Msaada wenu tafadhali kuhusu watoto wachanga

Mr Kind

Senior Member
Mar 4, 2017
178
308
Natanguliza shukrani zangu kwenu wana Jamvi.

Leo nakuja kwenu kuomba msaada wa uelewa juu ya mambo yafuatayo kuhusu watoto :-

1. Je, ni hali ya kawaida kwa mtoto wa miezi miwili kasoro kuzungusha zungusha shingo lake mara kwa mara au huashiria tatizo!? (anazungusha shingo toka upande mmoja kwenda mwingine kwa kasi akionyesha dalili za kulia)
2. Mtoto wa miezi miwili kasoro anaweza kujisaidia kinyesi chenye harufu na isiashirie tatizo lolote!?

3.Na kwa kawaida mtoto mchanga anatakiwa kunyolewa nywere zake alizozaliwa nazo baada ya muda gani!? Ikiwa ni chini ya muda huo, kuna madhara gani yatakayo mpata!?

Ni hayo tu, natumai hata kama si mtaalamu wa afya ya watoto, unaweza kuwa na uzoefu wa mambo mawili matatu kutokana na malezi. Nawasilisha tafadhali.
 
Kwanza hongera kwa kupata mtoto .Ni wa kwanza.?Analia sana?Kama huna uhakika mpeleke hospitali.
 
Namba moja na mbili muwahishe hospital haraka

Hiyo ya tatu mkuu kwa kweli me naonaga wakifikisha 40 ndio wananyolewa na wakiachwa nazo sjui wanapata tatizo gani

Nahisi njia sahihi ya wewe kupata jibu ni kumuacha mwanao na hizo nywele uone baadae yatakuaje!

Madame S
 
mtoto mdogo nikama malaika huonavingi kuliko sisi. Pili huwa watoto wadogo wanasumbuliwa sana na tatizo la mvurugiko tumboni ( tumbo kujaa gesi ) hii humsababishia maumivu pia hajakubwa kutoa har...Kali. nini chakufanya. mpe drip water na mafuta ya samaki yaweza msaidia. ila hali ikizidi muone Doctor.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hamna tatizo mkuu, kugeuza shingo ndio uzima wenyew, wangu nilimnyoa na miezi minne coz arusha kuna bard aisee na akawa hapendi kofia. Kinyes kuwa na haruf ni kawaida. Ila kama unahisi anaumia hiyo shingo mpeleke kwa dkt
 
No.1& 2 mpeleke hospitali...watoto.hawatabiriki na wapo sensitive

No 3 mara nyingi ni baada ya siku 40....... ingawa sie wengine huwanyoa hata baada ya mwaka au hata miezi 9 hatunaga formula
 
Back
Top Bottom