shughuli hiyo kuanza kushughulikiwa na Makao makuu. Kinara huyo ambaye amekuwa akitamba kwa muda mrefu bila kuguswa kwa mbinu ya kutumia pesa nyingi na ikibidi hujitoa yeye menywe ili mambo yaishe, hivi karibuni ametakiwa kujieleza kwa nini asifukuzwe kazi kwa kutoa vibali bandia kadhaa kwa raia wa kigeni.
Vibali hivyo vilikamatwa na kiongozi mgeni katika mkoa huo kwa kuwa kiongozi wa mkoa hana tena kauli kwa dada huyo ambaye kusema ukweli kajaliwa urembo. Kwa kuhofia taarifa za kukamatwa vibali hivyo kuhujumiwa kiongozi huyo mgeni ilibidi ahame ofisi na kwenda kufanya kazi hiyo mahala pengine kwakuwa ofisini hapo dada huyo amekamata kila eneo.
Pamoja na kutakiwa kujieleza mlimbwende huyo amesema hiyo ni nguvu ya soda na ugeni wa kiongozi huyo kwakuwa hajampatia nafasi ili nayeye amzibe mdomo. Mlimbwende huyo aliendelea kusema pamoja na kutakiwa kutoa maelezo hayo lakini anajua ni danganya toto kwa kuwa mtandao wake ulioko makao makuu umeahidi kulimaliza jambo hilo haraka bila kumletea madhara. Anasema muda mrefu anasaidiwa na dada yake mpenzi ambae sasa hivi mkuu wa sheria na Kibuzi chake cha utumishi. Watu hao wawili wamemuunganisha na watu wengine wa makao makuu ambao wanahakikisha mambo yake hayaharibiki.
Amejitapa kuwa miaka ya nyuma alikuwa akipokea maombi ya vibali vya wageni aliyapeleka kwa dada yake huyo ambaye naye aliviwasilisha kwa mkubwa wa Vibali nchini aliyemwagwa na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Shamsi Nahodha.
Amesema kuwa baada ya kupata mchongo wa kupata vibali bandia alipunguza kutuma maombi hayo jambo lililomshtua sana dada yake huyo, lakini alimtuliza kwa kuwa anamkatia mafungu kidogokidogo.
Wachunguzi wa mambo wanasema ujio wa kiongozi huyo mpya umeibua mambo mengi sana ofisi tena haikaliki, na mambo ya vibali bandia yanakwisha.
Julian.
 
Back
Top Bottom