Mkuu mambo mengine ukiyasikiliza utashikwa na butwaa,anacho sahau ni kwamba hilo ni shirika la UMMA sio mali au kampuni ya ukoo na mnacho kihita eti faida notwithstanding,Watanzania tunapumbazwa na uyoga wa majengo ya gharama lukuki not knowing kwamba yote hayo yamejengwa kwa mkopo kwa masharti ya kutia shaka - kuna mtu mweledi aliwahi kuonya kuhusu ukurupukaji wa uwekezaji holela lakini ni watu wachache walio muelewa.
Binafsi nachukulia miradi hii ya NHC ambayo haina breki kama ni a ticking time bomb inayo subili kulipuka as time goes by,tatizo la Watanzania tulio wengi tunaongozwa na mob saikologe wakisha msifia mtu basi hakuna mwenye ubavu wa kuhoji uwekezaji unao fanywa na shirika hili ambao mwingine umekaa ndio sivyo, tunawapa Wakuu wa mashirika a blank cheque wafanye wapendalo bila ya kuhojiwa,
hakuna cha check and balance wala nini sijui!!!
Kwa nini mtu usijiulize hivi inakuwaje Mkuu wa shirika anakuwa Judge,Jurry na excutioner all rolled in ONE
HAMY-D;
Mbona mna kawaida ya kuanza na dagaa mnaacha papa? Tueleze uhalali wa weye mbunge kupata nyongeza hiyo si kutafuta wenzio wanakula ngapi.
Kazi anayoifanya Mchechu unailinganisha na "Ndiyooo" tunayoisikia bungeni? Mbona unaogopa kuanza na yule wa TANAPA? Unaogopa kupotea au?
Usihalalishe uchafu wako kwa kuonesha wengine
taahira oneHata angelipwa bilioni 56 zinakuhusu nini?acheni tabia za umbea na majungu .
ndo tatizo la kuwa na wabunge af wanatumia fake accounts humu. mtu kuhoji milion 130 au milion36 kama mshahara ni umbea? mnadhani hii kauli mtu maskini anaweza kutamka? haiwaumI kwasababu we unaecomment inawezekana ni mbunge au ndugu yako mbunge! muwafkirie na walala hoi jamani
To me kazi za mbunge sioni kama zina tija yoyote, ukiwa mbunge wa mikoa kama Dodoma, Singida, Tabora na mikoa mingi ya pwani (ukitoa Dar but including Morogoro) na ukawa unapendwa na chama chako hasa ccm, huhitaji kutumia akili yoyote kwenye kazi yako ya ubunge na still utaendelea kua mbunge; wabunge hawazalishi faida yoyote kwa taifa but wakurugenzi wa mashirika ya umma wazalisha faida (monetary) na ndio hizo pesa wanazo zalisha nyingine wanakula wabunge. Hebu niambie kwamfano nchi ikiwa na wabunge 50 tu, tutapata hasara gani? Na jiulize kwa mfano tusipokua na ceo wa shirika lolote la serikali tutapata faida au hasara? Kazi za siasa nchi hi zimepewa kipaumbele sana kuliko za kitaalamu, ningependa sasa kupitia kubana matumizi kulikofanywa na mhe Pombe kuwanufaishe madaktari, manesi, walimu, askari wote wa majeshi yote hasa magereza (kwa utafiti wangu nadhani hawa ndio wanaishi maisha magumu zaidi kuliko askari wengine) na hao ma ceo waendlee kujilipa kadiri wanavyozalisha. Kabla ya Nehemia Mchechu hajawa CEO wa NHC, shirika hilo lilikua halina vision wala mission but through him tumeona umuhimu wa shirika hilo, tumtie moyo zaidi badala ya kumkatisha tamaa. Ungenambia watu kama yule w TIC, SSRA ningekuelewa cause ukweli hayo mashirika sioni TIJA yake kwa taifa zaidi ya kuongezeana ulaji tu.
Kwani alijipangia mwenyewe au ndicho alichokubaliana nacho na waliomwajiri?
Faida anaileta personally au kama kampuni? Na ingekua kulipwa ni directly proportion watafiti wangepewa kiasi gani? Think big banaa
Hivi kazi anayofanya Rished Bade pale TRA utataka kumlipa million 3?? Kazi anayofanya Massawe pale TPA utataka kumlipa Million 3?? MD wa NSSF au PPF au TANAPA utataka kuwalipa mishahara ya hivyo?? Mkuu Msechu anafanya miradi mpaka ya mpaka 100 Billion, ukitaka kumlipa kimshahara cha million 3 si unataka kumwingiza kwenye matatizo tu?? Rished Bade anakusanya 800 Billion a month, ukitaka kumlipa Million 3 si unataka kumsababishia matatizo tu?? Hivi hawa wabunge wetu wengi wanafanya nini cha maana zaidi ya kugonga meza na kupitisha sheria zenye loopholes kibao kule bungeni??
Hoja yako ni ya kijinga sana. Kwahiyo kwanini tunalalama kuhusu maslahi ya wabunge...kwani wabunge wamejipangia wenyewe!? Si ni makubaliano yao wenyewe huko Bungeni? Sasa hizi kelele huku mtaani za nini?
Mimi nimepata tu wasiwasi kuwa
HIYO MISHAHARA NA MAPOSHO ndio inafanya nyumba ya vyumba viwili ya bei rahisi iuzwe Milioni 48????
Hivi kazi anayofanya Rished Bade pale TRA utataka kumlipa million 3?? Kazi anayofanya Massawe pale TPA utataka kumlipa Million 3?? MD wa NSSF au PPF au TANAPA utataka kuwalipa mishahara ya hivyo?? Mkuu Msechu anafanya miradi mpaka ya mpaka 100 Billion, ukitaka kumlipa kimshahara cha million 3 si unataka kumwingiza kwenye matatizo tu?? Rished Bade anakusanya 800 Billion a month, ukitaka kumlipa Million 3 si unataka kumsababishia matatizo tu?? Hivi hawa wabunge wetu wengi wanafanya nini cha maana zaidi ya kugonga meza na kupitisha sheria zenye loopholes kibao kule bungeni??
Mkuu hupo sahihi kabisa ni watu wachache watakao kuelewa,ukiangalia vizuri na mimi nilitoa angalizo hilo mapema - chukulia mfano wa mashariti ya mikopo ya Benki na ujenzi wa Project ya pale Morocco,unajua nini kitatokea baada ya miaka kupita? Benki itanyanganya NHC jengo pamoja na aridhi!!! Kuna mikataba mengine ya ajabu kweli kweli.Endelea kumsifia lakini hujui kuwa shirika lina madeni makubwa sana na yeye mkataba wake utaisha na shirika ataliacha katika hali ya kukabwa na mabenki.
Sioni cha maana alichofanya Mchechu NHC zaidi ya kuliingiza shirika kwenye madeni tu. Na mbaya zaidi miradi ina returns ndogo kulinganisha na zile ambazo zilikuwa anticipated...hii ni hatari sana kwa maana madeni yatashindwa kulipwa na shirika litafilisiwa na mabenki na hilo likifanyika itakula kwetu Watanzania maana sisi ndio wenye shirika.
Tsh. 36m haizidi $17k kwa mwezi, ni mshahara wa kawaida sana kwa Mkuu wa Shirika ambaye ufanisi wake haufichiki.
Kulipa wafanyakazi vizuri ni njia mojawapo ya kuzuia tamaa za wizi, sioni tatizo na Mshahara wa Tsh. 36m.