Msiba wa Wananafunzi: Clouds group kusimamisha vipindi vyake vya TV na redio ili kuomboleza

Uzalendo wa kweli. Angalau mtatufariji kwa kuona mubashara kinachoendelea kwenye msiba. Ruge hana hela nyingi kama IPP,Azam, lakini yeye na wenzake wameguswa.
 
Taarifa imetokea Clouds Media makao makuu Dar es salaam ambapo vyombo vyake vya CloudsFM, ChoiceFM, CloudsTV havitorusha vipindi vyake kama ilivyozoeleka kila siku.

Sababu kubwa za kufanya hivyo kuanzia leo Jumapili mpaka Jumanne usiku ni kuungana na Watanzania kuomboleza vifo vya watu 32 wakiwemo Wanafunzi 29 ambao wamepoteza maisha kwenye ajali ya Basi dogo la Shule Karatu Arusha.

Screen-Shot-2017-05-07-at-1.55.48-PM.png
Pamoja na majonzi bado watz wanahitaji kujua ulimwenguni kunaendelea nini.Nimepita kwenye mabaa kuna watz wanapata kinywaji tu hawajali hata kuna msiba.Zipo sherehe na vikao vya harusi.Majonzi siyo kwenye vyombo vya habari tu.
 
daladala zilizochoka ndio zinageuzwa school bus

Mbona tuna Viongozi pia waliochoka nchini lakini bado ndiyo hao hao wanatuongoza na tunaenda nao hivyo hivyo ' mdogo mdogo / hado hado ' Mkuu na wala huwalalamikii?
 
Pamoja na majonzi bado watz wanahitaji kujua ulimwenguni kunaendelea nini.Nimepita kwenye mabaa kuna watz wanapata kinywaji tu hawajali hata kuna msiba.Zipo sherehe na vikao vya harusi.Majonzi siyo kwenye vyombo vya habari tu.
Uko sahihi mkuu.....ndio tunamsiba mkubwa japo sio msiba wa kitaifa....Lakini haimaanishi kila kitu kisimame eti sababu ya maombolezo.

Lakini kwa sababu ni kituo binafsi hatuwezi kuwapangia cha kufanya....
 
Hawa Jamaa Wamegeuza Msiba Huu Sehemu Ya Promo, Najua Mmeumia Kama Sisi Na Ni Vizuri Mkapunguza Matangazo Yenu Kuhusu Msiba Huu, Mnaweza Fikiri Kuwa Mnawafariji Lakini Mnawaumiza Wafiwa, Wanahitaji Kusahau Ili Maisha Yasonge Mbele, Nyie Mngejikita Zaidi Kutoa Elimu Ili Yasitokee Tena, Hizi Promo Mnazopiga Hazisaidii Sasa Hivi.
 
Back
Top Bottom