Msumbiji: Basi la Kampuni ya Nagi Investment lapata ajali ya kupinduka, 4 wafariki

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Basi la Kampuni ya Nagi Investment linalofanya safari zake kati ya mkoa wa Zambezia, Quelimane kwenda mkoa wa Sofala, Beira, limepata ajali ya kupinduka na kuua watu wanne nchini Msumbiji.

Taarifa zilizoripotiwa zikieleza chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa dereva wa basi hilo aina ya Zhongtong Climber.

Kampuni ya Nagi Investment inamilikiwa na Mtanzania aliyefanya uwekezaji nchi jirani ya Msumbiji.
IMG_20181119_230335_644.jpeg
IMG_20181119_230316_214.jpeg
 
Poleni sana..Mungu atuhifadhi atuepushe na majanga haya ya ajali
 
RIP kwa waliotangulia mbele za haki na pole kwa majeruhi wote Mungu awape uponyaji wa haraka kama atakavyo.
Mkuu naona umeanza kuwa international accident reporter.
Keep it man.
 
Naifahamu hiyo njia baada ya kupita sehemu inahitwa Chimoio njia panda ya kwenda Zimbabwe wanalipa sana ndizi. Msumbiji barabara yenye lami moja kwa moja kuunganisha mkoa na mkoa ni ile ya kutoka Tete kwenda Maputo. Umbali wake ni kilometa 1526. Uzuri magari yanasafiri usiku kucha mnafika Maputo asubuhi, lakini Msumbiji ni moja ya nchi yenye mabasi ya hovyo mno ya abiria. Huyo Mtanzania angalau amepeleka mabasi ya kisasa
 
Asante mkuu kwa kutujuza kiasi cha haja
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom