Msichana achaniwa nguo hadharani

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
MSICHANA anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 20 hadi 22 ambaye hakufahamika jina lake mara moja amekumbwa na kadhia ya kuchaniwa nguo yake baada ya wanaume kuchoshwa na mavazi yake ya nusu uchi ambayo yanaenda kinyume na maadili ya mtanzania.
Msichana huyo amechaniwa nguo hiyo jana majira ya saa 11 jioni baada ya kukatiza mbele madereva wa usafiri wa pikipiki ‘bodaboda’ huko maeneo ya JetLumo jijini Dar es Salaam
Msichana huyo alikuwa ametinga kivazi cha nusu uchi kaptula ‘mini’ ambayo tena haikuwa na maadili ni fupi kupitiliza ambayo ilikuwa ni mithili ya kutovaa kitu katika maungo yake

Hivyo msichana huyo imedaiwa alichosha watu wanaomzunguka eneo hilo kutokana na mavazi yake yasiyo na maadili na hivyo kupelekea wanaume kujitolea kumshikisha adabu kwa kumchania nguo hiyo ili aweze kutembea uchi bila nguo ya chini

Msichana huyo alifika katika kituo hicho kwa lengo la kupata usafiri wa pikipiki apelekwe mahali ambapo alikuwa akihitaji apelekwe

Hata hivyo mteja huyo hakufurahiwa na wengi kutokana na maadili yake na hivyo kutokea madereva wawili ambao walijitolea muhanga na walimtatulia nguo yake ya chini aina ya kaptula ambayo aliyokuwa amevaa

Hivyo kutokana na hilo hakuna raia yeyote ambaye aliweza kumtetea kuhusiana na hilo na kujikuta akipata aibu ya mwaka na kuangua kilio cha aibu na kuomba asitiriwe katika moja ya saluni iliyokuwa karibu na hapo

Hadi NIFAHAMISHE inaondojka eneno hilo ilicha msichana huyo akiwa ndani ya Saloon hiyo ya kike na kuhofia kutoka kwa aibu aliyoipata
 
Back
Top Bottom