Mtakatifu Paulo, ulaghai wa kutumia misamiati tata, na umachiaveli

Mama Amon

JF-Expert Member
Mar 30, 2018
2,021
2,478
maxresdefault.jpg

Kwenye piramidi la vitu vyote vilivyo katika ulimwengu wa miili sisi wanadamu tumeketi kileleni kwa sababu ya urazini wetu.

Katika mipaka ya utambuzi tuliyozaliwa nayo kama wanadamu, tunao uwezo wa kuvuna maarifa kutoka katika mazingira yetu, kufikiri kimantiki, kuteua malengo, kubuni mbinu kwa ajili ya kufanikisha malengo yetu, na kutekeleza mipango iliyo na masikilizano ya kimantiki na malengo yetu.

Kwa hiyo, kanuni za mantiki ni vigezo vya kupima kiwango cha urazini wa binadamu. Kwa sababu ya ukweli huu, linafuata hitimisho kwamba, kama kwa makusudi tukitoa matamko yanayokiuka kanuni za mantiki, tunakuwa tumekumbatia uzezeta unaotuweka katika daraja la nyani.

Kwa mfano, kauli zenye mikanganyiko ya kimantiki, ambazo pia huitwa kauli zenye migogoro ya kimantiki, ni kauli zinazoonekana kuwa ukweli na kuwa na upotofu kwa wakati ule ule na kwa mtazamo ule ule. Lakini, kanuni moja ya mantiki inasema kuwa hakuna kauli inayoweza kuwa ukweli na kuwa na upotofu kwa wakati ule ule na kwa mtazamo ule ule. Kuvunja kanuni hii ni kuzalisha janga la kimaarifa katika jamii.

Kwa hiyo, kukumbatia, kwa maukusudi, kauli zenye mkanganyiko wa kimantiki ni kufanya uamuzi unaopingana na hulka ya binadamu, ambayo, inatupa jukumu la kufukuzia wema wa umantiki (the good of logical coherence) na kuepuka uovu wa ukanganyifu (the evil of logical incoherence).

Kwa kuzingatia msimamo huu, napendekeza kujibu maswali matatu: mkanganyiko wa kimantiki ni kitu gani na kauli zipi zinahesabiwa kuwa ni mikanganyiko ya kimantiki? Kutokana na mikanganyiko ya kimantiki, janga la kimaarifa katika imani ya jamii tuliyo nayo leo ni kubwa kwa kiasi gani? Na tufanye nini ili kuepuka janga la kimaarifa linalotukabili?

Kwa ajili ya uchambuzi huu nachuja na kutumia baadhi ya fikra za wanazuoni watatu. Kuna Alvin Plantinga (1974) na kitabu chake, "God, Freedom and Evil"; na James Anderson (2007) na kitabu chake, "Paradox in Christian Theology"; na Tuomas Tahko (2009) na makala yake, "The Law of Non-Contradiction as a Metaphysical Principle."

Maana ya janga la kimaarifa

Mwaka 2020, aliyekuwa Rais wa Marekani, Baraka Obama, akihojiwa na Jeffrey Goldber, mhariri mkuu wa gazeti la “The Atlantic,” aliwaonya Wamarekani kuhusu “janga la kimaarifa,” yaani “epistemological crisis,” lililokuwa linawakabili.

Katika "soko la mawazo," hii ni changamoto ambayo hujitokeza pale ambapo jamii hupoteza “uwezo wa kutofautisha kati ya ukweli na uwongo,” alisema Obama.

Kuwepo kwa janga hili huthibitishwa na utitiri wa sentensi unganifu ambazo zimebeba kauli za kweli na kauli za uwongo,” hali ambayo huitwa “mkanganyiko,” yaani, “paradox,” “mystery,” au “contradiction,” kwa Kiingereza.

Kwa mfano, “Tanzania ni nchi ya kijamaa; na Tanzania si nchi ya kijamaa” ni mfano wa mkanganyiko wa kimantiki. Pia, "Zanzibar ni nchi huru; na Zanzibar sio nchi huru" ni mfano mwingine wa mkanganyiko.

Kwa sabab huu unapata taifa moja, ambalo watu wake hawakubaliani tena juu ya maswali ya msingi kuhusu ukweli thabiti kutokana na taarifa potofu zinazosambazwa ama kwa makusudi, au taarifa potofu zinazosambazwa kwa bahati mbaya.

Kwa kila swali kunatolewa majibu mawili kwa mpigo: ndiyo na hapana. Ukweli wa kudumu hauna nafasi tena katika taifa la aina hii kwa sababu kila kambi inakuwa na toleo lake la ukweli wa kisekta.

Hili linakuwa ni taifa linalotawaliwa na itikadi ya ukweli kinyonga, ambapo watu huona ukweli kwa njia tofauti kulingana na miwani ya kisekta waliyoivaa kutoka sekta ya kijamii, kisiasa au kiuchumi.

Katika hali kama hiyo, taifa linapata mgawanyiko katika kambi mbili, ambapo watu wanauliza maswali yale yale na kufikia majibu yanayopingana, na wanadiriki kuyakumbatia majibu yote mawili, kana kwamba hilo ni jambo la sifa.

Lakini, kulingana na kanuni ya mantiki ya kutojipinga (the Law of Non-Contradiction), kama ilivyojadiliwa na Tahko (2009), kauli ile ile haiwezi kuwa kweli na isiwe kweli wakati ule ule na katika mtazamo ule ule.

Sentensi yenye kubeba “mkanganyiko” wa aina hii inakuwa na tatizo la “ukanganyifu,” yaani “incoherence,” ama katika ngazi ya kimantiki, au ngazi ya kimetafizikia, au katika ngaz zote mbili.

Tahko (2009:32-33) anasema kuwa, Sheria ya kutojipinga ni kanuni ya kimetafizikia inayohusu muundo msingi wa ukweli duniani.

Inataja mipaka inayohusu udhati wa mambo badala ya kauli za kisemantiki pekee.

Kwa hivyo tafsiri ya kimetafizikia ya Sheria ya Kutojipingana ni sawa na hii: vitu vilivyo katika ulimwengu halisi nje ya fikra za watu hutawaliwa na aina fulani za kanuni, ambapo mojawapo inasema kwamba, "sifa ile ile haiwezi kumilikiwa na kitu wakati huo huo isimilikiwe na kitu hicho."

Kwa mfano, atomu haiwezi kuwa na protoni na isiwe na protoni kwa wakati mmoja; au kitu hakiwezi kuwa kijani kwa silimia mia moja na kikawa na rangi nyekundu kwa asilimia mia moja katika wakati mmoja.

Mifano hii inaonyesha kwamba udhati wa vitu (the essense of things) unaongozwa na sheria ya kutojipingana.

Kwa mujibu wa Obama, “janga la kimaarifa” ni sumu katika “soko huria la mawazo,” na hivyo sumu kwa uhai wa mifumo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii. Mtazamo huu ni sahihi kwa kuwa jawabu la “ndiyo na hapana” kwa maswali muhimu haliwezi kuwa msingi thabiti wa maamuzi.

Mkanganyiko daraja la kwanza: mkanganyiko ulio bayana ndani ya seti husika

Kwa mujibu wa Plantinga (1974), kama tukitumia kigezo cha aina za kauli zinazozalisha mikanganyiko, tunaweza kubainisha mikanganyiko ya aina tatu. Kuna mkanganyiko daraja la kwanza, mkanganyiko daraja la pili, na mkanganyiko daraja la tatu.

Seti ya matamko kadhaa inakuwa na mkanganyiko wa daraja la kwanza endapo kuna ukinzani wa wazi kati ya angalau kauli mbili zilizomo katika seti hiyo (explicit contradiction).

Mfano wa kwanza ni seti ya kauli hizi: “Afrika inazo nchi 54 ikiwemo Tanzanoa’; ‘kwa hiyo, Tanzania iko Afrika’; na ‘Tanzania haiko Afrika’.” Kauli ya pili na ya tatu zinapingana.

Mfano wa pili ni seti ya kauli hizi: “‘Pembetatu inazo kona tatu’; ‘kwa hiyo, pembetatu sio mraba’; na ‘Pembetatu ni mraba.’” Kauli ya tatu na nne zinapingana.

Mfano wa tatu ni seti ya kauli hizi: “‘Watanzania wote huongea Kiswahili’; ‘Juma ni Mtanzania’; kwa hiyo, ‘Juma anaongea Kiswahili’; ‘Juma haongei Kiswahili.’” Kauli ya tatu na nne zinapingana.

Mfano wa nne ni seti ya sentensi hizi: "Dunia inalizunguka jua; na jua linaizunguka dunia."

Mfano wa tano ni seti ya sentensi hizi: "Mimi nakupenda; na Mimi sikupendi."

Mfano wa sita ni seti ya sentensi hizi: "katika wakati mmoja divai ya zabibu ni tunda kutokana na mmea uitwao mzabibu; na katika wakati mwingine divai ya zabibu ni damu ya binadamu aitwaye Yesu." Lakini, katika ulimwegu wa miili, seli za mmea haziwezi kugeuka seli za mnyama.

Mfano wa saba ni seti ya sentensi hizi: "katika wakati mmoja mkati wa hostia ni tunda la mmea uitwao mpunga; na katika wakati mwingine mkati wa hostia ni mwili wa binadamu aitwaye Yesu." Lakini, katika ulimwegu wa miili, seli za mmea haziwezi kugeuka seli za mnyama.

Mfano wa nane ni seti ya sentensi hizi: (1) Mabadiliko yoyote kuzalisha kitu kipya au kuangamiza kitu kilichokuwepo awali; (2) Wakati wa misa, sala ya konsekrasio haileti mabadiliko ya kuzalisha kitu kipya au kuangamiza kitu kilichokuwepo mezani kabla ya sala; (3) Hivyo, hakuna mabadiliko yanayoonekana na ya kweli yanayotokea kutokana na maombi hayo; (4) kuna mabadiliko yasiyoonekana na ya kweli ambayo hutokea kupitia sala ya konsekrasio.” Matamko namba tatu na namba nne yanapingana.

Mfano wa tisa ni seti ya sentensi hizi: “Mwana alitwaa asili ya kibinadamu; Mwana ni Mungu; hivyo, Mungu alichukua asili ya mwanadamu; Baba hakuchukua asili ya kibinadamu; Baba ni Mungu; hivyo, Mungu hakuchukua asili ya mwanadamu.” Madai ya tatu na ya sita yanapingana.

Na mfano wa kumi ni seti ya sentensi sifuatazo: "(1) fumbo ya mageuzi ya mkate na divai linasema kwamba, baada ya sala ya konsekrasio, inayoendeshwa na padre, mwili wa Yesu, aliyeko mbinguni, huwa kwa kweli, kwa uhalisia, na kwa ukamilifu, upo ndani ya kila hostia, mahali popote itakapokuwa hapa duniani; (2) kwa mujibu wa kanuni ya fizikia kuhusu kutopenyeka kwa vitu yabisi (impenetrability), hakuna vitu viwili vinaweza kukaa kwenye nafasi moja kwa wakati mmoja; na (3) kwa mujibu wa kanuni ya fizikia juu ya uhusiano wa kitu-kimoja-katika-nafasi-moja-kwa-wakati-mmoja (anti-mutlilocation), kama vitu viwili X na Y vinakalia nafasi mbili tofauti katika wakati mmoja, basi kitu X ni tofauti na kitu Y." Katika seti hii, kauli ya kwanza inapingana na kauli ya pili na inakinzana na kauli ya tatu.

Mkanganyiko daraja la pili: Mkanganyiko uliojificha ndani ya seti husika

Seti ya matamko kadhaa inakuwa na mkanganyiko wa daraja la pili endapo kuna ukinzani usio wa wazi kati ya angalau kauli mbili zilizomo katika seti hiyo, lakini ukinzani huo unaweza kufichuliwa kwa kutumia kanuni za udadavuzi wa kimantiki, utakaozalisha mkanganyiko wa daraja la kwanza. (formal contradiction).

Yaani, katika mkanganyiko wa daraja la pili: ama kuna seti ndogo ya kauli inayozalisha hitimisho linalopingana na kauli nyingine ndani ya seti, au kuna seti ndogo mbili za kauli zinazozalisha mahitimisho yanayopingana.

Mfano wa kwanza ni seti ya kauli hizi: “‘Watanzania wote huongea Kiswahili’, ‘Juma ni Mtanzania’, ‘Juma haongei Kiswahili.’”

Wakati kauli ya tatu inasema kuwa, “Juma haongei Kiswahili,” kauli mbili za kwanza, zinazalisha hitimisho kinzani kwamba, “Juma anaongea Kiswahili.”

Mfano wa pili ni seti ya kauli hizi: “‘Pembetatu inazo kona tatu’; ‘mraba unazo kona nne’; na ‘Pembetatu ni mraba.’”

Wakati kauli ya tatu inasema kuwa, “pembetatu ni mraba,” kauli mbili za kwanza, zinazalisha hitimisho kinzani kwamba, “pembetatu sio mraba.”

Mfano wa tatu ni seti ya kauli hizi: “Mungu ni nafsi tatu; Baba ni nafsi Moja; na Baba ni Mungu.” Wakati kauli ya tatu inasema “Baba ni Mungu” kauli mbili za kwanza zinazalisha hitimisho kwamba “Baba sio Mungu.”

Mfano wa nne ni seti ya kauli hizi: “Mungu ni nafsi tatu; Mwana ni nafsi Moja; na Mwana ni Mungu.” Wakati kauli ya tatu inasema “Mwana ni Mungu” kauli mbili za kwanza zinazalisha hitimisho kwamba “Mwana sio Mungu.”

Mfano wa tano ni seti ya kauli hizi: “Mungu ni nafsi tatu; Roho Mtakatifu ni nafsi Moja; na Roho Mtakatifu ni Mungu.” Wakati kauli ya tatu inasema “Roho Mtakatifu ni Mungu” kauli mbili za kwanza zinazalisha hitimisho kwamba “Roho Mtakatifu sio Mungu.”

Mfano wa sita ni seti ya kauli hizi: “Baba ni Mungu; Mwana ni Mungu; Roho Mtakatifu ni Mungu; na Kuna Mungu mmoja.” Wakati kauli ya tatu inasema “Kuna Mungu mmoja” kauli tatu za kwanza zinazalisha hitimisho kwamba “Kuna Miungu Watatu.”

Mfano wa saba ni seti ya kauli hizi: “‘Wavulana huwa na kromozomu zenye fomati ya XY na mabinti huwa na kromozomu zenye fomati ya XX’; ‘kwa hiyo, wavulana huwa na fomati ya XY na jenitalia ya kiume na mabinti huwa na fomati ya XX na jenitalia ya kike’; na ‘Kuna mtu mwenye kromozomu zenye fomati ya XY na jenitalia kike.’”

Wakati kauli ya tatu inasema kuwa, “Kuna mtu mwenye kromozomu za fomati ya XY na jenitalia ya kike,” kauli mbili za kwanza, zinazalisha hitimisho kinzani kwamba, “Hakuna mtu mwenye kromozomu za fomati ya XY na jenitalia ya kike.”

Mfano wa nane ni seti ya kauli hizi: “‘Mungu ni roho’; na ‘Mungu aliandika Torati kwa kidole chake.’” Kutokana na kauli kwamba “Mungu ni roho” inafuata kimantiki kwamba, “Mungu hana mwili.”

Lakini, kutokana na kauli kwamba “Mungu aliandika Torati kwa kidole chake,” inafuata kimantiki kwamba, “Mungu ana mwili.” Mahitimisho mawili kwamba “Mungu ana mwili” na kwamba “Mungu hana mwili” ni matamko yanayopingana.

Mfano wa tisa ni seti ya kauli kwamba: “Mungu ni muumba na mtawala wa vitu vyote, Yesu ni Mungu, Bikira Maria aliumbwa na alikuwa anatawaliwa na Mungu, Mwanamke mwenye mimba hutawala mimba hiyo, Bikira Maria mwenye mimba alikuwa mtawala wa Mungu.”

Wakati matamko matatu ya kwanza yanazalisha hitimisho kwamba “Mungu alikuwa mtawala wa Bikira Maria,” tamko la tano linasema kwamba “Bikira Maria mwenye mimba alikuwa mtawala wa Mungu.” Huu ni mkanganyiko wa kimantiki.

Mfano wa 10 ni seti ya kauli kwamba: “Kwa hulka yake Mungu ni roho isiyo na mwili, Yesu ni Mungu, na Yesu ana mwili.”

Wakati matamko mawili ya kwanza yanazalisha hitimisho kwamba “Yesu hana mwili,” tamko la tatu linasema kwamba “Yesu ana mwili.” Huu ni mkanganyiko wa kimantiki.

Na mfano wa 11 ni seti ya kauli kwamba: “Nafsi ni kitovu cha maamuzi, Mungu ni nafsi na binadamu ni nafsi, Yesu ni Mungu-mtu, Yesu ana kitovu kimoja cha maamuzi.”

Wakati matamko matatu ya kwanza yanazalisha hitimisho kwamba “Yesu ana vitovu viwili vya maamuzi,” tamko la nne linasema kwamba “Yesu ana kitovu kimoja cha maamuzi.” Huu ni mkanganyiko wa kimantiki.

Mfano wa 12 ni seti ya sentenso hizi: "Juma amemwoa Jane; na Jane hajaolewa na Juma." Lakini, kauli ya kwanza inamaanisha hitimisho kwamba, "Jane ameolewa na Juma" pia, hitimisho linalopingana na kauli ya pili.

Mfano wa 13 ni seti ifuatayo ya kauli: “Mwana alitwaa asili ya kibinadamu; Mwana ni Mungu; Baba hakuchukua asili ya kibinadamu; Baba ni Mungu.”

Mkanganyiko unakuja kwa njia hii: Kutoka kwa kauli ya kwanza na ya pili, tuna hitimisho kwamba "Mungu alitwaa asili ya mwanadamu"; na kutoka kwa madai ya tatu na ya nne, tuna hitimisho kwamba, "Mungu hakuchukua asili ya kibinadamu". Hitimisho hizi mbili zinapingana.

Mkanganyiko daraja la tatu: Mkanganyiko uliojificha nje ya seti husika

Seti ya matamko kadhaa inakuwa na mkanganyiko wa daraja la pili endapo kuna ukinzani usio wa wazi kati ya angalau kauli mbili zilizomo katika seti hiyo, lakini ukinzani huo unaweza kufichuliwa kwa kuongeza kauli mpya katika seti, lakini kauli ambayo ukweli wake haukanushiki, na hivyo kuzalisha mkanganyiko wa daraja la kwanza au daraja la pili. (implicit contradiction)

Mfano wa kwanza ni seti ifuatayo ya kauli: “Mwana alitwaa asili ya kibinadamu; Mwana ni Mungu; hivyo, Mungu alijitwalia asili ya mwanadamu.” Seti hii haina ukinzani wazi au rasmi.

Lakini, ikiwa seti hiyo itapanuliwa kwa kuongeza kauli tatu zifuatazo, mkanganyiko hutokea: “Baba hakuchukua asili ya kibinadamu; Baba ni Mungu; hivyo, Mungu hakuchukua asili ya mwanadamu.” Sasa, madai ya tatu na sita yanapingana.

Mfano wa pili ni seti ya kauli zifuatazo: “Mungu yupo; na Shetani yupo.” Hakuna upinzani katika kauli hizi mbili; na hakuna hitimisho linaloweza kuzlaishwa kutokana na kauli hizi mbili, hadi kuibua mkanganyiko katika seti husika.

Lakini, utata utadhihirika baada ya kuongeza taarifa zifuatazo ambazo ukweli wake haukanushiki.

“Uweza wa Mungu humruhusu kuondoa uovu wa kifizikia; ukarimu wa Mungu kwa kila kitu humruhusu kutamani kuondoa uovu wa kifizikia; na ujuzi wa Mungu unaomwezesha kujua jinsi ya kuondoa uovu wa kifizikia; Kwa hiyo, Mungu mweza yote, mpenda wote na mjua yote hayupo.” Sasa, dai la sita linapingana na dai la kwanza.

Mkanganyiko unaotokana na mipaka ya uhalisia

Na kwa mujibu wa Anderson (2007), kama tukitumia kigezo cha uwezekano wa kutibika kwa mkanganyiko husika, kuna aina kuu mbili za mikanganyiko: mikanganyiko halisi na mikanganyiko isiyo halisi.

Hii aina ya pili Anderson anaiita, "merely apparent contradiction resulting from unarticulated equivocation," yaani "macrue" kwa kifupi. Naona kuwa "macrue" inazo aina ndogo mbili. Hivyo, tunapata aina kuu tatu za mikanganyiko.

Yaani, Mkanganyiko usio halisi unaotokana na mipaka ya kimaarifa (macrele), Mkanganyiko usio halisi unaotokana na utata wa kimisamiati (macrasle), na Mkanganyiko halisi unaotokana na mipaka ya uhalisia (macrole).

Mkanganyiko unaotokana na mipaka ya uhalisia wa vitu pia unaitwa mkanganyiko wa “macrole,” yaani, “most accurate contradiction resulting from ontologically limited explanantion.”

Huu ni mkanganyiko halisi na usioweza kutibika kwa kuondoa utata wa kimisamiati, hata baada ya jitihada za kutumia taarifa zote zinazoweza kukusanywa kwa msaada wa akili ya binadamu wa leo.

Unapingana na uhalisia au udhati wa vitu, yaani “the being of things” au “the essence of things.”

Mfano wa kwanza ni seti ya kauli hizi: “‘Kuna duara lenye umbo la mraba’; na ‘hakuna duara lenye umbo la mraba.’” Hakuna ulimwengu ambako duara ni mraba.

Mfano wa pili ni seti ya kauli hizi: “‘Binadamu ni mmea’; na ‘Binadamu ni mnyama.’” Hakuna ulimwengu ambako binadamu ni mmea na mnyama.

Mkanganyiko unaotokana na utata wa kimisamiati

Mkanganyiko unaotokana na utata wa kimisamiati pia unaitwa mkanganyiko wa “macrasle,” yaani “merely apparent contradiction resulting from ambiguous and semantically limited explanantion.”

Huu kuna mkanganyiko usio halisi na unaoweza kutibika kwa kuondoa utata wa kimisamiati, baada ya kutumia taarifa muhimu zilizokusanywa kwa msaada wa akili ya binadamu wa leo.

Mfano wa kwanza ni seti ya kauli hizi: “‘Nina sababu ya kufuatilia afya ya mke wangu’ na ‘sina sababu ya kufuatilia afya ya mke wangu.’”

Huu ni mkanganyiko unaotibika kama taarifa zifuatazo zikifichuliwa na msemaji: “‘Nina sababu ya kufuatilia afya ya mke wangu kwa kuwa najali ustawi wake’ na ‘sina sababu ya kufuatilia afya ya mke wangu anapokuwa yuko mikononi mwa daktari bingwa.’” Mkanganyiko umefutika.

Mfano wapili ni seti ya kauli hizi: “‘Wavulana huwa na kromozomu zenye fomati ya XY na mabinti huwa na kromozomu zenye fomati ya XX’; ‘kwa hiyo, wavulana huwa na fomati ya XY na jenitalia ya kiume na mabinti huwa na fomati ya XX na jenitalia ya kike’; na ‘Kuna mtu mwenye kromozomu zenye fomati ya XY na jenitalia kike.’”

Wakati kauli ya tatu inasema kuwa, “Kuna mtu mwenye kromozomu za fomati ya XY na jenitalia ya kike,” kauli mbili za kwanza, zinazalisha hitimisho kinzani kwamba, “Hakuna mtu mwenye kromozomu za fomati ya XY na jenitalia ya kike.”

Huu ni mkanganyiko unaotibika kama taarifa zifuatazo zikifichuliwa na msemaji:

Kisayansi, “Kuna mtu mwenye kromozomu za fomati ya XY na jenitalia ya kike, kama ni hunta” na, “Hakuna mtu mwenye kromozomu za fomati ya XY na jenitalia ya kike, kama sio hunta.” Mkanganyiko umefutika.

Mfano wa tatu ni seti ya kauli hizi: “‘Moja kujumlisha moja ni mbili’ na ‘moja kujumlisha moja ni ni kumi.’”

Lakini tarakimu mbili haziwezi kuzalisha jumla tofauti wakati ule ule nakatika mtazamo ule ule. Hata hivyo, huu ni mkanganyiko unaotibika kama taarifa zifuatazo zikifichuliwa na msemaji:

Nilimaanisha kwamba: “‘katika kizio cha kumi, moja kujumlisha moja ni mbili’ na ‘katika kizio cha pili, moja kujumlisha moja ni kumi.’” Mkanganyiko umefutika.

Mkanganyiko unaotokana na mipaka ya kimaarifa

Mkanganyiko unaotokana na utata wa kimisamiati pia unaitwa mkanganyiko wa “macrele,” yaani “merely apparent contradiction resulting from epistemologically limited explanantion.”

Huu ni mkanganyiko usio halisi na usioweza kutibika kwa kuondoa utata wa kimisamiati, hata baada ya kutumia taarifa zote zilizokusanywa na zitakazokusanywa kwa msaada wa akili ya binadamu wa leo.

Yaani, mkanganyiko huu hutokana na utata wa misamiati kwa saabu ya kufichika kwa taarifa za ziada zinazoweza kumaliza utata huo, kama zikipatikana.

Lakini, taarifa hizo haziwezi kuvunwa, kwa kutumia milango ya fahamu, kwa sababu ziko nje ya uzio wa maarifa unaobainishwa na mpaka asilia wa akili ya binadamu wa leo (human cognitive closure).

Hii maana yake ni kwamba, kuna ulimwengu wa kimaarifa ambako, mikanganyiko inayotokana na mipaka ya kimaarifa (macrele) inaweza kutibika.

Kuhusu aina hii, baadhi ya mifano inayotajwa katika fasihi andishi inahusiana na: hulka ya mungu, umwilisho wa Yesu, msukumano uliopo kati ya roho na mwili, na uhuru wa akili ya binadamu.

Mkanganyiko kuhusu hulka ya Mungu unasomeka hivi: “Mungu ni roho tupu; akili ya binadamu haiwezi kutumia milango ya fahamu kutambua kuwepo au kutokuwepo kwa roho ya Mungu popote; na kuna binadamu wanatambua kuwepo kwa Mungu.” Kauli mbili za mwisho zinapingana.

Mkanganyiko hapa ni kwamba: wanamtambua Mungu walitambuaje? Na hata kama ni kwa kuambiwa, huyo anayewambia alijuaje? Kama ni kwa kusoma maandiko ya mwanahistoria, huyo aliyeandika alijuaje?

Mkanganyiko kuhusu umwilisho wa Yesu unasomeka hivi: “Yesu ana roho ya kimungu”; na Yesu ana mwili wa kibinadamu.” Kitendawili hapa ni kwamba: inatokeaje Yesu ana mwili wa kimungu na roho ya kibinadamu?

Mkanganyiko kuhusu msukumano uliopo kati ya roho na mwili wa binadamu unasomeka hivi:

“Mawazo hayachukui nafasi yenye ujazo wowote; mwili unachukua nafasi yenye ujazo maalum;kwa hiyo, mawazo hayawezi kuingiliana na mwili.” Lakini, mawazo yanaongoza matendo ya kimwili.

Kitendawili hapa ni kwamba: inatokeaje mawazo yasiyo na mwili wenye kuchukua nafasi yaogoze mwili wenye kuchukua nafasi?

Mkanganyiko kuhusu uhuru wa akili ya binadamu unasomeka hivi:

Mosi, “mfumo wa ulimwengu ni kama wavu unaounda mtandao wa mafundo ya sababu na matokeo, kila fundo likuwa linawakilisha mtendaji au tukio mmojawapo.”

Pili, “binadamu ni sehemu ya mtandao huu wa sababu na matokeo, akiwa anashiriki kwa njia ya maamuzi na matendo anayoyafanya kwa hiari.”

Tatu, na kwa hiyo, “uhuru wake wa maamuzi unaminywa kwa sababu yeye ni sehemu ya mtandao wa sababu na matokeo.”

Lakini, inaonekana kwamba, uhuru wake wa maamuzi ya kibinadamu na mtandao wa sababu na matokeo unaomzunguka vinasikilizana, kiasi cha mfumo huu kumwachia kiwango cha uhuru anaoutumia katika fikra, maamuzi na matendo yake.

Kitendawili hapa ni kwamba: inatokeaje binadamu apate uhuru huo? Na kama anao ni uhuru kiasi gani, na hasa tukizingatia kwamba, akili yake inao mpaka asilia wa kimaarifa (cognitive closure)?

Na mkanganyiko kuhusu usawa wa kimungu kati ya Mungu Baba, Mungu Mwana, na Mungu Roho Mtakatifu linasomeka hivi:

“‘Mungu Baba anajua kila kitu, anaweza kila kitu, yuko sehemu zote, anapenda wote, yupo milele yote’; ‘Yesu na Roho Mtakatifu ni sawa na Mungu Baba kwa kila kitu’; ‘Yesu na Roho Mtakatifu hawajui kila kitu’; na ‘Yesu, Roho Mtakatifu na Mungu Baba ni sawa kwa kila kitu.’”

Kitendawili hapa ni kwamba: inawezekanaje kwamba “Yesu na Roho Mtakatifu ni sawa na Mungu kwa kila kitu” na “Yesu na Roho Mtakatifu sio sawa na Mungu kwa kila kitu”?

Majibu ya wanateolojia kuhusu tiba ya mikanganyiko

Wanateolojia kama vile Anderson na Plantinga wanasema kuwa, mikanganyiko ya kimantiki inayoonekana kwenye Misahafu ya kidini, sio halisi, bali ni mikanganyiko inayotokana na mipaka ya kimaarifa tuliyo nayo sisi wanadamu (macrele).

Kwa mfano, kitabu cha Anderson kinaweza kufupishwa katika hoja yenye muundo ufuatao kimantiki:

Mosi, mikanganyiko yote ya kimantiki inagawanyika kwenye makundi matatu, yaani “macrole,” “macrasle,” na “macrele.”

Pili, mikanganyiko ya kimantiki iliyomo katika Misahafu sio “macrole” wala “macrasle.”

Tatu, na kwa hiyo, mikanganyiko ya kimantiki iliyomo katika Misahafu ni “macrele,” ambayo ni mafumbo ya imani yanayokubaliana na kanuni za urazini na yanayopaswa kuhifadhiwa bila kuhojiwa.

Kwa maoni ya Anderson, Misahafu inasema kwamba, mikanganyiko katika Misahafu inatokana na mipaka ya kimaarifa inayoweza kutibika tu kama tukifika katika ulimwengu mwigine wa maarifa, ambako sasa hatujafika na hatuwezi kufika. Ni mafumbo ya imani yanayopaswa kuhifadhiwa, anasema.

Lakini, ndani ya Misahafu kuna taarifa zinaweza kutafsiriwa kwa kutumia akili ya kibinadamu wa leo ili kuondoa mikanganyiko ya kimantiki iliyo katika makundi ya “macrole” na “macrasle.”

Yaani, dokezo lake la pili hapo juu sio kweli kwa kuwa, katika misahafu kuna mkanganyiko ya kimantiki ya aina zote tatu, yaani “macrole,” “macrasle,” na “macrele.”

Mfano, Yesu alipokuwa kwenye mtini alithibitika kwamba hajui kila kitu. Pia Yesu aliwahi kusema kwamba yeye na Roho Mtakatifu hawajui kila kitu, isipokuw Mungu Baba pekee ndiye anajua kila kitu.

Kwa hiyo, mkanganyiko ufuatao unaweza kutibika, kwa kutumia ushahidi wa Misahafu wenye nguvu kuliko mapokeo, na akili ya binadamu inao uwezo wa kuutafsiri ushahidi huo:

Yaani, “Yesu na Roho Mtakatifu wanajua kila kitu” na “Yesu na Roho Mtakatifu hawajui kila kitu.”

Hivyo, ukweli huu unatia shaka kubwa katika majibu ya wanateolojia wetu kuhusu tiba sahihi ya mikanganyiko kimantiki.

Muhtasari, hitimisho na mapendekezo

Kwa muhtasari ninapendekeza kusema yafuatayo: Kwa kuzingatia seti ya kauli mbili, P na Q, ambapo Q ni ukanushaji wa P, yaani, Q ni sawa na sio-P, basi: tamko kwamba "P na Q", ni mkanganyiko, kwa kuwa hakuna tamko linaloweza kuwa kweli kwa wakati huo huo na kwa mtazamo ule ule.

Katika sayansi, falsafa na dini, kuna mikanganyiko mingi ya aina hii. Baadhi ni "macroles," mingine "macrasles," na mingine "macreles," kwa mujibu wa fasili zilizotolewa hapo awali.

Kwa maoni yangu, wanateolojia wetu bado hawajatuonyesha, kigezo cha kikanuni ambacho kwacho wanatofautisha kati ya hii mikanganyiko mitatu, ambayo ipo katika misahafu. Kwa mfano, hakuna kanuni zinazohalalisha utofautishaji wa mikanganyiko ifuatayo, ambayo ipo katika misahafu:

"Jua linaizunguka dunia, na dunia inazunguka jua (macrole)", na "Yesu ni mjuzi wa yote na Yesu sio mjuzi (macrele)."

Kwa hivyo, ninatilia shaka nadharia ya "fumbo la imani" kama ilivyopendekezwa na Anderson kuhusiana na mikanganyiko jamii ya "macrele."

Hivyo, ningependa kutoa wito kwa wanazuoni mamboleo kuungana katika kusaidia kusafisha "mafundisho yetu ya kijamii" kwa kuondoa aina zote za mikanganyiko ya kimantiki inayoweza kutibika leo.

Hasa, nina mapendekezo matatu muhimu. La kwanza ni kuhusu kitendawili cha ujamaa na ubepari nchini Tanzania.

Tukizingatia muundo wa sasa wa Muungano, unaobainisha wazi kati ya mambo ya Muungano na mambo yasiyo ya Muungano, tamko kwamba “Zanzibar ni nchi huru kwa mambo yasiyo ya Muungano; na Zanzibar sio nchi huru kwa mambo ya Muungano” sio mkanganyiko tena.

Mbinu hiyo inapaswa kutumika pia katika kutegua kitendawili kifuatacho cha ujamaa na ubepari: "Tanzania ni nchi ya kijamaa na Tanzania si nchi ya kijamaa."
Hapa, swali linalohitaji majibu ni: Je, Tanzania ni nchi ya kijamaa katika sera zipi na Tanzania ni nchi ya kibepari katika sera zipi?

Ni pale tu swali hili litakapojibiwa ndipo kitendawili cha ujamaa na ubepari kitatatuliwa.

Pili nina mapendekezo kuhusu mikanganyiko inayohisiana na fundidhsho la Utatu Mtakatifu.

Tukikubaliana kirazini kwamba, kwa mujibu wa misahafu, Mungu Mkuu “ni sawa na” Yaweh wa Agano la Kale; na kwamba; Yesu na Roho Mtakatifu wana Umungu wanafanana na Mungu Baba kwa kila kitu, isipokuwa hawajui kila kitu; basi matamko 12 yafuatayo yanamaliza mvutano kuhusu Utatu Mtakatifu:

(1) Mungu “ni sawa na” Yaweh; (2) Mungu “ana idadi ya” nafsi moja; (3) Baba “ana idadi ya” nafsi moja; (4) Mwana “ana idadi ya” nafsi moja; (5) Roho Mtakatifu “ana idadi ya” nafsi moja; (6) Mungu Baba “ni sawa na” Mungu; (7) Mungu Mwana “ni kama” Mungu; (8) Mungu Roho Mtakatifu “ni kama” Mungu; (9) Baba “sio sawa na” Mwana; (10) Mwana “sio sawa na” Mungu Roho Mtakatifu; (11) Roho Mtakatifu “sio sawa na” Baba; (12) Mungu “ni” dutu moja tu.

Na pendekezo la tatu ni kuhusu mikanganyiko inayohiusiana na uwemo wa Yesu katika maumbo ya mkate na divai (transubstantiation).

Hili ni fundisho kuhusu, mabadiliko ya dutu nzima ya mkate kuwa Mwili wa Kristo na dutu nzima ya divai kuwa dutu ya Damu ya Kristo. Mabadiliko haya yanaletwa katika sala ya Ekaristi kwa njia ya ufanisi wa neno la Kristo na kwa utendaji wa Roho Mtakatifu. Hata hivyo, sifa za nje za mkate na divai, ambazo ni aina ya ekaristi, hazibadiliki.

Fundisho hili halina tofauti na mafundisho ya kitapeli na kishirikina yanayotolewa na Mchungaji Mwamposa wa Tanzania.

Naona kuwa, suluhisho mwafaka ni hili hapa: Badala ya kuchukua kitenzi cha udhati wa vitu, yaani “the verb to be” kwa kimombo, “ni” kumaanisha “ni sawa na,” yaani “being as identity”; Tuchukue kitenzi cha “ni” kumaanisha “ni alama ya,” yaani “being as signification.”

Kisha, tunapata suluhisho lifuatalo: maneno “mkate huu ni mwili wangu” yanasomeaka “mkate huu ni alama ya mwili wangu”; na maneno “divai hii ni damu yangu” yanasomeaka “divai hii ni alama ya damu yangu.”

Mpaka hapo, mkanganyiko wa mkate na divai kama mwili na damu ya Yesu umefutika, tena bila kupoteza maana asilia iliyokusudiwa na Yesu, aliposema “fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu.”

Kwa ujumla, ninapendekeza kwamba taasisi ya kijamii inayoitwa "dini" ni chombo chenye jukumu la kukuza na kulinda utu wa binadamu, na wajibu huu unatokana na ukweli kwamba kila binadamu analo jukumu la kuufuata ukweli na kuukimbia upotofu.

Lakini, ikiwa dini inakubali kiholela nadharia ya fumbo la imani (mysterianism), basi, itakuwa imeipiga teke kanuni ya urazini ambayo ni msingi es heshima ya ubinadamu, na hivyo, imeamua kuikumbatia "itikadi ya Machiavellianism" kwa kiwango hicho.

Umachiaveli ni itikadi ambayo inafundisha kwamba, "malengo mema yanaweza kuhalalisha matumizi ya njia yoyote ili kuyafanikisha, hata kama mbinu husika ni haramu."

Kwa hivyo, dini za kweli zinapaswa kupinga "umachiaveli," kwa sababu hakuna "wema unaweza kuzaliwa kutokana na uovu," kama Mtakatifu Paulo alivyofundisha.

Kwa hakika, dini inayokumbatia "itikadi ya umachiaveli" inapoteza uhalali wake wa kimaadili. Kwa hivyo, majira ya taasisi za dini kujitakatifuza dhidi ya janga la kimaarifa ni sasa. Vinginevyo, tofauti inayodaiwa kuwepo kati ya dini na ushirikina wa aina ile ya Mchungaji Mwamposa wa Tanzania itatoweka.

Marejeo
  1. Alvin Plantinga, God, Freedom and Evil (Grand Rapids, Michigan: William B. Eerdmans, 1974).
  2. James Anderson, Paradox in Christian Theology: An Analysis of its Presence, Character, and Epistemic Status (Milton, Keynes, U.K.; Waynesboro, Ga.: Paternoster, 2007).
  3. Tuomas Tahko (2009), "The Law of Non-Contradiction as a Metaphysical Principle," The Australasian Journal of Logic, 7:32-47.

Chanzo: Deusdedith Kahangwa(2023), "Mtakatifu Paulo alikataza umachiaveli," Pambazuko, 29:21-23.

Tafsiri ya Kiingereza inapatikana hapa: Saint Paul, deception via equivocation and machiavellism
 
Una lengo zuri,ila ijue jamii yako,haipendi kusoma maandiko marefu.
Asante kwa andiko.
Nafahamu sana hiyo changamoto. Hivyo, kuna kuamua kati ya haya. Kupunguza ukubwa wa audience au kupunguza urefu wa andiko. Nimechagua kupunguza ukubwa wa audience, na kuweka sub-headings ili kurahisisha usomaji. Hadhira ninayoilenga hadi hapo nadhani itapokea ujumbe husika.
 
Inahitaji akili ambayo haijachafuliwa na kulishwa chakula mfu ili mtu aweze kuwa na fikra tunduizi inayowezesha kufanya uchakataji anuai wa bandiko lako.

Hongera kwa kazi njema uliyoifanya Mama Amon

Nimekuwa nikifuatilia mabandiko yako huko awali hakika nilipata chakula cha ubongo.

Usichoke kuleta vitu vinavyofikirisha ili watu wapate mawazo mbadala ya hoja kanganyifu.
 
Shuguli nzito, Sina uhakika kama watamaliza kusoma hichi kitabu maana uvivu umetawala katika maandiko haswa yakiwa marefu. Bg up broo.
 
maxresdefault.jpg

Mwaka 2020, aliyekuwa Rais wa Marekani, Baraka Obama, alihojiwa na mwandishi wa gazeti la “The Atlantic.”

Wakati wa mahojiano hayo, Baraka aliwaonya Wamarekani kuhusu “janga la kimaarifa,” yaani “epistemological crisis.”

Hii ni changamoto ambayo hujitokeza pale ambapo jamii hupoteza “uwezo wa kutofautisha kati ya ukweli na uwongo,” alisema Obama.

Seti ya sentensi unganifu ambayo imebeba kauli za kweli na kauli za uwongo” huitwa “mkanganyiko,” yaani, “paradox,” “mystery,” au “contradiction,” kwa Kiingereza. Mfano, “Tanzania ni nchi huru na Tanzania sio nchi huru.”

Lakini, kauli ile ile haiwezi kuwa kweli na isiwe kweli wakati ule ule na katika mtazamo ule ule. Sentensi yenye kubeba “mkanganyiko” wa aina hii inakuwa na tatizo la “ukanganyifu,” yaani “incoherence.”

Kwa mujibu wa Obama, “janga la kimaarifa” ni sumu katika “soko huria la mawazo,” na hivyo sumu kwa uhai wa mifumo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Kwa ajili ya kufafanua umantiki wa mtazamo huu wa Obama, na jinsi unavyotuhusu hapa Tanzania, najibu swali lifuatalo: “mkanganyiko ni kitu gani na sio kitu gani?”

Najibu swali hili kwa kutumia mawazo ya watu wawili. Kuna Alvin Plantinga (1974) na kitabu chake, “God, Freedom and Evil”; na kuna James Anderson (2007) na kitabu chake, “Paradox in Christian Theology.”

Kwa mujibu wa Plantinga (1974), kama tukitumia kigezo cha aina za kauli zinazozalisha mikanganyiko, tunaweza kubainisha mikanganyiko ya aina tatu.

Mkanganyiko ulio bayana ndani ya seti husika

Mosi, ni mkanganyiko unaotokana na ukinzani wa wazi ndani ya seti ya kauli zinazounda seti moja (explicit contradiction).

Mfano wa kwanza ni seti ya kauli hizi: “Afrika inazo nchi 54 ikiwemo Tanzanoa’; ‘kwa hiyo, Tanzania iko Afrika’; na ‘Tanzania haiko Afrika’.” Kauli ya pili na ya tatu zinapingana.

Mfano wa pili ni seti ya kauli hizi: “‘Pembetatu inazo kona tatu’; ‘kwa hiyo, pembetatu sio mraba’; na ‘Pembetatu ni mraba.’” Kauli ya tatu na nne zinapingana.

Mfano wa tatu ni seti ya kauli hizi: “‘Watanzania wote huongea Kiswahili’, ‘Juma ni Mtanzania’, kwa hiyo, ‘Juma anaongea Kiswahili’; ‘Juma haongei Kiswahili.’” Kauli ya tatu na nne zinapingana.

Mfano wa nne ni seti ya sentensi hizi: "Mimi nakupenda na Mimi sikupendi."

Mkanganyiko uliojificha ndani ya seti husika

Pili, ni mkanganyiko unaotokana na ukinzani uliojificha ndani ya kauli zinazounda seti moja, ambapo: ama kuna seti ndogo ya kauli inayozalisha hitimisho linalopingana na kauli nyingine ndani ya seti, au kuna seti ndogo mbili za kauli zinazozalisha mahitimisho yanayopingana (formal contradiction).

Mfano wa kwanza ni seti ya kauli hizi: “‘Watanzania wote huongea Kiswahili’, ‘Juma ni Mtanzania’, ‘Juma haongei Kiswahili.’”

Wakati kauli ya tatu inasema kuwa, “Juma haongei Kiswahili,” kauli mbili za kwanza, zinazalisha hitimisho kinzani kwamba, “Juma anaongea Kiswahili.”

Mfano wa pili ni seti ya kauli hizi: “‘Pembetatu inazo kona tatu’; ‘mraba unazo kona nne’; na ‘Pembetatu ni mraba.’”

Wakati kauli ya tatu inasema kuwa, “pembetatu ni mraba,” kauli mbili za kwanza, zinazalisha hitimisho kinzani kwamba, “pembetatu sio mraba.”

Mfano wa tatu ni seti ya kauli hizi: “Mungu ni nafsi tatu; Baba ni nafsi Moja; na Baba ni Mungu.” Wakati kauli ya tatu inasema “Baba ni Mungu” kauli mbili za kwanza zinazalisha hitimisho kwamba “Baba sio Mungu.”

Mfano wa nne ni seti ya kauli hizi: “Mungu ni nafsi tatu; Mwana ni nafsi Moja; na Mwana ni Mungu.” Wakati kauli ya tatu inasema “Mwana ni Mungu” kauli mbili za kwanza zinazalisha hitimisho kwamba “Mwana sio Mungu.”

Mfano wa tano ni seti ya kauli hizi: “Mungu ni nafsi tatu; Roho Mtakatifu ni nafsi Moja; na Roho Mtakatifu ni Mungu.” Wakati kauli ya tatu inasema “Roho Mtakatifu ni Mungu” kauli mbili za kwanza zinazalisha hitimisho kwamba “Roho Mtakatifu sio Mungu.”

Mfano wa sita ni seti ya kauli hizi: “Baba ni Mungu; Mwana ni Mungu; Roho Mtakatifu ni Mungu; na Kuna Mungu mmoja.” Wakati kauli ya tatu inasema “Kuna Mungu mmoja” kauli tatu za kwanza zinazalisha hitimisho kwamba “Kuna Miungu Watatu.”

Mfano wa saba ni seti ya kauli hizi: “‘Wavulana huwa na kromozomu zenye fomati ya XY na mabinti huwa na kromozomu zenye fomati ya XX’; ‘kwa hiyo, wavulana huwa na fomati ya XY na jenitalia ya kiume na mabinti huwa na fomati ya XX na jenitalia ya kike’; na ‘Kuna mtu mwenye kromozomu zenye fomati ya XY na jenitalia kike.’”

Wakati kauli ya tatu inasema kuwa, “Kuna mtu mwenye kromozomu za fomati ya XY na jenitalia ya kike,” kauli mbili za kwanza, zinazalisha hitimisho kinzani kwamba, “Hakuna mtu mwenye kromozomu za fomati ya XY na jenitalia ya kike.”

Mfano wa nane ni seti ya kauli hizi: “‘Mungu ni roho’; na ‘Mungu aliandika Torati kwa kidole chake.’” Kutokana na kauli kwamba “Mungu ni roho” inafuata kimantiki kwamba, “Mungu hana mwili.”

Lakini, kutokana na kauli kwamba “Mungu aliandika Torati kwa kidole chake,” inafuata kimantiki kwamba, “Mungu ana mwili.” Mahitimisho mawili kwamba “Mungu ana mwili” na kwamba “Mungu hana mwili” ni matamko yanayopingana.

Mfano wa tisa ni seti ya kauli kwamba: “Mungu ni muumba na mtawala wa vitu vyote, Yesu ni Mungu, Bikira Maria aliumbwa na alikuwa anatawaliwa na Mungu, Mwanamke mwenye mimba hutawala mimba hiyo, Bikira Maria mwenye mimba alikuwa mtawala wa Mungu.”

Wakati matamko matatu ya kwanza yanazalisha hitimisho kwamba “Mungu alikuwa mtawala wa Bikira Maria,” tamko la tano linasema kwamba “Bikira Maria mwenye mimba alikuwa mtawala wa Mungu.” Huu ni mkanganyiko wa kimantiki.

Mfano wa 10 ni seti ya kauli kwamba: “Kwa hulka yake Mungu ni roho isiyo na mwili, Yesu ni Mungu, na Yesu ana mwili.”

Wakati matamko mawili ya kwanza yanazalisha hitimisho kwamba “Yesu hana mwili,” tamko la tatu linasema kwamba “Yesu ana mwili.” Huu ni mkanganyiko wa kimantiki.

Na mfano wa 11 ni seti ya kauli kwamba: “Nafsi ni kitovu cha maamuzi, Mungu ni nafsi na binadamu ni nafsi, Yesu ni Mungu-mtu, Yesu ana kitovu kimoja cha maamuzi.”

Wakati matamko matatu ya kwanza yanazalisha hitimisho kwamba “Yesu ana vitovu viwili vya maamuzi,” tamko la nne linasema kwamba “Yesu ana kitovu kimoja cha maamuzi.” Huu ni mkanganyiko wa kimantiki.

Mfano wa 12 ni seti ya sentenso hizi: "Juma amemwoa Jane; na Jane hajaolewa na Juma." Lakini, kauli ya kwanza inamaanisha hitimisho kwamba, "Jane ameolewa na Juma" pia, hitimisho linalopingana na kauli ya pili.

Mkanganyiko uliojificha nje ya seti husika

Tatu, ni mkanganyiko unaotokana na ukinzani uliofichika katitika seti ya kauli ambazo hazipingani wazi wazi, na hata mahitimisho yake hayapingani kwa namna yoyote, isipokuwa kwa kuongeza kauli mpya, angalau moja, ambayo ukweli wake haukanushiki (implicit contradiction).

Mfano ni seti ya kauli zifuatazo: “Mungu yupo; na Shetani yupo.” Hakuna upinzani katika kauli hizi mbili; na hakuna hitimisho linaloweza kuzlaishwa kutokana na kauli hizi mbili, hadi kuibua mkanganyiko katika seti husika.

Lakini, ukinzani utabainika baada ya kuongeza kauli zifuatazo ambazo ukweli wake ni wa lazima.

“Mungu mweza yote angeweza kumwua shetani; Mungu mpenda wote angependa kumwua shetani; Mungu mjua yote angejua namna ya kumwua shetani; Kwa hiyo, ama Mungu yupo na Shetani hayupo au Mungu hayupo na Shetani yupo.”

Katika seti hii, kauli tatu za kwanza, zimezalisha hitimisho linalopingana na kauli ya awali kwamba “Mungu yupo na Shetani yupo.”

Mkanganyiko unaotokana na mipaka ya uhalisia

Na kwa mujibu wa Anderson (2007), kama tukitumia kigezo cha uwezekano wa kutibika kwa mkanganyiko husika, kuna aina kuu tatu za mikanganyiko.

Hapa, nitazitaja aina hizo tatu kama Mkanganyiko unaotokana na mipaka ya kimaarifa (macrele), Mkanganyiko unaotokana na utata wa kimisamiati (macrasle), na Mkanganyiko unaotokana na mipaka ya uhalisia (macrole).

Mkanganyiko unaotokana na mipaka ya uhalisia wa vitu pia unaitwa mkanganyiko wa “macrole,” yaani, “most accurate contradiction resulting from ontologically limited explanantion.”

Huu ni mkanganyiko halisi na usioweza kutibika kwa kuondoa utata wa kimisamiati, hata baada ya jitihada za kutumia taarifa zote zinazoweza kukusanywa kwa msaada wa akili ya binadamu wa leo.

Unapingana na uhalisia au udhati wa vitu, yaani “the being of things” au “the essence of things.”

Mfano wa kwanza ni seti ya kauli hizi: “‘Kuna duara lenye umbo la mraba’; na ‘hakuna duara lenye umbo la mraba.’” Hakuna ulimwengu ambako duara ni mraba.

Mfano wa pili ni seti ya kauli hizi: “‘Binadamu ni mmea’; na ‘Binadamu ni mnyama.’” Hakuna ulimwengu ambako binadamu ni mmea na mnyama.

Mkanganyiko unaotokana na utata wa kimisamiati

Mkanganyiko unaotokana na utata wa kimisamiati pia unaitwa mkanganyiko wa “macrasle,” yaani “merely apparent contradiction resulting from ambiguous and semantically limited explanantion.”

Huu kuna mkanganyiko usio halisi na unaoweza kutibika kwa kuondoa utata wa kimisamiati, baada ya kutumia taarifa muhimu zilizokusanywa kwa msaada wa akili ya binadamu wa leo.

Mfano wa kwanza ni seti ya kauli hizi: “‘Nina sababu ya kufuatilia afya ya mke wangu’ na ‘sina sababu ya kufuatilia afya ya mke wangu.’”

Huu ni mkanganyiko unaotibika kama taarifa zifuatazo zikifichuliwa na msemaji: “‘Nina sababu ya kufuatilia afya ya mke wangu kwa kuwa najali ustawi wake’ na ‘sina sababu ya kufuatilia afya ya mke wangu anapokuwa yuko mikononi mwa daktari bingwa.’” Mkanganyiko umefutika.

Mfano wapili ni seti ya kauli hizi: “‘Wavulana huwa na kromozomu zenye fomati ya XY na mabinti huwa na kromozomu zenye fomati ya XX’; ‘kwa hiyo, wavulana huwa na fomati ya XY na jenitalia ya kiume na mabinti huwa na fomati ya XX na jenitalia ya kike’; na ‘Kuna mtu mwenye kromozomu zenye fomati ya XY na jenitalia kike.’”

Wakati kauli ya tatu inasema kuwa, “Kuna mtu mwenye kromozomu za fomati ya XY na jenitalia ya kike,” kauli mbili za kwanza, zinazalisha hitimisho kinzani kwamba, “Hakuna mtu mwenye kromozomu za fomati ya XY na jenitalia ya kike.”

Huu ni mkanganyiko unaotibika kama taarifa zifuatazo zikifichuliwa na msemaji:

Kisayansi, “Kuna mtu mwenye kromozomu za fomati ya XY na jenitalia ya kike, kama ni hunta” na, “Hakuna mtu mwenye kromozomu za fomati ya XY na jenitalia ya kike, kama sio hunta.” Mkanganyiko umefutika.

Mfano wa tatu ni seti ya kauli hizi: “‘Moja kujumlisha moja ni mbili’ na ‘moja kujumlisha moja ni ni kumi.’”

Lakini tarakimu mbili haziwezi kuzalisha jumla tofauti wakati ule ule nakatika mtazamo ule ule. Hata hivyo, huu ni mkanganyiko unaotibika kama taarifa zifuatazo zikifichuliwa na msemaji:

Nilimaanisha kwamba: “‘katika kizio cha kumi, moja kujumlisha moja ni mbili’ na ‘katika kizio cha pili, moja kujumlisha moja ni kumi.’” Mkanganyiko umefutika.

Mkanganyiko unaotokana na mipaka ya kimaarifa

Mkanganyiko unaotokana na utata wa kimisamiati pia unaitwa mkanganyiko wa “macrele,” yaani “merely apparent contradiction resulting from epistemologically limited explanantion.”

Huu ni mkanganyiko usio halisi na usioweza kutibika kwa kuondoa utata wa kimisamiati, hata baada ya kutumia taarifa zote zilizokusanywa na zitakazokusanywa kwa msaada wa akili ya binadamu wa leo.

Yaani, mkanganyiko huu hutokana na utata wa misamiati kwa saabu ya kufichika kwa taarifa za ziada zinazoweza kumaliza utata huo, kama zikipatikana.

Lakini, taarifa hizo haziwezi kuvunwa, kwa kutumia milango ya fahamu, kwa sababu ziko nje ya uzio wa maarifa unaobainishwa na mpaka asilia wa akili ya binadamu wa leo (human cognitive closure).

Hii maana yake ni kwamba, kuna ulimwengu wa kimaarifa ambako, mikanganyiko inayotokana na mipaka ya kimaarifa (macrele) inaweza kutibika.

Kuhusu aina hii, baadhi ya mifano inayotajwa katika fasihi andishi inahusiana na: hulka ya mungu, umwilisho wa Yesu, msukumano uliopo kati ya roho na mwili, na uhuru wa akili ya binadamu.

Mkanganyiko kuhusu hulka ya Mungu unasomeka hivi: “Mungu ni roho tupu; akili ya binadamu haiwezi kutumia milango ya fahamu kutambua kuwepo au kutokuwepo kwa roho ya Mungu popote; na kuna binadamu wanatambua kuwepo kwa Mungu.” Kauli mbili za mwisho zinapingana.

Mkanganyiko hapa ni kwamba: wanamtambua Mungu walitambuaje? Na hata kama ni kwa kuambiwa, huyo anayewambia alijuaje? Kama ni kwa kusoma maandiko ya mwanahistoria, huyo aliyeandika alijuaje?

Mkanganyiko kuhusu umwilisho wa Yesu unasomeka hivi: “Yesu ana roho ya kimungu”; na Yesu ana mwili wa kibinadamu.” Kitendawili hapa ni kwamba: inatokeaje Yesu ana mwili wa kimungu na roho ya kibinadamu?

Mkanganyiko kuhusu msukumano uliopo kati ya roho na mwili wa binadamu unasomeka hivi:

“Mawazo hayachukui nafasi yenye ujazo wowote; mwili unachukua nafasi yenye ujazo maalum;kwa hiyo, mawazo hayawezi kuingiliana na mwili.” Lakini, mawazo yanaongoza matendo ya kimwili.

Kitendawili hapa ni kwamba: inatokeaje mawazo yasiyo na mwili wenye kuchukua nafasi yaogoze mwili wenye kuchukua nafasi?

Mkanganyiko kuhusu uhuru wa akili ya binadamu unasomeka hivi:

Mosi, “mfumo wa ulimwengu ni kama wavu unaounda mtandao wa mafundo ya sababu na matokeo, kila fundo likuwa linawakilisha mtendaji au tukio mmojawapo.”

Pili, “binadamu ni sehemu ya mtandao huu wa sababu na matokeo, akiwa anashiriki kwa njia ya maamuzi na matendo anayoyafanya kwa hiari.”

Tatu, na kwa hiyo, “uhuru wake wa maamuzi unaminywa kwa sababu yeye ni sehemu ya mtandao wa sababu na matokeo.”

Lakini, inaonekana kwamba, uhuru wake wa maamuzi ya kibinadamu na mtandao wa sababu na matokeo unaomzunguka vinasikilizana, kiasi cha mfumo huu kumwachia kiwango cha uhuru anaoutumia katika fikra, maamuzi na matendo yake.

Kitendawili hapa ni kwamba: inatokeaje binadamu apate uhuru huo? Na kama anao ni uhuru kiasi gani, na hasa tukizingatia kwamba, akili yake inao mpaka asilia wa kimaarifa (cognitive closure)?

Na mkanganyiko kuhusu usawa wa kimungu kati ya Mungu Baba, Mungu Mwana, na Mungu Roho Mtakatifu linasomeka hivi:

“‘Mungu Baba anajua kila kitu, anaweza kila kitu, yuko sehemu zote, anapenda wote, yupo milele yote’; ‘Yesu na Roho Mtakatifu ni sawa na Mungu Baba kwa kila kitu’; ‘Yesu na Roho Mtakatifu hawajui kila kitu’; na ‘Yesu, Roho Mtakatifu na Mungu Baba ni sawa kwa kila kitu.’”

Kitendawili hapa ni kwamba: inawezekanaje kwamba “Yesu na Roho Mtakatifu ni sawa na Mungu kwa kila kitu” na “Yesu na Roho Mtakatifu sio sawa na Mungu kwa kila kitu”?

Majibu ya wanateolojia kuhusu tiba ya mikanganyiko

Wanateolojia kama vilr Anderson na Plantinga wanasema kuwa, mikanganyiko ya kimantiki inayoonekana kwenye Misahafu ya kidini, sio halisi, bali ni mikanganyiko inayotokana na mipaka ya kimaarifa tuliyo nayo sisi wanadamu (macrele).

Kwa mfano, Anderson anaonekana kujenga hoja yenye muundo ufuatao kimantiki:

Mosi, mikanganyiko ya kimantiki iliyomo katika Misahafu ama ni “macrole,” au “macrasle,” au “macrele.”

Pili, mikanganyiko ya kimantiki iliyomo katika Misahafu sio “macrole” wala “macrasle.”

Tatu, na kwa hiyo, mikanganyiko ya kimantiki iliyomo katika Misahafu ni “macrele.”

Kwa maoni yake, Misahafu inasema kwamba, mikanganyiko katika Misahafu inatokana na mipaka ya kimaarifa inayoweza kutibika tu kama tukifika katika ulimwengu mwigine wa maarifa, ambako sasa hatujafika na hatuwezi kufika.

Lakini, ndani ya Misahafu kuna taarifa zinaweza kutafsiriwa kwa kutumia akili ya kibinadamu wa leo kuondoa baadhi ya mikanganyiko ya kimantiki.

Yaani, katika misahafu kuna mkanganyiko ya kimantiki ya aina zote tatu, yaani “macrole,” “macrasle,” au “macrele,” ambapo mikanganyiko jamii ya “macrasle” inatibika leo.

Mfano, Yesu alipokuwa kwenye mtini alithibitika kwamba hajui kila kitu. Pia Yesu aliwahi kusema kwamba yeye na Roho Mtakatifu hawajui kila kitu, isipokuw Mungu Baba pekee ndiye anajua kila kitu.

Kwa hiyo, mkanganyiko ufuatao unaweza kutibika, kwa kutumia ushahidi wa Misahafu wenye nguvu kuliko mapokeo, na akili ya binadamu inao uwezo wa kuutafsiri ushahidi huo:

Yaani, “Yesu na Roho Mtakatifu ni sawa na Mungu kwa kila kitu” na “Yesu na Roho Mtakatifu sio sawa na Mungu kwa kila kitu.”

Hivyo, ukweli huu unatia shaka kubwa katika majibu ya wanateolojia wetu kuhusu tiba sahihi ya mikanganyiko kimantiki.

Hitimisho na mapendekezo

Ukweli ni kwamba, wanateolojia wetu hawajaonyesha ni kwa vipi, kwenye misahafu, wanatofautisha kati ya mikanganyiko ya kimantiki inayotibika na isiyoweza kutibika. Kwa hiyo, hapa natofautiana na kina Anderson na Plantinga.

Tunafahamu kuwa, ndani na nje ya misahafu, kuna mikanganyiko ya kimantiki inayotibika kwa kutumia maarifa yanayoweza kuvunwa kwa kutumia akili ya binadamu wa leo.

Hivyo, wito wangu ni kwamba, wanazuoni mamboleo tusaidiane kusafisha “imani ya jamii” kwa kuwaepusha watu wote na mikanganyiko ya kimantiki inayotibika.

Napendekeza kwamba, taasisi inayoitwa “Kanisa” ni chombo cha kukuza na kuhami heshima ya ubinadamu.

Lakini, kama Kanisa linakubali kuwa nyenzo ya kusigina heshima ya ubinadamu linakuwa limeamua kukumbatia “itikadi ya umachiaveli.” Yaani, itikadi kwamba “lengo zuri linaweza kuhalalisha mbinu yoyote, ikiwemo mbinu haramu.”

Hivyo, Kanisa linapaswa kuupinga “umachiaveli,” kwa kuwa “ubaya hauwezi kuzaa wema,” kama Mtakatifu Paulo alivyofundisha.

Kwa hiyo, Kanisa linalokumbatia “itikadi ya umachiaveli” hupoteza uhalali wa kimaadili. Mwaka wa Kanisa kujitakatifuza ni sasa.

Chanzo: Pambazuko, toleo namba 029, uk. 21-23.
Unisaidie tu, hili ni somo gani? Linanisaidia vipi?
 
Unisaidie tu, hili ni somo gani? Linanisaidia vipi?
Hebu tuanzie mfano huu uliomo kwenye andiko:

  1. “‘Watanzania wote huongea Kiswahili’,
  2. ‘Juma ni Mtanzania’,
  3. Kwa hiyo, ‘Juma haongei Kiswahili’.
Seti hii inazo kauli tatu. Kauli ya tatu hi hitimisho kutokana na kauli mbili za kwanza.

Lakini, hitimisho halitokani na kauli mbili za kwanza.

Hitimisho sahihi lilipaswa kuwa: "Kwa hiyo, JUma anaongea Kiswahili"

Lakini bado, tunao watu wengi wanafikiri kwa mtindi huo unaoendana na upotofu wa kimantiki.

Na huu ndio mfano hai wa janga la kimaarifa (epistemological crisis) linaloongelewa.

Kwa lugha nyepesi, janga la kimaarifa kimaarifa (epistemological crisis) ni udodoki wa kifikra.

Dodoki huwa linazoa kila kitu kinachofaa na kisichofaa--nyasi, nywele, manyoya, na kila kitu.

Katika jamii yetu ya Afrika, na kidogo huko nje ya Afrika, hili ni tatizo sugu.

Ni ugonjwa unatishia heshima ya ubinadamu, maana kila binadamu analo jukumu la kuutafuta ukweli na kuukimbia upotofu.

Lakini, sisi Waafrika wengi tunafanya kinyume.

Hata tuna vitivo katika seminari zetu vinaandaa watetezi wa kile kinachoitwa "mafundisho msingi," yaani "dogmatic theology". Huwa naita "teolojia ya kutetea mawazo mgando," maana neno DOGMA ndio tafsiri yake hasa.

Kwa maoni yangu, watetezi wa "mafundishi msingi," na hasa yale yenye kubeba mikanganyiko ya kimantiki wanafanya, umachiaveli wa kuwamezesha watu fikra potofu kwa nguvu, na hivyo kufanya uhalifu dhidi ya utu.

Hadi baadhi ya wazungu wanasema "Waafrika ni binadamu daraja la pili"; kwamba sisi ni kama dodoki; kila tunachoambiwa tunameza bila kuchuja.

Wafrika makini hatupaswi kukumbatia udodoki wa kifikra.

Hivyo, wito wa mwandishi ni kwamba, tuchukue hatua kutibu ugonjwa huu.

Hope this helps...
 
Shuguli nzito, Sina uhakika kama watamaliza kusoma hichi kitabu maana uvivu umetawala katika maandiko haswa yakiwa marefu. Bg up broo.
Hadhira iliyolengwa ni wanazuoni waliofunzwa na kuhitimu katika masuala ya usanifu na uchambuzi wa fasihi andishi.

Hawa wameandika tasnifu za uzamili na uzamivu zenye kurasa 250+, sawa na maneno 250,000

Makala hii inayo maneo 4,000 sawa na kurasa kama 10 hivi

Kwao sioni kama urefu huu ni tatizo hata kidogo
 
Uzi mzuri saana,je ilisoma? Falsafa?
Nimesoma masuala haya katika falsafa:
  1. Descriptive philosophy: This is First order knowledge. It includes
    1. Ontology,
    2. Logic,
    3. epistemology,
    4. Psychology,
    5. Cosmology,
    6. Semiotics,
    7. Mereology,
    8. Theodicy, etc.
  2. Normative Philosophy: This is Second order knowledge,that depends on first order knowledge. It includes
    1. ethics,
    2. axiology,
    3. Agathology, etc.
  3. Applied philosophy: This is Third order knowledge that depends both on first and second order knowledges.It includes
    1. philosophy of causality,
    2. philosophy of politics,
    3. philosophy of economics,
    4. philosophy of sex,
    5. philosophy of technology,
    6. philosophy of medicine,
    7. philosophy of religion,
    8. philosophy of sports,
    9. philosophy of education,
    10. philosophy of science,
    11. philosophy of marriage,
    12. philosophy of peace and war,
    13. philosophy of society,
    14. philosophy of management,
    15. philosophy of law,
    16. philosophy of history,
    17. philosophy of mathematics,
    18. philosophy of counselling,
    19. philosophy of consultancy,
    20. philosophy of business, etc.
Na bado naendelea kujielimisha.
 
Nimesoma haya:
  1. Descriptive philosophy (metaphysics, logic, epistemology, etc)--First order knowledge
  2. Normative Philosophy (ethics, axiology, etc)--Second order knowledge
  3. Applied philosophy (political philosophy, economic philosophy, sexual philosophy, technological philosophy, medical philosophy, religious philosophy, sports philosophy, etc)--Third order knowledge
Na bado naendelea kujielimisha.
Mkuu ww n padre au?
Upo nondo sana kwenye falsafa.

Sent from my M10_Max using JamiiForums mobile app
 
Nimekutana na msamiati mpya kwangu ambao sijauelewa maana yake , umachiaveli maana yake please.
 
Nimesoma haya:
  1. Descriptive philosophy: This is First order knowledge. It includes
    1. metaphysics,
    2. logic,
    3. epistemology, etc.
  2. Normative Philosophy: This is Second order knowledge,that depends on first order knowledge. It includes
    1. ethics,
    2. axiology, etc.
  3. Applied philosophy: This is Third order knowledge that depends both on first and second order knowledges.It includes
    1. philosophy of politics,
    2. philosophy of economics,
    3. philosophy of sex, philosophy of technology,
    4. philosophy of medicine,
    5. philosophy of religion,
    6. philosophy of sports,
    7. philosophy of education,
    8. philosophy of science,
    9. philosophy of marriage,
    10. philosophy of peace and war,
    11. philosophy of society,
    12. philosophy of management, etc.
Na bado naendelea kujielimisha.
Sikuwahi kujua kama philosophy ina mapana kiasi hiki.
 
Nafurahi sana kukutana na mada fikirishi namna hii, japo inaweza kuwa juu ya upeo wangu lakini sijakosa mawili matatu ambayo yameacha tafakari ya kina kwenye fikra na mtazamo wangu kwenye imani yangu.

Katika mafundisho ya msingi kwenye imani , ni kwamba imani ni kuwa na uhakika na jambo fulani, haijalishi lipo au halipo ila likishaitwa la Kiimani basi moja kwa moja linapaswa kuwepo.

Imani hupatikana kwa kusikia, kwa hiyo ili kuweza kuwa na imani inakupasa kusikia kwanza.

Katika mafundisho ya imani yangu kuna kitu kinaitwa fumbo la imani.
Najaribu kufikiria maana ya fumbo la imani , inaweza kuwa ni kitu kilichofichika lakini kipo.
Au kimefunuliwa kwa baadhi ya walengwa lakini kwa ujumla kipo.
Naweza kusema ni kama code ambayo naweza kuifungua, au kutoweza kuifungua au kuwezeshwa kufungua, au kufunguliwa na mwenye kuijua.

Hili fumbo la imani limebeba mengi sana ambayo akili ya kimantiki inayakataa kama mada hiii inavyo eleza.

Mwishoni mwa hii mada umesema ni wakati wa kanisa kujitakatifuza , naam nakubaliana nawe kwa kiasi Kibwana sasa iwe rasmi kanisa kusema ukweli.

Maana kwa mfano kanisa langu kuna viapo vitatu kwa wachungaji wake, ambavyo ni utii, useja, na ufukara.

Hiko cha utii ni kutii kila kitu unacho ambiwa hatakama wewe unaona sivyo ila kama kimetoka kwa mkuu wako basi inakupasa kutii.

Unaweza ukaona kitu fulani kwa rangi mfano nyeupe lakini mkuu wako akakuambia ile ni nyeusi, wewe unatakiwa uamini na kujua ni nyeusi hata kama akili yako inaona ni nyeupe.

Hili limepelekea uwepo wa mafundisho yenye shida unapo ya tazama kwa akili nje ya imani.

Changamoto nyingine ni kuwa kwa sasa wigo wa elimu umekua mpana sana kupelekea kufunguka kwa fikra na mitazamo kwa watu wengi.

Na kwa mfumo huu kama kweli kanisa halitaji tafakari upya mafundisho yake, miaka 100 mbele sidhani kama litakua kama lilivyo sasa.
 
Nafahamu sana hiyo changamoto. Hivyo, kuna kuamua kati ya haya. Kupunguza ukubwa wa audience au kupunguza urefu wa andiko. Nimechagua kupunguza ukubwa wa audience, na kuweka sub-headings ili kurahisisha usomaji. Hadhira ninayoilenga hadi hapo nadhani itapokea ujumbe husika.
Andiko bora sana ila umewaandikia Watanzania! Liwe kwenye kiingereza then share uone wenzetu wanaopenda kuchangamsha akili itavyokuwa.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom