Msaada wa kisheria unahitajika

sijazaliwa

JF-Expert Member
Dec 11, 2014
207
141
Hivi ikatokea wachumba wamefunga NDOA bila kupima HIV. Baada ya miezi mitatu kupita mkaenada kupima na kugundua mmoja wenu ni HIV POSTIVE na mwingine ni HIV NEGATIVE.......je sheria inawaruhusu kuendelea kuishi pamoja au inasemaje?

....Msaada kwa Bi NYAU plz CONDA.........!
 
Ndoa ni muungano wa hiyari ,hapa tz hakuna Sheria inayolazimisha wanandoa kuishi kwa shuruti.Isipokuwa taasisi ya ndoa inaweza kuvunjwa pale tu Mahakama itakapothibitisha kuwa ndoa hiyo imeharibika kiasi kwamba haiwezi kurekebishika tena(broken down irreparable).

Wanandoa husika wanaweza kuamua kuendelea kuishi pamoja au kuomba ndoa kuvunjwa kwa sababu ya kutokuwepo kwa tendo la ndoa baina yao.

Kukosekana kwa tendo LA ndoa au kushindwa kwa mwanandoa kutekeleza tendo LA ndoa baada ya kufunga ndoa kunampa nafasi yule aliyeshindwa kutekelezewa haki ya kuvunjwa kwa ndoa hiyo.
 
nashukuru mkuu....... ila sasa kwa hii issue sharia ipo kimya?
Ndoa ni makubaliano ya watu wawili, whether ameathirika or not, agreement ya couples ndio itakayotazamwa zaidi. Kuweka sheria kwamba aliyeathirika asioe wakati wenyewe wamekubaliana ni sawa na kuwahumiliate waathirika ambapo ni kinyume na sheria. Though swala la kuathirika linaweza kupelekea ndoa kutofungwa endapo wanandoa wameridhia hivyo.
 
sheria ya ndoa ya mwaka 1971 inaeleza kuhusu void marriage na voidable marriage.
void marriage ni aina ya ndoa iliyofungwa ambayo haitambuliki kisheria kwa sababu wahusika (mwanamme na mwanamke) hawakuwa na vigezo vya kuoana . mfano kama mwanamke anandoa yake akiamua kuolewa tena hiyo ndoa ya pili haitatambulika kisheria kwa sababu sheria ya ndoa imekataza mwanamke kuolewa ktk ndoa mbili tofauti bila kupewa talaka ktk ndoa ya kwanza.
voidable marriage ni ndoa halali kwa mujibu wa sheria lakin endapo mmoja ya wanandoa ataleta ushahidi fulani uliojificha wakati wanaoana basi ndoa itavunjwa kisheria endapo ikithibitika hilo jambo.
mfano ni maradhi sugu au mwanaume hana uwezo wa kufanya tendo la ndoa. ikitokea watu wakafunga ndoa ya halali, ikaja kufahamika baadaye kuwa mmoja ni HIV+ yule ambaye ni negative au atayetaka kusitisha ndoa yao kutokana na tatizo hilo atatakiwa kuomba talaka mahakamani ndani ya mwaka mmoja tokea alipogundua tatizo hilo. nje ya muda huo sheria haitakuwa rafiki kwa upande wake.
 
Mkuu swali zuri sana moja kati ya vitu vinavyoweza mfanya mtu kuomba kuvunja ndoa mahakamani ni
@kutokuwepo na tendo la ndoa kuishi mbali kwa wanandoa kwa muda mrefu Kubadiri dini kwa mmojawapo baada ya ndoa ukatiri wa mmoja wa wanandoa nk
Nakuja kwa point yako kutokana na maradhi sheria yetu ipo kimya ila tayari kuna kesi kama hizo zimeshaamliwa hivyo tunatumia case law(maamuzi ya mahakama) uingereza kama mshirika wetu kimahakama (common law state) hiyo ndoa yaweza kuvunjwa na unahaki ya kuvunja na kama utahitaji msaada zaidi ni Pm kwa ushauri zaidi bureee
 
Last edited by a moderator:
Isipokuwa taasisi ya ndoa inaweza kuvunjwa pale tu Mahakama itakapothibitisha kuwa ndoa hiyo imeharibika kiasi kwamba haiwezi kurekebishika tena(broken down irreparable).

Wanandoa husika wanaweza kuamua kuendelea kuishi pamoja au kuomba ndoa kuvunjwa kwa sababu ya kutokuwepo kwa tendo la ndoa baina yao.

Kukosekana kwa tendo LA ndoa au kushindwa kwa mwanandoa kutekeleza tendo LA ndoa baada ya kufunga ndoa kunampa nafasi yule aliyeshindwa kutekelezewa haki ya kuvunjwa kwa ndoa hiyo.

Mahakama huwa inathibitishaje ukosefu wa tendo la ndoa kwenye ndoa?
 
Mahakama huwa inathibitishaje ukosefu wa tendo la ndoa kwenye ndoa?

Ili ndoa iwe rasmi ni pale ambapo wanandoa waweze kufanya tendo la ndoa. Endapo mwanandoa mmoja atashindwa kutekeleza tendo la ndoa yule mwanandoa mwingine anaweza kuiomba Mahakama kuivunja ndoa hiyo.

Kushindwa kutekeleza tendo la ndoa kunaweza kukasababishwa na maumbile ya kibaiolojia au magonjwa.

Kama umefunga ndoa na MTU aliyeathilika na HIV bila ya kujua fact hiyo na ukagundua fact hiyo Mara baada ya ndoa na kabla ya tendo LA ndoa .Hii inaweza kuchukuliwa kuwa mwanandoa aliyeathilika ameshindwa kufanya tendo LA ndoa kwa kuwa kufanyanae tendo LA ndoa kutapelekea yule mzima kuambukizwa.Ombi la kuomba ndoa hiyo kuvunjwa ipo kwa yule asiyeathilaka.
MAHAKAMA ITATHIBITISHA KUTOKUWEPO KWA TENDO LA NDOA KUPITIA VIPIMO VYA KITABIBU (MEDICAL TEST).
 
MAHAKAMA ITATHIBITISHA KUTOKUWEPO KWA TENDO LA NDOA KUPITIA VIPIMO VYA KITABIBU (MEDICAL TEST).

Ni vipimo gani hivyo ambavyo vinaweza kuthibitisha kuwa mtu hapewi tendo la ndoa na mwenzake?

Vinaitwaje hivyo vipimo?
 
Ni vipimo gani hivyo ambavyo vinaweza kuthibitisha kuwa mtu hapewi tendo la ndoa na mwenzake?

Vinaitwaje hivyo vipimo?

Mkuu naomba uisome post yangu ya mwisho na uielewe.Nimesema kuwa uwepo wa mwanandoa aliyeathilika na HIV na kama tatizo hilo halikujulikana kwa mwenza mwingine kabla ya ndoa na wawili hao hawajafanya tendo la ndoa.Mwanandoa asiyeathilika anaweza kuomba ndoa ivunjwe kwa kukosa tendo LA ndoa sababu ikiwa ni HIV. Nani asiyejua HIV inapimwaje?
 
Mkuu naomba uisome post yangu ya mwisho na uielewe.Nimesema kuwa uwepo wa mwanandoa aliyeathilika na HIV na kama tatizo hilo halikujulikana kwa mwenza mwingine kabla ya ndoa na wawili hao hawajafanya tendo la ndoa.Mwanandoa aliyeathilika anaweza kuomba ndoa ivunjwe kwa kukosa tendo LA ndoa sababu ikiwa na HIV. Nano asiyejua HIV inapimwaje?

Tuache hayo mambo ya HIV.

Turudi kwenye ulichoandika kuhusu kuvunjwa kwa ndoa kwenye bandiko lako namba 2.

Uliandika hivi:

Isipokuwa taasisi ya ndoa inaweza kuvunjwa pale tu Mahakama itakapothibitisha kuwa ndoa hiyo imeharibika kiasi kwamba haiwezi kurekebishika tena(broken down irreparable).

Sawa.

Wanandoa husika wanaweza kuamua kuendelea kuishi pamoja au kuomba ndoa kuvunjwa kwa sababu ya kutokuwepo kwa tendo la ndoa baina yao.

Okay, hapa ni unamaanisha hata katika mazingira ambayo hayahusishi HIV, siyo?

Kukosekana kwa tendo LA ndoa au kushindwa kwa mwanandoa kutekeleza tendo LA ndoa baada ya kufunga ndoa kunampa nafasi yule aliyeshindwa kutekelezewa haki ya kuvunjwa kwa ndoa hiyo.

Kiini cha swali langu kipo hapo. Tukiweka pembeni suala la HIV, katika hali ya kawaida, endapo tendo la ndoa likakosekana kwenye ndoa, ukosefu wa tendo hilo unaweza ukawa ni msingi wa kuvunjwa kwa ndoa, si ndiyo?

Sasa basi, ili mahakama ifikie uamuzi wa kuivunja hiyo ndoa, kwa mujibu wa ulichokiandika wewe ni kwamba "taasisi ya ndoa inaweza kuvunjwa pale tu Mahakama itakapothibitisha kuwa ndoa hiyo imeharibika kiasi kwamba haiwezi kurekebishika tena(broken down irreparable)."

Swali langu ni hili: mahakama huwa inathibitishaje kuwa tendo la ndoa kwenye ndoa ya fulani na fulani halipo? Je, mahakama hutegemea tu maneno ya muombaji/ mtaka talaka na maneno mtalaka mtarajiwa?

Kuna njia gani ingine ya kuthibitisha hali ya huo ukosefu wa hilo tendo?
 
Ukisoma vizuri mabandiko yangu utagundua kuwa nimesema kuwa kushindwa kufanya tendo la ndoa kunaweza kusababishwa na maumbile ya kibaiolojia au magonjwa.Sasa mtu kama ni impotent(hanisi) inshindikanaje kupimwa kitabibu?

Inawekana mwanandoa mmoja hana kiungo cha kufanya tendo la ndoa hapo mahakama inashindwaje kuthibitisha?

NB. Fahamu kuwa kipimo cha ndoa kuchukuliwa kama imeharibika kiasi cha kushindwa kurekebishika kinatumika kwa wanandoa ambao ndoa yao ilikamilika kwa vigezo vyote ikiwa ni pamoja na tendo la ndoa .Mara bsada ya kuvunjwa kwa ndoa hii wawili hao wataitwa wataliki (Divorced and Divorcee).Lakini ndoa inayovunjwa kwa ukosefu wa tendo hiyo ni voidable marriage (inaweza kuvunjwa na kuonekana kama hakujawahi kuwa na ndoa kati ya wawili hao).
 
Ukisoma vizuri mabandiko yangu utagundua kuwa nimesema kuwa kushindwa kufanya tendo la ndoa kunaweza kusababishwa na maumbile ya kibaiolojia au magonjwa.Sasa mtu kama ni impotent(hanisi) inshindikanaje kupimwa kitabibu?

Je, kama mtu hana tatizo la kimaumbile au ugonjwa unaoweza kusababisha kushindwa kufanya hilo tendo lakini hapendi tu kulifanya na mwenzake kwa sababu anazozijua yeye, mahakama huthibitishaji hilo?
 
Je, kama mtu hana tatizo la kimaumbile au ugonjwa unaoweza kusababisha kushindwa kufanya hilo tendo lakini hapendi tu kulifanya na mwenzake kwa sababu anazozijua yeye, mahakama huthibitishaji hilo?

Akisema mbele ya Mahakama kama hajawahi kujamiiana na mwenzie eti kwasababu tu hapendi.Hapo mahakama itakuwa imerahisishiwa kazi kwakuwa muhusika mwenyewe kathibitisha kuwa hapendi kufanya hivyo.
 
Akisema mbele ya Mahakama kama hajawahi kujamiiana na mwenzie eti kwasababu tu hapendi.Hapo mahakama itakuwa imerahisishiwa kazi kwakuwa muhusika mwenyewe kathibitisha kuwa hapendi kufanya hivyo.

Vipi kama mmoja (mwanamme mdai talaka) akisema hakuna tendo la ndoa kwenye ndoa yake huku mwanamke akisema lipo, hapo inakuwaje?

Nani ataaminiwa kuwa anasema ukweli?
 
Kesi ni evidence na hvyo basi anayesema hamna tendo hlo anatakiwa kuithibishia mahakama,(should convis the court)
 
Ndoa ni muungano wa hiyari ,hapa tz hakuna Sheria inayolazimisha wanandoa kuishi kwa shuruti.Isipokuwa taasisi ya ndoa inaweza kuvunjwa pale tu Mahakama itakapothibitisha kuwa ndoa hiyo imeharibika kiasi kwamba haiwezi kurekebishika tena(broken down irreparable).

Wanandoa husika wanaweza kuamua kuendelea kuishi pamoja au kuomba ndoa kuvunjwa kwa sababu ya kutokuwepo kwa tendo la ndoa baina yao.

Kukosekana kwa tendo LA ndoa au kushindwa kwa mwanandoa kutekeleza tendo LA ndoa baada ya kufunga ndoa kunampa nafasi yule aliyeshindwa kutekelezewa haki ya kuvunjwa kwa ndoa hiyo.

Mkuu umesahau kuwa hata maradhi , kufungwa jela inaweza kuwa sababu tosha ya kuvunjwa ndoa..so HIV inaangukia kwenye maradhi..unaweza kuvunja ndoa mkuu
 
Back
Top Bottom