Mshahara - Fedha za Nauli/Mafuta = kiasi gani kinabakia?

Ndo maana watumishi wa uma ni wezi kupindukia.

Hapo mnampigia hesabu yeye mwenyewe. Hujaweka:
~ misiba ya majirani na ndugu. Pengine atahitaji kusafiri pia.
~ anakaa na vishemeji/viwifi 2 vinasoma sekondari
~ ana mama mkwe ama baba mkwe wa kusupport
~jirani kajifungua, ana harusi ama kitchen party
~akifika hosp na kikadi chake cha bima ya afya wanamuambia xray haifanyi kazi akapigie regency alete majibu.

Ni utani mtupu aisee!
 
Hahaha na bora usiseme wazi lol.
Yaani ukiona ofisi ya umma parking haitoshi manake hadi masekretari wana magari. Nchi ya kitu kidogo hii.
..Mzee wangu ukilijua hili utpigwa na butwaa,mi mtumizi yangu ni makubwa kuliko mshahara ,thats the fact. ila ngoja wachambuzi wazuri waje kuainisha..
 
kwa habari hiyo mm ntaendelea kufanya kazi wilayani ambako hakuna daladala, ni miguu tu kwenda kazini
 
Hahaha na bora usiseme wazi lol.
Yaani ukiona ofisi ya umma parking haitoshi manake hadi masekretari wana magari. Nchi ya kitu kidogo hii.
...umeonaa eeeh..! ngoja tuanze jitihada za kuipeleka nchi yetu kwenye Guiness book maana kilakitu ni ajabu ajabu tu... mkuu watu8 tupe muongozo...
 
yani kwa mwendo bado kuna jitu na akili zake timamu huliaambii kuhusu magamba.. shiiiiit
 
Hahaha...mkuu ni kweli kuna mambo sio tu kuwa ni ya ajabu bali huwa yanasikitisha na kuwafanya wananchi wa kijiwe hiki cha Tanzania kuwa katika hali ya sintofahamu.
Na kweli inabidi tufanye mchakato wa kui-nominate nchi yetu kwenye matukio tata ya Guinness Book of World Records.

...umeonaa eeeh..! ngoja tuanze jitihada za kuipeleka nchi yetu kwenye Guiness book maana kilakitu ni ajabu ajabu tu... mkuu watu8 tupe muongozo...
 
Nauli ya mabasi imepanda Jijini Dar; najiuliza kwa wale wanaotumia usafiri wa umma na wanaoenda kazini JIjini wanatumia kiasi gani kwa siku (nauli, chakula) na wanabakia na kiasi gani mwisho wa mwezi? Na wale wanaojiendesha wenyewe wanatumia kiasi gani kwa mafuta kila siku tukuchukulie umbali wa kama kutoka Mbagala - Posta, Mikocheni Posta, Ubungo/Kimara Posta na Mwenge - Posta.

Na ziada inapatikana vipi?

Naombeni mfani wa hisabu...mtu anaweza kutumia kiasi gani kwa mwezi?

Mtu ambaye anatumia shilingi 1400 (kwenda na Kurudi), kwa siku tano mfululizo (Jumatatu hadi Ijumaa) kwa siku ishirini tu za mwezi (wiki nne) atakuwa ametumia shilingi 140,000 kwa nauli tu!

ongeza na billi za maji...umeme...king'amuzi...navingenevyo...
 
Jamani tunaomba wale wanaotumia magari yao kwenda kazini - watuambia wanatumia kiasi gani cha mafuta?????

Hii ni thread muhimu sana kwa kutoa picha ya mustakabali wa maisha yetu.
 
Tuwe wavumilivu kidogo jamani mambo yatanyooka muda si mrefu, mishahara ya sekta binafsi inapanda mwezi huu na ya uma ni Julai. Mtupe kamuda kidogo tushughulikie hili jambo.
 
Nauli ya mabasi imepanda Jijini Dar; najiuliza kwa wale wanaotumia usafiri wa umma na wanaoenda kazini JIjini wanatumia kiasi gani kwa siku (nauli, chakula) na wanabakia na kiasi gani mwisho wa mwezi? Na wale wanaojiendesha wenyewe wanatumia kiasi gani kwa mafuta kila siku tukuchukulie umbali wa kama kutoka Mbagala - Posta, Mikocheni Posta, Ubungo/Kimara Posta na Mwenge - Posta. Na ziada inapatikana vipi?
Ziada inapatikana kwenye rushwa. Kwa hali hii ni lazima kila mtumishi atoe na kupokea rushwa, tena hii inachochea na rushwa za ngono. Wanawake wengi bila kujalisha wameolewa au hawajaolewa watagawa kwa makonda ili nauli isiwe tatizo!Wanaume ndio watazidi kutafuta mijimama ya kuwalea.Watoto wetu .... uwiiiiiiiiiiiiiiiii Mungu tusaidie!Kwa kifupi, Tanzania yote matatani kila mmoja anatafuta pa kupatia unafuu! HALI NI MBAYA. TUMEKWISHA
 
Nauli ya mabasi imepanda Jijini Dar; najiuliza kwa wale wanaotumia usafiri wa umma na wanaoenda kazini JIjini wanatumia kiasi gani kwa siku (nauli, chakula) na wanabakia na kiasi gani mwisho wa mwezi? Na wale wanaojiendesha wenyewe wanatumia kiasi gani kwa mafuta kila siku tukuchukulie umbali wa kama kutoka Mbagala - Posta, Mikocheni Posta, Ubungo/Kimara Posta na Mwenge - Posta.

Na ziada inapatikana vipi?

Mimi ni mtumishi wa Serikali mshahara wangu net pay ni 421,256 naishi Mbezi mwisho natumia usafiri binafsi kila siku mafuta natumia wastani wa Tshs20,000, chakula cha mchana nikiwa mjini ofisini natumia Chai asubuhi wastani wa Tshs1500 na chakula mchana wastani wa Tshs2500. Naomba tusifanye calculations kuhusianisha na mshahara itakuwa ni uchochezi
 
Kausafiri Kangu kutoka maeneo ya Kimara kanatumia mafuta ya elfu ishirini kila uchao kufika mjini na kurudi home.

Kwa mshahara wa sh ngapi kwa mwezi hata kama umejiajiri mwenyewe unapiga dili gani au na wewe uko kwenye kundi la mafisimaji?
 
ni wazo tu na mtazamo wa 'king kinya' king.jpg
 
Mimi ni mtumishi wa Serikali mshahara wangu net pay ni 421,256 naishi Mbezi mwisho natumia usafiri binafsi kila siku mafuta natumia wastani wa Tshs20,000, chakula cha mchana nikiwa mjini ofisini natumia Chai asubuhi wastani wa Tshs1500 na chakula mchana wastani wa Tshs2500. Naomba tusifanye calculations kuhusianisha na mshahara itakuwa ni uchochezi

Chai tu kwa mwezi ni sh30000/=, mafuta kwenda ofisini ni sh 400,000/=, chakula cha mchan sh, 50,000/=
jumla ni sh 480,000 toa mshahara wako sh 421,256 hapo tu unadaiwa sh 58744,
bado hapo kila siku ukitoka kazini kuna mahali huwa unapitia kusubiri foleni ipungue ili uweze kurudi (wakwanza kuamka wa mwisho kulala) Mbezi sh............,
wakati m wingien huwa ukienda lunch nakuonaga ukiwalipia wafanyakazi wenzako hii huwa walau unaifanya mara mbili kwa wiki sh.................,
ijumaa ndio unaanza weekend ukitoka kazini unapitia pale......... unatumia sh.......... ukiwa na mama watoto msaidizi.
Hapo bado vocha za simu kwa siku shukuru mungu siku hizi laini moja ya tosha pengine sh 1000 kwa siku x 30= 30,000/=

weekend jumamosi ni siku ya marafikiri = mafuta 20,000/= vinywaji na chakula sh...........
Jumapili ni siku ya familia mafuta sh 20,000, vinywaji na chakula sh..............

wastani ma kununua nguo zako binafsi kwa mwezi sh............

huwa unafua dry-cleaner kwa mwezi sh..................

kila siku unaacha sh 20,000 nyumbani kwaajili ya matumizi kwa mwezi sh 600,000/=

Una watoto wanne wife mmoja, house girl wawili, gardener mmoja, mbwa wawili, small house mbili.

Lukukwa mwzi...............

maji kwa mwezi...............

Akiba kwa mwezi.............

Huwa unatuma hela nyumbani kwa wazazi wako na wazazi wa mke wako kila mwezi sh............

bado kuna watoto wa ndugu jamaa na marafiki huwa unawasaidi mara kwa mara katika ishu mbalimbali kama ada za shule unifomu, nk. sh..........

michango ya harusi, kipaimara, harambee mbalimbali, pamoja na sadaka.sh...........

matengenezo ya kagari chako ikiwamo service za kawaida kila mwezi sh..............

Dstv au kimauzi chochote kwa mwezi sh..............

Bado una bonge la nyumba huko mbezi unakoishi

Pengien bado unalia maishi ni magumu.

WAZIRI MKUU MWENYEWE PAMOJA NA KUWA NA UAHAKIKA WA KWETUMIA USAFIRI WA UMMA NA MAMBO MENGIE AKAUNTI YA INA SH.................???
 
Mtu ambaye anatumia shilingi 1400 (kwenda na Kurudi), kwa siku tano mfululizo (Jumatatu hadi Ijumaa) kwa siku ishirini tu za mwezi (wiki nne) atakuwa ametumia shilingi 140,000 kwa nauli tu!

hivi kwa Dar bado kuna wanaopanda ruti mbili mwendo mmoja na kurudi vivyo hivyo??
Ishu sio kiasigani anatumia kwa nauli je analipwa sh ngapi pengine mshahara watosha kwa gharama za maisha .

Tuwekee na viwango vya mishahara, kabla hatujaenda kwenye gharama nyingine
 
Back
Top Bottom