GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,571
- 108,922
Historia ya huyu kijana aliyezaliwa miaka takribani 36 iliyopita ni ndefu yenye milima na mabonde mengi mno.
Ni kijana aliyezaliwa ktk familia iliyokuwa ikijiweza kimaisha lakini baada tu ya muda fulani wazazi wake wakatengana hivyo kukaanza kupelekea huyu kijana kuhangaika na kutokujua ni wapi ashikilie.
Kijana kamaliza shule ya msingi hivyo hivyo kishida shida akafaulu kwani ana uwezo mkubwa pia darasani. Akafanikiwa kuingia sekondari ambapo na penyewe pia alisoma kishida mno na akamaliza kwa kufaulu daraja la pili.
Akajiunga na kidato cha tano hadi cha sita ambapo na penyewe pia akafanikiwa akamaliza na kufaulu kwa daraja la pili na kufanikiwa kujiunga na chuo kikuu.
Tambueni kuwa kipindi chote hiki huyu kijana alikuwa anaishi tu kwa msaada wa watu kwani ilipelekea hadi wazazi wake kila mmoja kumsusia na kila alipowafuata kwa msaada hao wazazi wake wawili walikuwa wanamkana japo kuwa wao ndiyo wazazi wake halisi.
Hali hii ilimpelekea huyu kijana aishi maisha ya taabu sana lakini akajitahidi kufanya vijikazi vya hapa na pale ili ajipatie ada ya chuo na kweli akafanikiwa na kusoma chuo kikuu na kufanikiwa kumaliza na shahada yake ya kwanza ya mawasiliano ya umma.
Alipomaliza tu chuo huyu kijana akapata kazi ktk taasisi moja hapa jijini ambapo alifanya kazi kwa miaka mitatu na hapo hapo wale wazazi wake wakajifanya kurudisha uhusiano na yeye na kijana wa watu akaona kuwa asilipe kisasi kwao.
Baada tu ya kufanya kazi katika hiyo taasisi kwa miaka yake hiyo mitatu bahati mbaya hiyo taasisi ikakumbwa na tatizo kubwa iliyopelekea wafanyakazi wake kusimamishwa ajira zao ambapo walilipwa mafao yao.
Kijana wa watu alipowaambia tu wazazi wake kuwa kazi hana tena wale wale wazazi waliojifanya kumpenda kipindi kile ana kazi wakampotezea tena na kijana kwakuwa alikuwa amejiwekea vijihela vyake akaamua kurudi masomoni na kusomea shahada ya pili ya Uzamiri ya mambo hayo hayo ya mawasiliano ya umma na sasa anamalizia tu kufanya utafiti na kuhitimu rasmi mwezi Oktoba / Novemba.
Kwa sasa kijana wa watu huyu anahangaika sana kutafuta vibarua bila ya mafanikio na akijaribu tena kwenda hata tu kuwasalimu wazazi wake na kuwaomba msaada kuwa wamsaidie tu hata na pesa za yeye kujikimu au kufungulia mradi ili aendeshee maisha yake wazazi wake wote wawili wanamtukana na kumfukuza na kijana amepanga na kodi yake imebaki mwezi kama mmoja tu kumalizika hivyo hajui hatima yake kimaisha.
M imi binafsi nimekuwa nikijitahidi sana kutoa ushirikiano wangu wa hali na mali kwake ila kinachonipelekea kuwasilisha hapa kwenu hali yake hii ni kwamba kijana wa watu sasa ameshakata tamaa ya maisha na anataka kunywa sumu na kujiua kwani anasema kuwa inawezekana wazazi wake hao walimzaa kibahati mbaya kwani hawana hata huruma na upendo nae.
Ni kijana anayejituma, mkarimu na mwenye kumcha sana Mungu na hicho nilichokiandika hapo ni sehemu tu ndogo ya maisha yake ya shida na taabu aliyopitia na hata hichi nilichokiandika hapa yeye hajui na hafahamu kwani siyo mtu wa kushinda au kutembelea humu JF.
Nimewasilisha hili jambo kwenu ili kwa yoyote msamaria mwema atakayeguswa na tatizo la huyu kijana basi atoe ushauri wake ili nami niweze kumshauri na kwa wale watakaotaka kumsaidia siyo kipesa kwani yeye anachokitaka tu ni kupata kazi ya uhakika ili aweze kuendesha maisha yake haya magumu hivyo kwa bosi yoyote au mwenye kampuni au mtu yoyote mwenye ofisi au taasisi au kampuni yake na inahitaji mtu wa kazi basi mni pm ili niwapeni namba yake na muweze kumsaidia.
Bahati nzuri hata kozi aliyosomea hiyo ya mawasiliano ya umma ( Mass Communication ) anaweza kufanya kazi ktk taasisi yoyote ile inayojihusisha na jamii/uhusiano na habari.
Naomba kuwasilisha kwenu na nawaombeni radhi kwa uzi huu mrefu ila imenibidi niuwasilishe kwenu ili tuweze kumsaidia.
Mbarikiwe