Emma.
JF-Expert Member
- Jun 25, 2012
- 19,935
- 5,559
Heshima kwenu wana JF,
Viongozi wa vyama vinavyounda Umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA)wakiongozana na mbunge wa ACT Zitto kabwe wameeleza kamwe hawataacha serikali iendelee kuwanyima wananchi haki ya kikatiba kwa kuwazuia kutoa na kupata habari.
Viongozi hao wa UKAWA waliwaonyooshea vidole wabunge wa CCM kwamba ni wanafiki, kwa sababu wao (wapinzani )wakijadiliana na kamati ya Uongozi wa Bunge, walikuwa wakipokea vimemo wakiomba waendelea kupambana kwa sababu hata wao hawapendi yanaendelea kufanywa.
Akizungumza kwa niaba ya viongozi wenzake wa UKAWA Mwenyekiti mwenza wa UKAWA, Freeman Mbowe alisema wanalaani udhalilishwaji waliofanyiwa wabunge wa upinzani bungeni, kwa kutumia askari wenye silaha mbalimbali na mbwa, kwamba ni ukiukwaji wa haki za bunge.
Amesema sababu zilitolewa serikali kuzuia TBC kurusha moja kwa moja matukio ya bungeni hazina mashiko na kwamba wamebaini mambo matano yanayoipa serikali kiwewe mpaka kufikia hatua hiyo.
Hata hivyo Mbowe amesema hawajasusia vikao vya bunge, leo wataendelea kushiriki shughuli za bunge kama kawaida lakini wakiendelea kudai haki za kikanuni na kikatiba kuzingatiwa, kwa maslahi ya watanzania wote.
Mambo matano yanayoipa serikali kiwewe ni kuhusu hali ya kisiasa Zanzibar,kasoro zilizojitokeza kwenye uchaguzi uliyomalizika 2015,maamuzi yanayochukuliwa na baadhi ya viongozi wa serikali awamu ya tano, bila kufuata kanuni mbalimbali kwa kisingizio cha kutumbua majibu. Na swala la katiba mpya.
Naye Mwenyekiti mwenza wa UKAWA James Mbatia amesema wabunge wengi kwa sasa wanafanya siasa za kizazi kipya, hawatokubali kurudishwa kwenye enzi za 'zidumu fikra za Mwenyekiti ' Mbatia amesema "Tuko tayari kuuawa sote lakini ifahamike hilo likitokea, wengine wataendelea kujitokeza kuendeleza madai mpaka haki itapopatikana "