Torra Siabba
Senior Member
- Jul 24, 2016
- 105
- 102
Mwanza ni Jiji la pili Tanzania linalokua kwa kasi kutokana na Wingi wa watu na miradi mikubwa ya kimkakati ambayo imejengwa kwenye jiji hilo, Lakini mbaya zaidi ni kwamba takribani mikoa yote ya Tanzania ukiacha mkoa wa Mara huingia Mwanza kupitia njia kuu ya Shinyanga, kisha Buhongwa na Baadae Mwanza mjini.
Kwa wale wazoefu wakati unakaribia kuingia Mwanza mjini kuna eneo linaitwa "MSWAHILI" ni eneo maarufu la kuuza gadaa wabichi mida ya Asubuhi.
Eneo hili kiukweli limekuwa kero kwakua linatoa harufu mbaya na Uozo kutokana na wananchi kuanika Uduvi ambao hutumika kama chakula cha Kuku, sasa Ardhi ya eneo hilo imeshakua sugu kiasi kwamba ukifika eneo hilo la Mswahili Harufu utakayokutana nayo ni kali sana kiasi kwamba unamuomba Mungu mharakishe kupita ili harufu hiyo iwapite maana ni kali mno.
Hivyo kwa Kujali maslahi ya jiji kubwa kama Mwanza serikali ya jiji hilo inatakiwa kuhamisha shughuli za kuanika huo Uduvi eneo hilo ili Harufu hiyo isiwepo maana kwa hali ilivyo sasa utadhani kuna Mizoga imefufuliwa.
============
TAMKO LA MAMLAKA
Mkurugenzi wa Jiji Mwanza, Yahya Sekiete amesema "Kwanza eneo hilo linatumiwa hasa majira ya asubuhi kama sehemu ya kupokelea dagaa, lakini dagaa wanapokuwepo popote pale harufu haikosekani.
"Pia Mwalo unasaidia wananchi wetu wa hali ya chini ambao ndio asilimia kubwa wanaofanya biashara eneo hilo, lakini Serikali ina mradi wa kujenga soko kubwa la kimkakati, mradi utakapokamilika automatic huo Mwalo wa Mswahili utaisha.
"Kuhusu masuala ya usafi wa eneo hilo, nitafika eneo la tukio ili kufanya ziara kuona kama kuna mazingira ambayo ni machafu na yanakiuka afya."

Mitaa ya Mswahili