Msafara wa Meli za Kivita za Iran wakamilisha kwa mafanikio safari ya kuzunguka dunia yote

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
9,000
17,909
Msafara wa 86 wa Meli za Kivita za Jeshi la Wanamaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran umerejea nchini baada ya safari ya kuzunguka dunia kama sehemu ya juhudi za Jamhuri ya Kiislamu za kupanua uwepo wake kijeshi katika bahari za mbali.

Msafara huo wa Jeshi la Wanamaji la Iran, ulijumuisha meli ya kivita ya Dena iliyotengenezwa nchini ambayo ina uwezo mkubwa wa kuharibu manowari za adui na hali kadhlika meli ya kivita ya Makran inayosheheni zana za kivita na vifaa vingine muhimu vinavyotumika katika oparesheni za kijeshi majini.

Msafara huo uliingia katika maji ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran siku ya Jumatano, baada ya kusafiri masafa ya kilomita 63,000 baharini katika muda wa miezi minane na kuzunguka dunia kwa nyuzi 360.

Msafara wa 86 wa Manowari za Jeshi la Wanamaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ambao ulianza safari ya kuzunguka dunia katika jiji la bandari la kusini mwa Iran wa Bandar Abbas mnamo Septemba 20, 2022, ulisimama kwa mara ya kwanza kwenye bandari ya Mumbai, India, na kisha kutia nanga Jakarta, mji mkuu wa Indonesia baada ya kupita katika Ghuba ya Bengal na Mlango-Bahari wa Malaka.

Msafara huo uliendelea na njia yake kuelekea Bahari ya Java na kupita kwenye Mlango-Bahari wa Makassar na Bahari ya Celebes, na kufika katika bahari kubwa ya Pasifiki kwa mara ya kwanza katika historia ya Jeshi la Wanamaji la Iran.

Baada ya kuvuka upana mkubwa zaidi wa Bahari ya Pasifiki na kupita visiwa vya Micronesia na Polynesia, msafara huo ulisonga mbele na kuelekea Mlango-Bahari wa Magellan kusini mwa Amerika na kuingia Bahari ya Atlantiki ya Kusini.

Manowari wa Makran ya Jeshi la Wanamaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambayo imeundwa kikamilifu na wataalamu Wairani

Msafara wa 86 wa Meli za Kivita za Jeshi la Wanamaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ulielekea kaskazini na kupita mwambao wa Chile, Argentina, Uruguay na Brazil, hatimaye kutia nanga katika bandari ya Rio de Janeiro nchini Brazil, ambayo iliambatana na kumbukumbu ya miaka 120 ya kuanzishwa kwa uhusiano kati ya Iran na Brazil.

Baada ya kusimama kwa siku chache huko Rio de Janeiro, wanamaji hao shupavu wa Iran walivuka Bahari ya Atlantiki na kutia nanga katika jiji la Cape Town, Afrika Kusini. Msafara huo kisha ulitia nanga katika bandari ya Salalah, Oman, na baada ya safari ya siku 40, uliingia katika maji ya Iran.

Manowari ya Dena ni ya kiwango cha Mowj na imeundwa kikamilifu na wataalamu wa Iran ambapo iijiunga na Jeshi la Wanamaji la Iran mnamo Juni 2021. Meli hiyo ya kivita ina makombora ya kukinga meli, torpedo au makombora ya chini ya maji na mizinga ya majini.

Nayo Makran ni manowari yenye kutangulia katika msafara na ina uzito wa tani 121,000. Meli hiyo ya kivita inaweza kubeba helikopta tano na ina jukumu la kutoa usaidizi wa vifaa kwa meli za kivita.

4c3lef352bf0b02ah41_800C450.jpg
 
Da!!! kila mbabe wa kijeshi sasahiv anakuja na mbinu zake... wengine wakiwa wanahangaika na anga za mbali... Iran kwao imekuwa tofauti, wanazunguka kwenye maji....
 
Msafara wa Meli za Kivita za Iran wakamilisha kwa mafanikio safari ya kuzunguka dunia

May 18, 2023 07:05 UTC

[https://media]

Msafara wa 86 wa Meli za Kivita za Jeshi la Wanamaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran umerejea nchini baada ya safari ya kuzunguka dunia kama sehemu ya juhudi za Jamhuri ya Kiislamu za kupanua uwepo wake kijeshi katika bahari za mbali.

Msafara huo wa Jeshi la Wanamaji la Iran, ulijumuisha meli ya kivita ya Dena iliyotengenezwa nchini ambayo ina uwezo mkubwa wa kuharibu manowari za adui na hali kadhlika meli ya kivita ya Makran inayosheheni zana za kivita na vifaa vingine muhimu vinavyotumika katika oparesheni za kijeshi majini.

Msafara huo uliingia katika maji ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran siku ya Jumatano, baada ya kusafiri masafa ya kilomita 63,000 baharini katika muda wa miezi minane na kuzunguka dunia kwa nyuzi 360.

Msafara wa 86 wa Manowari za Jeshi la Wanamaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ambao ulianza safari ya kuzunguka dunia katika jiji la bandari la kusini mwa Iran wa Bandar Abbas mnamo Septemba 20, 2022, ulisimama kwa mara ya kwanza kwenye bandari ya Mumbai, India, na kisha kutia nanga Jakarta, mji mkuu wa Indonesia baada ya kupita katika Ghuba ya Bengal na Mlango-Bahari wa Malaka.

Msafara huo uliendelea na njia yake kuelekea Bahari ya Java na kupita kwenye Mlango-Bahari wa Makassar na Bahari ya Celebes, na kufika katika bahari kubwa ya Pasifiki kwa mara ya kwanza katika historia ya Jeshi la Wanamaji la Iran.

Baada ya kuvuka upana mkubwa zaidi wa Bahari ya Pasifiki na kupita visiwa vya Micronesia na Polynesia, msafara huo ulisonga mbele na kuelekea Mlango-Bahari wa Magellan kusini mwa Amerika na kuingia Bahari ya Atlantiki ya Kusini.

[https://media]Manowari wa Makran ya Jeshi la Wanamaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambayo imeundwa kikamilifu na wataalamu Wairani

Msafara wa 86 wa Meli za Kivita za Jeshi la Wanamaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ulielekea kaskazini na kupita mwambao wa Chile, Argentina, Uruguay na Brazil, hatimaye kutia nanga katika bandari ya Rio de Janeiro nchini Brazil, ambayo iliambatana na kumbukumbu ya miaka 120 ya kuanzishwa kwa uhusiano kati ya Iran na Brazil.

Baada ya kusimama kwa siku chache huko Rio de Janeiro, wanamaji hao shupavu wa Iran walivuka Bahari ya Atlantiki na kutia nanga katika jiji la Cape Town, Afrika Kusini. Msafara huo kisha ulitia nanga katika bandari ya Salalah, Oman, na baada ya safari ya siku 40, uliingia katika maji ya Iran.

Manowari ya Dena ni ya kiwango cha Mowj na imeundwa kikamilifu na wataalamu wa Iran ambapo iijiunga na Jeshi la Wanamaji la Iran mnamo Juni 2021. Meli hiyo ya kivita ina makombora ya kukinga meli, torpedo au makombora ya chini ya maji na mizinga ya majini.

Nayo Makran ni manowari yenye kutangulia katika msafara na ina uzito wa tani 121,000. Meli hiyo ya kivita inaweza kubeba helikopta tano na ina jukumu la kutoa usaidizi wa vifaa kwa meli za kivita.

View attachment 2628033View attachment 2628034View attachment 2628035
Amazing
 
Back
Top Bottom