Msaada wa kisheria

Kulugo Tise

New Member
Apr 12, 2011
2
0
Habari wanasheria,
Naweza kupata msaada wa 'utaratibu wa kisheria' unaotakiwa kufuatwa pindi mtu anapofanyiwa RETRENCHMENT au Redundancy kazini?

Aksanteni,
K. Tise.
 
inakubaliwa kisheria ila kama una madai au hukuridhika kabla siku thelathini hazijapita tangu upunguzwe ukafungue lalamiko dhidi ya mwajiri wako CMA yani baraza la usuluishi la kazi hatua nyigine zote utajua ukiwa huko kama upo dar lipo hapo idara ya kazi karibu na CBE arusha karibu na metropole etc
 
Kifungu na.38 cha Sheria ya kazi na mahusiano kazini 2004 inasema kwamba iwapo mwajiri anataka kufanya redundancy afanye yafuatayo:-

(a) kutoa notice ya nia ya kupunguza wafanyakazi;
(b) kuweka wazi information zote muhimu za jinsi ya kupunguza wafanyakazi na nia ya kufanya hivyo kwa ajili ya kupata mawazo kwa wafanyakazi;
(c) kutafuta maoni ya wafanyakazi kwa ajili ya yafuatayo-
(i) sababu za kufanya punguzo hilo;
(ii) njia zilizo na zitakazosaidia kutokupunguza wafanyakazi;
(iii) vigezo vitakavyotumika kuchagua wafanyakazi watakaopunguzwa;
(iv) muda zoezi litakapofanyika; na
(v) malipo kwa watakaopunguzwa,

(d) kutoa notice, kuweka wazi info za zoezi la kupuguza wafanyakazi, kwa-
(i) vyama vya wafanyakazi vinavyotambuliwa na kifungu na 67;
(ii) kwa vyama vya wafanyakazi vya ndani vilivyosajiliwa;
(iii) mwakilishi yeyote wa mwajiri na kwa ambaye hana mwakilishi basi kwa mtu yeyote anayetambulika naye au chama.

(2) Pale ambapo consultations zimefanyika na hakuna makubaliano kati ya mwajiri, waajiriwa na vyama vya wafanyakazi juu ya jinsi ya kupunguza wafanyakazi, basi suluhu yaweza patikana kwenye Tume ya Uamuzi na Usuluhishi (CMA).

(3) Pale ambapo, mfanyakazi amepunguzwa kazi kwasababu amekataa kukubali mabadiliko ya ajira, mwajiri anawajibika kudhibitishia mahakama ya kazi kwamba isingewezekana kampuni kuendeshwa bila mabadiliko hayo.
 
Nawashukuruni sana wote kwa michango yenu, Quinty aksante sana kwa kunipa huu utaratibu wa kisheria naaamini nitaendelea kukisoma hicho kifungu no. 38 zaidi na zaidi nikielewa na nione kitaweza kunisaidiaje.

Aksanteni wote.
Tise.
 
Back
Top Bottom