Mshahara wa mwalimu unavyotafunwa CWT

Song of Solomon

JF-Expert Member
Aug 5, 2021
2,733
5,490
Na Thadei Ole Mushi.

Walimu wa nchi hii asilimia 90 uliwaambia kwa nn Viongozi wa CWT huwa wanapigana wenyewe kwa wenyewe hawawezi kukuambia na wala hawajui chochote.

Nataka leo usijiulize tena kwa nini wanapigana na kupelekana mahakamani kila siku…. Twende sawa na ripoti hii ifuatayo:-

1. RIPOTI YA CAG

Tarehe 27/3/2017 Katibu mkuu kiongozi alimuomba CAG afanye ukaguzi kwenye chama cha Waalimu CWT.

Ukaguzi ulijikita katika tuhuma dhidi ya Uongozi wa chama cha waalimu zinazohisu ubadhirifu wa fedha na mali za chama.

Ukaguzi maalumu ulikagua taarifa za mapato na matumizi ya Chama, Uliangalia uhusiano uliopo kati ya Benki ya waalimu na waalimu wenyewe, uhusiano uliopo kati ya Mwalimu haouse na mwalimu mwenyewe.

YALIYOBAINIKA.

a) Hakuna mfumo mzuri wa wanachama unaoonyesha kumbukumbu za wanachama. Katiba ya CWT inaeleza kuwa kunatakiwa kuwe na aina nne za wanachama lakini CWT hawaonyeshi aina hizo za wanachama hivyo haijulikani CWT ina wanachama wangapi.

Pia katika suala la wanachama hakuna taarifa zinazoonyesha wanachama walijiunga lini, mishahara yao kwa mwezi, namba ya uanachama, kiwango anachochangia kwa mwezi nk. Jambo hili CAG anasema kuna uwezekano kuna fedha nyingi zinaliwa kutokana na kutokuwepo kwa taarifa hizo.

b) Malipo ya shilingi 11,924,250,620.13 yakifanyika bila viambatanisho vyovyote. Hii ina maana hakuna nyaraka zinazoonyesha matumizi sahihi ya fedha hizo.

C) Shilingi 3,287,708,358 zilipwa bila kuidhinishwa na katibu mkuu au mweka hazina wa Chama na pia hakuna viambatanisho.

d) Shilingi 11,924,250,620.13 zililipwa bila kuzingatia makisio. Hii ina maana fedha hizi zilitumika bila kuzingatia bajeti ya CWT.CAG anasema viongozi wanakosa nidhamu ya matumizi ya fedha hivyo kuna fedha hapa zilitumika bila wanachama kujua zimekwenda wapi.

e) Hakuna nyaraka zinazoonyesha umiliki wa moja kwa moja wa CWT na miradi yake.

f) Hakuna nyaraka zinazoonyesha mtiririko wa mapato wa vitega uchumi vya chama toka CWT kianzishwe.

g)Mwalimu House imesajiliwa Brela kwa jina lingine la Teachers Development kupitia usajili wa Brea 45719 Badala ya TDCL. Na CAG amebaini kuwa kampuni hilo la Teachers Development hakijawahi kufanya kazi toka kuanzishwa kwake. Kwa hiyo mapato yake hayaonekani.

2. SHEIRIA ZA NCHI ZINAVYOKIUKWA.

Imekuwa ni kawaida sasa kila mwalimu anayeajiriwa na ambao walikuwa wameajiriwa kuingizwa CWT kwa nguvu wakati Sheria za nchi zipo wazi. Aidha Sheria za nchi zinakataza vyama vya wafanyakazi visikate makato yake kwa kutumia Asilimia ni CWT pekee ambayo wanachama wake wanakatwa kwa kutumia asilimia… sheria zinasemaje?

~ Kuna sheria ya mwaka 1961,"The organisation of Tanzania Trade Union Act,1961,[Act no. 20/91],the trade Union(Revocation of special powers)

~Kuna sheria ya mwaka 1962 "Act,1962,The Trade Union ordiance Act,1962,"The Trade Unions and Trade Disputes (Miscellaneous Provision)Act,

~Sheria ya mwaka 1964 [Act No. 64/64] hadi hii ya sasa iliyofanyiwa marekebisho 2006 "The Trade Union Act,1998.

Katika sheria zote hizo hakuna mahali ambapo wamepewa mamlaka ya kukata mshahara mwa mfanyakazi kwa kutumia asilimia isipokuwa kwa sheria ya "Employment and Labour Relations Act,2004 part 4 ndiyo inayotoa maelekezo ya kitu gani kifanyike baada ya mwajiriwa kuridhia mbele ya mashahidi kuhusu makato husika [Sio kwa %] ya mshahara wake kwenda katika trade union husika.

3. MASWALI AMBAYO VIONGOZI HAWAWEZI KUYAJIBU.

Walimu Wana maswali mengi ambayo kwa muda Mrefu CWT hawataki kujibu na wala Watawala hawajawahi kufanya chochote. Baadhi ya maswali hayo ni haya:-.

i) Mapato yatokanayo na vitega uchumi vya chama mfano: Mwalimu house na ofisi za CWT kila mkoa (rent), je vinamnufaishaje mwalimu ambaye ni mchangiaji mkuu?

ii)Kwanini C.W.T wanakusanya michango kwa wanachama kila mwezi badala ya kukusanya mara moja kwa mwaka kama vyama vingine?

iii) Kwanini kuna tofauti katika makato ya kuchangia mfuko wa C.W.T wakati huduma ni sawa? Kuna nini kinachoongezeka kwa anayekatwa zaidi na nini kinachopungua kwa anayekatwa chini? Tofauti hizo zinaletwa na mfumo wa asilimia zilizowekwa na hivyo kuweka wachangiaji katika matabaka yasiyo na tija wakati huduma ni sawa.

Mfano mwalimu mwenye TGTS I yeye kwa Mwaka CWT huchukua 674,000 kwenye mshahara wake. Huyu anasaidiwaje zaidi tofauti na mwenye TGTS E ambaye hukatwa 225,000?. CWT wanakata Fedha nyingi Sana kwa Walimu na hakuna anayejali.

Malipo ya wanayopata ni T-shirt ambazo wamekuwa wakizilalamikia kila mwaka kutokana na kukosa ubora.

iv) Je kuna uhalali gani wa kiinua mgongo wa mwanachama anayestaafu kwa uwiano na alichochangia toka uanachama wake hadi kustaafu? Ikiwa kiinua mgongo kilichopangwa na C.W.T kwa sasa ni mabati ishirini (20) au laki tatu (300,000/=)

V) Je C.W.T kwa mwaka inakusanya kiasi cha shilingi ngapi kwa waalimu wote Tanzania kwa makato ya asilimia mbili (2%) ya kila mshahara wa mwanachama ambayo pia inatofautiana kulingana na madaraja.

Vi) C.W.T inawafanyakazi wangapi kwa kila mkoa na taifa kwa ujumla na posho zao zikoje?

Vii) Kwa kuwa waalimu wamekua wakinyanyasika na kudharaulika na kutosikilizwa katika halmashauri, Je C.W.T inafanya nini kurudisha hadhi ya mwalimu katika ngazi ya halmashauri ilihali mambo haya yanaendelea kumgandamiza na kumnyanyasa mwalimu?

4. NAMNA YA KUJITOA CWT

Ili makala hii isiwe ndefu sana kesho tarehe 18 nitafafanua namna na njia za kupitia kujitoa CWT. Ni haki yako kujitoa nitawapa mwongozo huo…,

Hakuna uhusiano wowote wa Kuongezwa mshahara na SERIKALI na CWT… SERIKALI haiwezi kumwongeza Daktari au nesi mshahara ikamwacha Mwalimu…..

Share na Mwalimu mwingine

Ole Mushi
0712702602

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Uelewa HURU

Cwt ni kichaka cha serikali (hasa chama Tawala)kuhujumu Maisha ya walimu kuwa Duni ili pale wanapowahitaji iwe rahisi kuwapata kwa kazi maalum za kitaifa kama sensa,uchaguzi,mitihani na n.k!

YAANI Maisha ya walimu yawe ya kuunga unga!

Ni kama Bodi ya mikopo hslb inavowafanya WATUMISHI ni ku spin Maisha yao ili yabaki kama yalivyo!

YUPO mtu atakuja atamaliza hata yote,maana maandamano sio utamaduni wetu!
 
Back
Top Bottom