Msaada wa Kisheria: Mdogo wangu ametapeliwa Ardhi na rafiki yake wa karibu

ris

Member
Jun 16, 2017
73
109
Wanajamvi naombeni msaada wenu wa kisheria katika hili.

Iko hivi nina mdogo wangu wa hiari (tumekutana kazini sina vinasaba nae) mnamo mwezi wa nne alisimamishwa kazi.

Hivyo kutokana na majukumu ya kifamilia akaamua ajiingize kwenye biashara ya kununua mahindi na kuuza.

Changamoto ikawa mtaji maana mzigo upo ila mtaji haukidhi akajaribu kuomba mikopo ikashindikana akaamua kuuza baadhi ya vitu vyake vya ndan kama tv, fridge na kiwanja kimoja (alikua na viwanja viwili).

Mambo yote hayo alikua anayafanya na rafiki wa karibu sana ambapo walifanikisha kuuza vitu vya ndani kwa haraka kuliko kiwanja. Hivyo ikamlazimu dogo arudi vijijini kutafuta mahindi akampa taarifa huyo rafiki yake kuwa wasitishe zoezi la kuuza kiwanja. Wakati akiwa kijijini jamaa yake aliingia nyumbani kwa dogo akaibia document zote za viwanja akaenda akauza na hela akaenda akanunua gari ya kutembelea. Dogo akiwa kijijini aliibiwa hela tsh milioni tisa

Akaamua arudi mjini kuuza viwanja vyake aongezee mtaji maana tayari umepungua anakuta kiwanja kimoja kuna mtu anajenga kufuatilia anaambiwa kwenye uongozi wa mtaa anaambiwa viwanja vyake vimeuzwa viwili na alipigiwa simu siku vinauzwa na akatoa ruhusa (yeye dogo anadai hakupigiwa simu)

Ameenda polisi wamemuambia kama hana copy za document za ununuaji wa viwanja akubali tu maumivu wao hawana cha kumsaidia.

Amejaribu kukutana na wamiliki wapya wa viwanja kwa maongezi ya usitishaji wa ujenzi lakini huyo rafiki yake anawaambia nyie endeleeni na ujenzi huyo hana documnet zozote asiwatishe. Sasa dogo amekwama asijue nini cha kufanya hivyo naomba kwa wenye ujuzi mtusaidie msaada wa kisheria hapa tunafanyaje.
 
1. Kiwanja kina hati au mkataba wa manunuzi?
2.Mashahidi wakati wa kukinunua ni akina nani?
3.Document zilikuwa na majina gani?
1.Viwanja vyote havina hati vina mikataba ya manunuzi ambayo ndo hiyo jamaa yake aliiba akaenda kuuzia
2.Miongoni mwa mashahidi wakati anakinunua ni mimi kwa viwanja vyote viwili na huyo jamaa yake alieviuza
3.Document zilikua na majina ya dogo ila aliuza muuzaji akisema kuwa amepewa ruhusa na mmiliki na akafake kwa kupiga simu akiwa na viongozi wa mtaa
 
Aanzie wizarani ila atoe taarifa ya loss report polisi kama viwanja vina hati mtu mwingine hawezi kuuza bila idhini ya mwenye hati Sheria zipo za kumlinda mwenye hati
Polisi wanamzungusha inaonekana jamaa yake ana ushawishi upande huo maana walimwambia alitakiwa awe na copy ya mikataba ya mauziano ndo wampe loss report
 
huyo rafikiye aliingiaje ndani(nyumbani)kwa mdogo wako na kuiba documents za hivyo Viwanja??alivunja mlango??alitumia funguo bandia au ilikuaje??jibu kwanza hilo tujue maana kama Jinai inabidi ianzie hapo kwamba documents muuzaji alizipata vipi??
 
Nashukuru kwa mchango wako lkn hauko sahihi
Acha ujanja ujanja kijana ,hapo juu umesema ulikuwa shahidi wa rafiki yako wakati ananunua viwanja na ukawa shahidi wa jamaa aliyemuibia wakati anauza, kwa nini uwe shahidi wa mtu ambaye unajua sio chake?
 
1.Viwanja vyote havina hati vina mikataba ya manunuzi ambayo ndo hiyo jamaa yake aliiba akaenda kuuzia
2.Miongoni mwa mashahidi wakati anakinunua ni mimi kwa viwanja vyote viwili na huyo jamaa yake alieviuza
3.Document zilikua na majina ya dogo ila aliuza muuzaji akisema kuwa amepewa ruhusa na mmiliki na akafake kwa kupiga simu akiwa na viongozi wa mtaa
Kama shahidi wakati wa ununuzi basi nendeni mahakamani kwa kusakdiana na serikali za mtaa
 
Acha ujanja ujanja kijana ,hapo juu umesema ulikuwa shahidi wa rafiki yako wakati ananunua viwanja na ukawa shahidi wa jamaa aliyemuibia wakati anauza, kwa nini uwe shahidi wa mtu ambaye unajua sio chake?
Umeelewa vibaya nilikua shahidi wakati dogo anananua mashahidi nilikua ni mimi na huyo jamaaa yake nadhani hii itakua mara ya mwisho kukujibu maana naona mimi na wewe tunapishana uelewa wa mambo
 
Acha ujanja ujanja kijana ,hapo juu umesema ulikuwa shahidi wa rafiki yako wakati ananunua viwanja na ukawa shahidi wa jamaa aliyemuibia wakati anauza, kwa nini uwe shahidi wa mtu ambaye unajua sio chake?
ndugu mbona umekaza fuvu tu, kama humuamini si upite kushoto!
 
huyo rafikiye aliingiaje ndani(nyumbani)kwa mdogo wako na kuiba documents za hivyo Viwanja??alivunja mlango??alitumia funguo bandia au ilikuaje??jibu kwanza hilo tujue maana kama Jinai inabidi ianzie hapo kwamba documents muuzaji alizipata vipi??
Acha kuhangaika na mleta mada ni yeye ndiye aliyemuibia mshikaji anatafuta huruma ya sheria. Nilichogundua ni kwamba huyo anayemuita mdogo wake ni mtu aliyemuamini na kumshirikisha Mambo mengi mpaka kufikia kuniamini Kama mdhamini wakati anannunua hivyo kwa maana nyingine huyo ndo mtu mwenye taarifa kamili ya uwepo wa document hizo na sehemu gani zipo
 
Back
Top Bottom