Msolopa Investment Company Ltd (MICL)

Game Theory

Platinum Member
Sep 5, 2006
8,545
835
Kama unadaiwa na serikali basi hawa ndio watakuja kukudai

Madalali 11 waomba kukusanya Fedhaza Ufisadi..



KAMPUNI 11 za udalali zimeomba zipewe kazi ya kukusanya Sh bilioni 199 zilizochotwa serikalini na ‘wajanja’ kupitia Mpango wa Uagizaji wa Bidhaa Nje (CIS), lakini zikatumika kwa matumizi mengine bila kurudishwa. Wizara ya Fedha na Uchumi inalazimika kutumia madalali kukusanya fedha hizo kutokana na watu waliochota fedha hizo kwa kisingizio cha kuagiza bidhaa nje kugoma kuzirudisha kama mkataba ulivyowataka kufanya.

Jana ilikuwa siku ya mwisho ya kuwasilisha zabuni za kufanya kazi hiyo ya kukusanya mabilioni hayo ya fedha. Hadi kufikia saa nne jana, kampuni 11 ndizo zilikuwa zimewasilisha maombi ya zabuni hiyo.

Kampuni itakayopewa kazi hiyo italazimika kukusanya madeni hayo kutoka kwa watu na kampuni zipatazo 916 ambazo zilikopeshwa Yeni ya Japan Bilioni 16 (Sh bilioni 199). Watu hao wamegoma kurejesha fedha hizo, kitendo kinachotafsiriwa kuwa ni ufisadi dhidi ya fedha za umma.

Kampuni za udalali zilizoomba kufanya kazi hiyo ni Yono Auction Mart, Majengo Auction Mart, Rhino Auction Mart, Msolopa Investment Co Ltd, Bani Investment Ltd, Kitindi Co Ltd, GM Auction, Mpoki & Associates Advocates, Nakara Auction Mart, Aslyla Attorneys & TMK Enterprises na Rex Attorney. Kila kampuni ambayo imeomba kufanya kazi hiyo imeambatanisha dhamana ya Sh milioni mbili na mapendekezo ya riba inayoombwa ilipwe kutokana na kiasi cha fedha itakachokusanya.

Wizara ya Fedha na Uchumi imeitisha zabuni hiyo huku tayari ikiwa imeshatishia kuwaanika hadharani na kuwachukulia hatua za kisheria watu waliochota fedha hizo kama hawatalipa deni hilo ndani ya miezi mitatu tangu tangazo hilo lianze kutoka kwenye vyombo vya habari.Miongoni mwa wadaiwa hao wamo wafanyabiashara maarufu nchini, wanasiasa wakiwamo wabunge na baadhi ya maofisa wa serikali.Habari hii kwa msaada wa Shadrack Sagati
 
Malizia basi mkuu Msolopa kwa nini awe kwenye heading? Ama naye anadaiwa na serekali?
 
Kama unadaiwa na serikali basi hawa ndio watakuja kukudai

Hapa sijaelewa vizuri;

Kama jana ilikuwa mwisho wa kuomba zabuni hiyo....je Tenda board ya Hazina ilikaa saa ngapi na kuipitisha Msolopa? au heading yako haijaka vyema?

Nikiacha hilo....! hicho wanachotaka kukifanya Haziza ni Ufisadi juu ya Ufisadi? Jamaani situliambiwa fedha za EPA zilikuwa na uhusiano na CIS (Mpango wa kuagiza bidhaa toka nje) au network yangu haikamati vyema hapa?
 
Mbona nilisikia siku moja Msolopa wakitangaza katika RFA notice kwa wadaiwa wa pesa hiyo? ina maana walipewa wao hiyo kazi? ni kama wiki mbili sasa! au nilisikia vibaya? Iweje watu waseme matokeo ya tenda hayajatangazwa?
 
NINACHOJUA ni kuwa wenye kumiliki magazeti haya ni walewale waliomiliki yale yaliyomkapenia Aliyeko madarakani hadi akaingia Ikulu.

Jamaa hawa wanatumika tu kama kinyago usoni mwa mtu halisi. Isitoshe jamaa hawa wameungana na makundi fulani ya kijamii na kiimani wakiwa na lengo la kuona kwamba jamaa harejei madarakani baada ya 2010, yaani, akienda kuona World Cup Afrika Kusini atakuwa na miezi 4 au 5 tu tena Ikulu. Baada ya hapo anakuwa raia wa kawaida.

Mkakati wao unasaidiwa na watu kadhaa Ikulu, taasisi za dini na kibiashara pamoja na jamaa wa nje ambao tayari walikwishaanza miradi kadhaa na kundi hilo linalompiga vita JK wakati baadhi yao wakiwa ndani ya serikali.
 
NINACHOJUA ni kuwa wenye kumiliki magazeti haya ni walewale waliomiliki yale yaliyomkapenia Aliyeko madarakani hadi akaingia Ikulu.

Jamaa hawa wanatumika tu kama kinyago usoni mwa mtu halisi. Isitoshe jamaa hawa wameungana na makundi fulani ya kijamii na kiimani wakiwa na lengo la kuona kwamba jamaa harejei madarakani baada ya 2010, yaani, akienda kuona World Cup Afrika Kusini atakuwa na miezi 4 au 5 tu tena Ikulu. Baada ya hapo anakuwa raia wa kawaida.

Mkakati wao unasaidiwa na watu kadhaa Ikulu, taasisi za dini na kibiashara pamoja na jamaa wa nje ambao tayari walikwishaanza miradi kadhaa na kundi hilo linalompiga vita JK wakati baadhi yao wakiwa ndani ya serikali.

Huduma nafikiri hii post yako ina thread yake utakuwa umeziconfuse!
 
Mbona nilisikia siku moja Msolopa wakitangaza katika RFA notice kwa wadaiwa wa pesa hiyo? ina maana walipewa wao hiyo kazi? ni kama wiki mbili sasa! au nilisikia vibaya? Iweje watu waseme matokeo ya tenda hayajatangazwa?

Hii tenda ilishapewa kwa kampuni ya Msolopa wiki chache zilizopita.

This Day said:




Debt collectors zero
in on Manji



A DEBT collector hired by the government to recover more than 180bn/- from the Commodity Import Support (CIS) scam has confirmed that prominent businessman Yusuf Manji is among the biggest debtors on the list.

Debt collectors have thus far established that the chief executive officer of Quality Group Limited is behind a string of companies that benefited from the CIS funds, but held back in repaying the money to the government.

As a one-week ultimatum given to the CIS debtors to pay up has formally expired, it has emerged that Manji has already returned some of the funds but is yet to clear his ’massive’ debt.

Ibrahimu Msolopa, the Executive Director of Msolopa Investment Company Limited, a debt collection agency commissioned by the Ministry of Finance and Economic Affairs to recover the CIS funds, confirmed to THISDAY that Manji was among the high-profile debtors on the list.

He revealed that the controversial businessman has paid some of the debts, but was yet to settle the full amount of money he received from the CIS fund, which amounts to billions of shillings.

’’Manji took many loans from CIS -- both small and large -- through his various companies. However, only a few of his companies have so far paid the debts, while others are continuing to pay up,’’ he explained.

According to THISDAY investigations, Yusuf Manji, who is strongly linked to the import support scam is believed to have pocketed tens of billions of shillings out of the CIS scheme.

Msolopa could not immediately confirm Manji’s total debt to the CIS fund, but said his debt collectors were continuing to recover more funds from the businessman.

He explained that Manji and other debtors who were yet to settle their debts after the expiry of the set deadline would be given a grace period to pay up if they demonstrate a willingness to do so.

However, he revealed that debtors who fail to settle their debts would be named and shamed publicly and ultimately dragged to court.

It is understood that some of the company owners on the list had disputed the debts and were reluctant to settle their long overdue debts.

Msolopa said some company owners simply disowned the debts, while others claimed they did not recall the money owed.

A number of businessmen demanded clarifications from debt collectors as to when they actually went to take loans from the CIS funds, and ultimately agreed to pay the debts after being shown documentary evidence.

’’Other debtors have been trying to disown the debts, claiming that they have inherited the debts from former shareholders of their companies thus showing some difficulties in accepting the liability,’’ he said.

He insisted that all individuals who fail to settle their debts would be publicly named.

’’We will publicize the names of the defaulters then discuss with the Ministry of Finance and Economic Affairs further steps to be taken, including legal action,’’ he added.

He explained that officials from his debt collection agency were making visits to companies that have failed to settle their debts so far to discuss the way forward.

After a much-publicised crackdown on corruption at the Bank of Tanzania (BoT), the government has appeared ready to shift its focus onto the long-standing import support scheme scandal, where around 16.6 billion Japanese yen (approx. 180bn/-) mysteriously disappeared.

Official records from the Ministry of Finance indicate that a total of 916 companies countrywide are on the debtors’ list.

It has been confirmed that several companies on this list are owned by Manji, who appears to have already started to pay his debts.

Well-placed sources have told THISDAY that the Prevention and Combating of Corruption Bureau (PCCB), the office of the Director of Criminal Investigations (DCI), and other law enforcement agencies have long been trailing the import support scam.

In particular, the PCCB investigation on the CIS scandal was reported to have reached an advanced stage, but it remains uncertain if the government’s corruption watchdog plans to pursue criminal proceedings against some well-known suspects.

Insiders say apart from Manji, the names of various well-known businessmen and politicians - both past and present - are among those featured on the list of debtors.

Under the CIS scheme, beneficiaries were supposed to provide 30 per cent of the requested funds known as ’cash cover.’

It is understood that some of the listed debtors were basically duped by a notorious businessman into borrowing CIS funds they thought they would never have to repay.

The scheme was initially administered by the Ministry of Finance, but from September 2002 it was moved to the Tanzania Investment Bank (TIB), ostensibly for better management of the funds.
Tanzania Daima said:
Slaa aponda ukusanyaji madeni CIS


na Sauli Giliard


KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amesema kitendo cha serikali kuteua kampuni ya Msolopa Investment Ltd kukusanya madeni ya Commodity Import Support (CIS) ni cha ‘kisanii’.

Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu jana, Dk. Slaa alisema utaratibu huo kamwe hautaweza kubaini ufisadi, kwani zaidi ya sh bilioni 800 zimefujwa na makampuni hewa.
“Nilipozungumzia suala hili kwa mara ya kwanza, serikali, watu na vyombo vya habari havikunielewa….sikumaanisha madeni ya CIS...nilikuwa namaanisha ufisadi ambao ndio uliosababisha upotevu wa fedha nyingi,” alisema Katibu huyo.

Alisema kutokana na matatizo ya kifedha Tanzania iliyokuwa nayo, ilitoa vibali maalumu kwa ajili ya kuagiza vifaa kutoka Japan, mwanya uliotumiwa vilivyo kuanzishwa kwa makampuni hewa na kuchota fedha za serikali.

Dk. Slaa, alisema baada ya serikali kutangaza kutoa vibali hivyo vya kuingiza bidhaa nchini, zaidi ya makampuni 980 yalinufaika na fedha za serikali.

Bila kutaja jina, kwa madai ya kufanya hivyo muda utakapofika, Slaa alisema kuna kampuni moja iliyosajiliwa ambayo uchunguzi wa haraka unaonyesha kuwa ilikuwa na makampuni hewa 35.
Kutokana na hali hiyo, Dk. Slaa ambaye pia ni Mbunge wa Karatu alisema ni vigumu kubaini vitendo vya kifisadi vilivyofanywa na kampuni zilizonufaika na mfuko huo, kwani nyingi ni hewa na hazina nyaraka zinazoonyesha kunufaika moja kwa moja.

Dk. Slaa, alisema vigogo wengi wanahusika na ufisadi huo, kwani waliuza hati zao kwa matajiri.

“Kuna ufisadi mkubwa hapa, bila uchunguzi wa kina si rahisi kuwabaini…mengi ya makampuni ni hewa,” alisisitiza.
Kutokana na hali hiyo, Dk. Slaa alisisitiza kufanyika uchunguzi wa kina kubaini makampuni hayo, kwani njia inayotumika sasa kamwe haiwezi kubaini aliyehusika na ufisadi huo.

Kauli ya Slaa imekuja siku moja baada ya kampuni iliyoshinda kandarasi ya kukusanya madeni ya CIS kutoa muda wa siku saba kwa makampuni yaliyohusika kueleza namna ya kurejesha kiasi cha zaidi ya sh bilioni 190.
 
Back
Top Bottom