Msaada wa tatizo la korodani ya mtoto mchanga kupanda juu kuelekea tumboni

herio

JF-Expert Member
Jan 1, 2021
2,080
3,922
Wasalam JF,

Wakuu nina kichanga cha miezi mitatu,tangu akiwa na mwezi mmoja nimekuwa nikimwambia mama yake amchunguze vizuri hasa sehemu za siri.

Akawa ananiambia mtoto ana korodani moja sikuchukulia serious kwakuwa alikuwa mdogo nikasema labda bado hayajakua vizuri.

Leo hii nimemchunguza mimi mpaka eneo la juu kidogo...ni kweli sehemu zinapokaaga korodani ipo moja tu lakini ukiangalia kwa juu kidogo [kwa wakubwa ni ile sehemu yanapootaga mavuzi]nimekuta korodani ya pili imegota pale ukiangalia ni kama kuna uvimbe kumbe ndiyo korodani yenyewe wakuu nimejaribu kuisogeza chini ila ipo palepale.

Je hili ni tatizo au vipi?

Nifanye nini ili irudi sehemu yake?

Nimeona nipite kwanza humu nipate ushauri kabla ya kwenda kituo cha afya
Nawasilisha.
 
Ilishawahi tokea kwa mwanangu akiwa na umri wa miezi 7, ilikuwa usiku wa manane mtoto akaanza kulia kwa maumivu makali, bahati nzuri akili ikanituma kumkagua, nikakuta kweli pale korodani hazipo, nikakimbilia hospital kwanza akachomwa sindano ya kupunguza maumivu na mpaka wanataka kuanza kunshughulikia zilikuwa tayari zisharudi zenyewe.

Nikapewa appointment ya daktari wa watoto ili achunguzwe kama ni wa kufanyiwa operation au kama tatizo litaisha lenyewe kadili anavyokua.

Nilichokifanya sikurudi tena hospital ila nilimtuma kwa bibi yake akanywa dawa za kienyeji na tatizo halikujirudia tena mpaka sasa ana miaka 4.

Lakini nilishawahi kusikia inawatokea na watu wazima, wengine wanaita ngiri japo sijui kama wako sahihi.
Inasemekana ukimpaka MAFUTA YA TAA unazivuta na kuzirudisha kwa urahisi.

Lakini nakushauri uende hospita maana hapo korodani ilipo si mahali pake na inapelekea kupata joto kali kuliko ikiwa sehemu yake hivyo inaeza kupelekea matatizo makubwa.
 
Ipo sn,kuna kijana wangu wa wizi amefanyiwa operation leo.Nenda hospital achunguzwe nadhani utaambiwa subiri aongezeke ndo apate matibabu,though kama alivyosema mdau hapo dawa za asili zaweza tibu.
 
Ipo sn,kuna kijana wangu wa wizi amefanyiwa operation leo.Nenda hospital achunguzwe nadhani utaambiwa subiri aongezeke ndo apate matibabu,though kama alivyosema mdau hapo dawa za asili zaweza tibu.
Ukiuelewa na kufahamu zaidi kuhusu Cryptochidism na mfumo mzima wa uzazi hasa wa mwanaume huwezi zungumzia ishu ya dawa za asili ofcz siwezi kuwa na doubt kuhusu Hilo kwasababu sijaona lililotokea....

Changamoto ni Spermatic cord ambayo inahusika kupitisha mifumo mbalimbali tuifananishe Spermatic cord na Bomba la maji au kimfuko ambapo kazi yake ni kupitisha mifumo mbalimbali kama mishipa ya damu, mishipa ya fahamu (nerves ), mrija unaohusika kusafirisha mbegu na vinginevyo...

Changamoto hii inatokea endapo either kuchelewa au kuto kushuka kwa korodani ambazo hukaa juu kwenye tumbo, (Hii hutokea mtoto akiwa tumboni kwa mama yake, korodani zinakaa juu, anapokaribia kuzaliwa au anapozaliwa Tu zinashuka kutoka juu na kupita ndani ya Spermatic cord na kukaa sehemu husika au sehemu zinazostahili)

Wataalamu wa upasuaji huzishusha kutoka juu, na kupunguza ukubwa wa mrija (Spermatic cord) inayopitisha mifumo hii

Same hutokea kwa wanaopata inguinal hernia kwa wanaume..

Mpeleke mtoto akapate huduma na vipimo sahihi .... Na apate matibabu sahihi

Asante
 
Ubarikiwe🙏
 
Back
Top Bottom