Mshahara wa Nehemia Mchechu wa NHC ni USD 19,000 kwa mwezi

Status
Not open for further replies.
Sasa wewe ndio unaleta porojo kama unajua alikokuwa Msechu alikuwa analipwa kiasi gani kama si zaidi ya hizo USd 11,000.00 na je kabla ya kuingia huko huyu ndugu unajua NHC walikuwa na nyumba ngapi na sasa wana nyumba ngapi tena nyumba za kisasa sio zile za kwenda km 2 hadi ukikute choo.Penye kusifiwa wacha tutoe sifa na penye kukosolewa wacha tukosoe lakini isiwe mtu unaleta tu pole za kusikia kama vile unasoma magazeti ya Shigongo

Sio porojo bali ni ukweli. Kwani alipotoka si alitoka mwenyewe! Hakuna aliyemshikia bunduki. Hakuna cha ziada alichofanya ila uvivu na uzembe wako unakufanya uone amefanya ya ziada. Jaribu kutembea uone bob. Watu wana-graduate chuo kikuu baada ya miaka miwili wanafanya projects kubwa kuliko huo uchafu wako
 
Hapo ndio naona wengi mnabugi stepu, hivi wakati NHC wanatafuta CEO walimtia wapi, si sekta binafsi? Sasa utapataje watu competent bila kuwalipa vizuri? Eti shirika la umma!!!! Kwani anajitolea? Huo mtindo wa kuwekaweka tu watu kwenye nafasi eti kwa kuwa ni shirika la umma si ndiyo ulukuwa unayaua? Yaani mfano Mataragio, Mkurugenzi mpya wa TPDC ukamlipe milioni moja na nusu eti kwa kuwa ni taasisi ya serikali?

Una ukakika kwenye sector ya umma wasingepata mtu competent? Nani kakuambia wote wa sector binafsi wapo competent? Hizo kasumba zinatumiwa kupachika watu wao.
 
Kwani na huyo wa UK nayeye si aliitoa benki kwenye red na kuanza kutengeneza faida...

Kikubwa kinachomsaidia Nehemia ni kwa sababu wizara ya ardhi inavyo onekana sio inayo set agenda au mission ya shirika vinginevyo angekuwa amewekewa strategy na anapimwa na matokeo awezi anaenda zake...

NHC wana strategy mkuu. Ipo wazi kwenye website yao. Ipitie. Nyumba 15000 ndani ya miaka mi5 mwisho mwakani.

Akishindwa, naam, achomolewe awekwe mwingine. Alipokubali alipaswa kujua ataulizwa mwishowe.
 
Barrick Gold Corporation Employer Salary, Average Salaries | PayScale

Mishahara ya Barrick Gold US hii hapa. Hydrogeologist hazidi 130,000 kwa mwaka! Mining Engineer USD 95000 kwa mwaka. Leo mnatuambia mtu wa HR wa kawaida bongo analipwa mshahara wa USD 216000 kwa mwaka! Labda pamoja na marupurupu lakini si mshahara mtupu.

Mwanyika ni Vice President wa a Global Mining Company kwa hiyo si ajabu kulipwa mshahara wa ajabu. Tusichanganye mambo.

Amandla........

Mi sijakwambia Barrick US.

Kwahiyo kwa Mwanyika sawa kwa Mchechu... Au mna ajenda nje ya anacholipwa?
 
Kuna thread hapa ilikuja jinsi gani yule mmbena mwenzake aliekuwa ikulu na sasa hayupo alivyosaidia kufanikisha usaili wake, usidhani JF tuna argue na hadithi za mtaani.

Siifahamu. Nitashukuru ukiweka link mkuu. Hata mi nimetumia thread hiihii huko mwanzoni kuhusu ye kuchukuliwa toka CBA.
 
Ngazi, lifti, maji n.k. nazo ni jukumu la mpangaji? Na tangu lini mpangaji ndie anaewajibika kupaka rangi ndani, kurekebisha vitasa, kutengeneza vyoo n.k.!

Amandla......

Amandla......

Utakua hujanielewa. Ulivyotaja ndo miundombinu ya jengo.

Ndio, mpangaji anawajibika kwenye hivyo kwakua ndie anaevitumia. Yani balbu iungue au mwanao achubue rangi umfate mwenye nyumba? Mkuu ushawahi kupanga?
 
NHC wana strategy mkuu. Ipo wazi kwenye website yao. Ipitie. Nyumba 15000 ndani ya miaka mi5 mwisho mwakani.

Akishindwa, naam, achomolewe awekwe mwingine. Alipokubali alipaswa kujua ataulizwa mwishowe.
True but it was structured by the existing management.

But what roles did the owners (serikari) play in all this kwa taarifa yako mwenye mali ndio anaetakiwa kujua malengo ya biashara yake. Ndio maana simlaumu sana kwa kulipoteza shirika mwelekeo kwa kuja strategy ambazo hazipo social friendly kabisa kama mashirika mengine ya nyumba yaanayo milikiwa na serikari yanavyofanya duniani.

Existing assets za NHC kwa kuboresha ukusanyaji wa mapato shirika lingeweza kukuwa organically na bado kukawa na fiada vilevile kama wizara ingekuwa ina panga strategy inayoendana na majukumu ya serikari kwa jamii.

Angalia kenya wanavyofanya na idadi ya nyumba wanazojenga, bei zao ukilinganisha na soko halafu uone kama kuna miracles zozote kutoka kwa huyo Nehemia labda hizi ndio habari za chura kwenye dimbwi anavyojiona mbabe mbele ya tadpoles. Akiingia baharini si chochote si lolote.
 
Am sure the owner played significant role. No wonder the president breaks soil & curtain raises many NHC projects.

Sijui sana taarifa za NHC Kenya. Kama wanafanya vizuri sana na wanauza nyumba za bei nafuu (although kuna mradi wao niliona wanauza nyumba over KES 350000. Labda wana categories) basi si vibaya tukajifunza kwao pia.
 
OKay kwa hapa tupo pamoja nimekuelewa sasa unacho advocate for (yaani kuwepo grade ambazo zomepangwa kabisa tena ikiwezekana kuwe na entry level, mid level na ile ya mwisho kabisa ambapo ukifika hapo no kuongezwa unless uwe ume-qualify for higher level position zaidi ya hiyo post)

Hapa kwenye kuiba tatizo mindset hazitaki kubadilika kutokana na uzoefu wa watumishi wa serikali tangu nchi imepata uhuru, ila thanks for observation maana wakati mwingine unatakiwa unapomwajiri mtu uwaze atafanya mazuri hata wakati wa kupanga mipango wote mnakuwa positive
Pakiwa na grades ndio ile inafanya watu wanalipwa sawa regardless ya ufanisi au aina ya kazi so long as ww ni CEO unalipwa kiasi fulani. Tutashindwa kuattract watu wazuri ksbu tuu hawatakua tayari kupokea malipo ktk grades fulani. Imagine benki inayomilikiwa na serikali inatafuta CEO na grades za serikali ziko below market utaishia kupata watu wasio wazuri au kupromote from within.
 
Una mfano kwa hapa Tz ili vijana wapate hamasa?

Soma tena nilichoandika. Nimesema anachofanya huyo jamaa yako sio kitu extra-ordinary bali kwa sababu Tanzania ni nchi ya wavivu na wezi ndio maana vi-project vichache anavyofanya vimeonekana kama miujiza. Nimeishi Ujerumani na nimeona magraduate wakifanya mambo makubwa kuliko haya mara kumi. Kwako mimi perfomance yake bado ipo below standard na siwezi kuzuzuliwa kama wewe unavyotaka. Na kwa taarifa yako mishahara ya hao niliowaona ni midogo zaidi kuliko huu unaotetea ni ''mdogo''
 
Am sure the owner played significant role. No wonder the president breaks soil & curtain raises many NHC projects.

Sijui sana taarifa za NHC Kenya. Kama wanafanya vizuri sana na wanauza nyumba za bei nafuu (although kuna mradi wao niliona wanauza nyumba over KES 350000. Labda wana categories) basi si vibaya tukajifunza kwao pia.
We uongozi wa JK bado ujaujua mpaka sasa kwa sababu nyumba zinajengwa na zinahitaji kufunguliwa yupo happy kukata utepe sio nyumba tu na miradi ya barabara.

Ngoja sasa siku kinuke bunge licharuke barabara hazina viwango au nyumba zina gharama wahusika watakiwe kuwajibishwa na bunge. Ndio siku atakayo kwambia mimi sio mtaalamu wa ujenzi nimeunda timu ya kuchuguza hivyo viwango vya barabara na gharama za nyumba au riba za mikopo wataalamu wanishauri huyo ndio JK chezeya Mr President wewe.

On a serious note Kenya wanamipango mizuri zaidi ya kuwasiadia watu kumiliki nyumba na wanajenga zaidi kuna umuhimu wa kujifunza kutoka kwao, just look at their strategy and compare.
 
Soma tena nilichoandika. Nimesema anachofanya huyo jamaa yako sio kitu extra-ordinary bali kwa sababu Tanzania ni nchi ya wavivu na wezi ndio maana vi-project vichache anavyofanya vimeonekana kama miujiza. Nimeishi Ujerumani na nimeona magraduate wakifanya mambo makubwa kuliko haya mara kumi. Kwako mimi perfomance yake bado ipo below standard na siwezi kuzuzuliwa kama wewe unavyotaka. Na kwa taarifa yako mishahara ya hao niliowaona ni midogo zaidi kuliko huu unaotetea ni ''mdogo''

Ujerumani? Wanalipwa chini ya Mchechu? CEO? Sihitaji ushahidi hapa.
 
ukiangalia website ya PPRA utaona kwenye tender za consultancy mashirika mengi yanafanya salaryreview and remuneration packages hii ina maana gani? TR amelala
Hii kitu karibu inafika kikomo kwa kuwa kutakuwa na Bodi ya Mishahara
 
...

On a serious note Kenya wanamipango mizuri zaidi ya kuwasiadia watu kumiliki nyumba na wanajenga zaidi kuna umuhimu wa kujifunza kutoka kwao, just look at their strategy and compare.

Kama wana mipango hiyo mizuri na wanaitekeleza, tuwaige tu. Ndo maendeleo. Hopefully NHC wanapita humu.
 
Mkuu wewe unapicha ya hili linalofanyika NHC lkn watz wengi wakiona tu majengo wanadhan ndo basi uwekezaji na kupata hela bila kuwaza zaid ya hapo. mpaka sasa most of NHC investments are simply reliability not assets
Nadhani mkuu hapo kwenye reliability nadhani ni Liability. Ukiangalia financial statements za NHC utagundua kwamba kuna shida kubwa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom