msaidieni jamani!

KITOSA

Member
Jan 22, 2011
38
4
kuna rafiki yangu alikuwa na mke hapo awali,ikatokea tafrani wakaachana jamaa akiwa kwenye msoto mkali,akaahidi hatooa tena!Mungu si athumani akatokea mdada akampenda akamuoa,sasa kivumbi yule mke wake wa awali amemuangukia na ametuma watu amrudie na hii ni baada ya miaka sita!afanyeje na ikiwa na wazazi wa huyo rafiki yangu wameridhia baada ya kufuatwa?anaomba ushauri!

Ye bado anampenda huyo mke wa awali?Alichofanya mwanzo kinarekebishika?Kama majibu ni hapana asonge mbele na huyo mpya kama anampenda kweli!Kama anahisi kumpenda wa mwanzo zaidi awe mwangalifu au ajiandae kujuta!Ila ungeongeza maelezo ingekua rahisi kumpa mawazo!

Miaka sita mingi sana mkuu na yeye kasha move on, kaoa mtu mwingine ambae wanapendana.

Sasa akikubali kurudi kule mwanzo na huyu wa sasa je?Uungwana uko wapi hapo? Kama yeye alichukia alichofanyiwa mwanzo kwanini afanyie huyu dada anayependana nae sasa hivi baada kutoswa na huyu anaomba msamaha sasa hivi?

Amwambie tu kwamba kamsamehe lakini yeye kapata mwingine ambaye wanaishi kwa amani na furaha.

Kulikua hamna ulazima wa kuchangia!Especially kama huna cha kusema zaidi ya kuonyesha dharau!

wewe waona dharau but hii thread ni marudio tu ya thread za aina hii nyingi mno..

na ushauri pia ni marudio....
inachosha

wewe waona dharau but hii thread ni marudio tu ya thread za aina hii nyingi mno..

na ushauri pia ni marudio....
inachosha

kama imekuchosa ungesoma then usichangie,hujalazimishwa kuweka vidole na kutuliza akili halafu unaandika pumba!thanks lizzy mawazo mazuri sana

Asimrudie kama yule ndio alikuwa mgomvi ila kama yeye alikuwa mgomvi ndio wakaachana amrudie cause ukiangalia vitabu vya dini hasa bible mke wako anaehesabiwa mbinguni ni yule wakwanza mmoja tu ambae umeapa nae kanisani. Duh hii inatupa wadada angalizo kuolewa na mtu aliyeachana na mwenzake inaweza kukuletea sooo

kuna rafiki yangu alikuwa na mke hapo awali,ikatokea tafrani wakaachana jamaa akiwa kwenye msoto mkali,akaahidi hatooa tena!Mungu si athumani akatokea mdada akampenda akamuoa,sasa kivumbi yule mke wake wa awali amemuangukia na ametuma watu amrudie na hii ni baada ya miaka sita!afanyeje na ikiwa na wazazi wa huyo rafiki yangu wameridhia baada ya kufuatwa?anaomba ushauri!

Kwa nini asiombe ushauri mwenyewe hadi akutume wewe? Are you his messenger?

Unaanza safari unataka kurudi nyuma?? Hana msimamo huyo rafiki yako miaka sita mchezo?? Mwambie aache utoto kashakuwa huyo asonge mbele na asimuumize huyo mkewe wa sasa.

Kama alitendwa lipi linamfanya arudi nyuma? vipi huyu innocent wa sasa, huyu aliekubali na kumvmilia maana lazima kakutana na mengi, hasa yakiwa ni mwangwi wa alietangulia.
Tuwe na huruma jamani, ina maana huyu wa pili hana haki.
Kama jamaa asipoonyesha msimamo siku akitendwa tena atarudi kwa hyu wa pili?

Kama alitendwa lipi linamfanya arudi nyuma? vipi huyu innocent wa sasa,
Kama anampenda sana huyo wa mwanzo pamoja na kumtenda hatakua anamtendea haki wa sasa hivi kubaki nae wakati moyo wake uko kwingine!Bora amuache ili anae apate atakaempenda kikamilifu!Akijilazimisha kubaki nae ipo siku tu atamuacha kwenye mataa iwapo muda hautamfundisha kumpenda mdada wa watu!

Jamani muwe na huruma,huyu dada wa watu aliyeolewa baada ya kuachana na mkewe ye aende wapi? kama walishaachana basi,mwenzie ndo kapata mwenza mwingine wanaishi.....lazima tukubali kuna makosa mengine,yanasameheka lakini hatupaswi kurudi nyuma!!!!:coffee:
Halafu wazazi wengine sijui vipi,we mwanao anaachana na mwanamke,anaoa mwingine,after six years anarudi then wazazi wanajua mtoto wao ana ndoa wanaridhia mke wa kwanza kurudi,kawafanya baya gani mtoto wa mwenzao? anyway,story haina mapana mengi ila nahisi kuna uwezekano mkubwa wa kumuumiza mtu asiyestahili!!!

Hebu tujiulize, wakati mwingine tunatoa ushauri bila kupata fact za mahusiano ya watu. Ni nini kilichofanya waachane? Je hicho kilichofanya waachane kimetatuliwa? then tunaweza kuwa na wakati mzuri wa kushauri kwa sasa ni kama tunapiga ngumi kimvuli vile.

Jamani muwe na huruma,huyu dada wa watu aliyeolewa baada ya kuachana na mkewe ye aende wapi? kama walishaachana basi,mwenzie ndo kapata mwenza mwingine wanaishi.....lazima tukubali kuna makosa mengine,yanasameheka lakini hatupaswi kurudi nyuma!!!!:coffee:
Halafu wazazi wengine sijui vipi,we mwanao anaachana na mwanamke,anaoa mwingine,after six years anarudi then wazazi wanajua mtoto wao ana ndoa wanaridhia mke wa kwanza kurudi,kawafanya baya gani mtoto wa mwenzao? anyway,story haina mapana mengi ila nahisi kuna uwezekano mkubwa wa kumuumiza mtu asiyestahili!!!

Michelle kweli kabisa nakuunga mkono. Miaka sita ni mingi sana, kila mtu kesha chakachua kivyake mpaka basi.

Asimrudie kama yule ndio alikuwa mgomvi ila kama yeye alikuwa mgomvi ndio wakaachana amrudie cause ukiangalia vitabu vya dini hasa bible mke wako anaehesabiwa mbinguni ni yule wakwanza mmoja tu ambae umeapa nae kanisani. Duh hii inatupa wadada angalizo kuolewa na mtu aliyeachana na mwenzake inaweza kukuletea sooo

umeona eeh.....wengi wetu tunajidanganya kuwa jamaa kaachana na mke wake hampendi kabisa ananipenda mimi....nyooooo......tushtuke hapo

Asirudiane na huyo mkewe wa zamani, huenda akarudia tena tabia yake ya zamani iliyosababisha wakaachana!

thanks a lot kwa wote mlionipa ushauri mzuri na pia wote mlioponda pia nawashukuru coz wote hatufanani kwa uelewa na hat kuwasilisha hoja ambayo mwenzio ameona amekwama na ameomba msaada.thakns JF its a good place!!

Inabidi kuheshim na kuangalia flngs za mtu, kama walisha achana kwa kipindi chote hicho, najamaa kaoa mke mwingine then amuache amrudie wa zamani, hebu jiweke kwa nafasi ya huyu mpya utajiskiaje? Kwani huyu mke mpya hana moyo wa nyama jamani? Pia jamaa asitegemee akimrudisha kuna furaha atapata no. Asicheze na maisha yake kuliko na yeye amuumize mke wake huyu alienae, bora asimrudie wa zamani. Istoshe wazamani keshazoea maisha yake aendelee tu kuliko kumfanya huyu mpya aanze upya watamuumiza. Kama alikiona cha nini, anakitaka cha nini.

Back
Top Bottom