Msaada wa kisheria kuhusu talaka

Mama Joe

JF-Expert Member
Mar 30, 2009
1,504
828
Jamani wana JF, ninaomba mumsaidie huyu mama msaada wa kisheria jinsi gani apate talaka yake,
" Niliolewa ndoa ya kanisani 1999, nikazaa mtoto mwaka huo huo, tabia ya uzinzi ya mume wangu nikimfumania zaidi ya mara 3 na anakiri na kuomba msamaha, ugomvi, manyanyaso vilinifanya mwaka 2003 kurudi kanisani RC kuomba msaada. Wao walinielekeza nitafute ndugu zake wamwonye, hakusikia, hivyo 2003 nilirudi nyumbani na mtoto kuelezea tatizo. Wazazi walimwita ili aje asikie malalamiko yangu hakutaka kutokea na baada ya miezi 2 waliniambia nikachukue changu niondoke hapo, hakujali alisema niende tu hana shida na mimi. Hivyo miaka yote hii ninalea mtoto na nimekaa mwenyewe. Karibuni nimeona napoteza muda na ningependa kuolewa tena, kanisani wameniruhusu, ila nikavunje hiyo ndoa mahakamani.
Tatizo nimeanzia ustawi wa jamii wananiambia nimlete huyu mume hapo wakati mie sijui hata sasa hivi anaishi wapi, bahati nzuri karibuni nikaitwa na wenzie nikamuone amelazwa mgonjwa sana hospital, ila alipotoka tu sijui tena alipo. Sasa mie ombi langu ni nipate talaka yangu, je inawezekana niende mahakamani moja kwa moja na kudai bila hawa ustawi wanaonizungusha?
Pili kutokana na hali yake nadhani hataweza kusimama mahakamani, nami wala sintapenda kumsimamisha mgonjwa namuonea huruma je mahakama inaweza toa talaka hata kama mwingine hajulikani aliko?"
Mie sio mwanasheria msaada wenu please nimjibu nini, asante
 
Mama Joe..
Asante kwa kisa hiki.
Kwa kawaida mwanandoa yeyote anayedai talaka ana jukumu la kuthibitisha kwamba ndoa imevunjika kabisa (marriage has broken down irreperably), hii ndio test ya kwanza kabisa ambayo huyu mama atatakiwa kuthibitisha.,sasa ataweza vipi kufanya hivyo, ni kupitia ushahidi wa matukio kama hayo ya uasherati (adultery).
Kwa msaada zaidi nakuwekea vifungu hivi vya Sheria ya Ndoa ya Tanzania Sura ya 29 [RE:2002]

Hiki ni kifungu cha 99
Right to petition for separation or divorce
Subject to the provisions of sections 77, 100 and 101, any married person may petition the court for a decree of separation or divorce on the ground that his or her marriage has broken down but no decree of divorce shall be granted unless the court is satisfied that the breakdown is irreparable.

Hiki ni cha 107(2)
(2) Without prejudice to the generality of subsection (1), the court may accept any one or more of the following matters as evidence that a marriage has broken down but proof of any such matter shall not entitle a party as of right to a decree–
(a) adultery committed by the respondent, particularly when more than one act of adultery has been committed or when adulterous association is continued despite protest;

Lakini sheria inataka kwamba kabla hujapeleka maombi ya talaka mahakamani ni lazima kwanza upite katika baraza la usuluhishi la ndoa ambalo lina jukumu la kuwapatanisha na ikishindikana wao wanacertify kuwa wameshindwa kuwasuluhisha hivyo muende mahakamani, sasa kwa case ya huyu mama ambaye hajui mumewe yupo wapi basi sheria inampa uwezo wa kutokwenda kwenye baraza la usuluhishi hivyo kwenda mahakamani moja kwa moja, kifungu hiki cha 101 (a) Kinahusika zaidi.

101. Requirement of prior reference to Board
No person shall petition for divorce unless he or she has first referred the matrimonial dispute or matter to a Board and the Board has certified that it has failed to reconcile the parties:
Provided that this requirement shall not apply in any case–
(a) where the petitioner alleges that he or she has been deserted by, and does not know the whereabouts of, his or her spouse;
ANGALIZO
Kifungu hiki cha sheria kitamsaidia iwapo tu atabadili sababu ya maombi yake ya talaka kutoka kwenye uasherati (adultery) na kuwa kutelekezwa (dessertion) ili kumsaidia kupata talaka yake haraka kwani inavyoonekana kutokomea kwa huyo mume mi mpango wa makusudi ili huyu mama asifanikiwe lengo lake.
 
Mahakama haiwezi toa talaka hadi pande zote zisikilizwe na uthibitisho uwepo kwamba alitenda kosa ulilolitaja.Yamkini yeye aweza kusema anakupenda na hana mpango wa kukuacha na hatoi talaka.Hiyo inakuwa vigumu ila kama kuna uthibitisho wa yeye kufumaniwa,au ushahidi wa jinsi asivyoweza kukuhudumia basi kwa hali hiyo mahakama itatumia busara kuweza kusaidia kupata talaka.Lakini Mama Joe kama umesema hali yake ni mahututi yamkini Israeli atamtembelea wakati wowote basi na iwe amri ya Mungu pale kifo kitakapowatenganisha.
 
Mama Joe..
Asante kwa kisa hiki.
Kwa kawaida mwanandoa yeyote anayedai talaka ana jukumu la kuthibitisha kwamba ndoa imevunjika kabisa (marriage has broken down irreperably), hii ndio test ya kwanza kabisa ambayo huyu mama atatakiwa kuthibitisha.,sasa ataweza vipi kufanya hivyo, ni kupitia ushahidi wa matukio kama hayo ya uasherati (adultery).
Kwa msaada zaidi nakuwekea kifungu hiki cha Sheria ya Ndoa ya Tanzania Sura ya 29 [RE:2002]

Naona hapa ndio anapokwama maana miaka imepita, na huo ushahidi wa kitu gani ampeleke mashahidi au nini, maana ni kama ameamka toka miaka mingi aliyoachwa na kutaka haki yake, sijui napo kakosea?
 
mama joe,asante kwa kisa hiki but my advice iz huyo mama kapima lkn?maana isije ikawa anataka ndoa but pia hajajua kuhusu afya yake.ZINGUKA,TANZANIA BILA UKIMWI INAWEZEKANA
 
Mahakama haiwezi toa talaka hadi pande zote zisikilizwe na uthibitisho uwepo kwamba alitenda kosa ulilolitaja.Yamkini yeye aweza kusema anakupenda na hana mpango wa kukuacha na hatoi talaka.Hiyo inakuwa vigumu ila kama kuna uthibitisho wa yeye kufumaniwa,au ushahidi wa jinsi asivyoweza kukuhudumia basi kwa hali hiyo mahakama itatumia busara kuweza kusaidia kupata talaka.Lakini Mama Joe kama umesema hali yake ni mahututi yamkini Israeli atamtembelea wakati wowote basi na iwe amri ya Mungu pale kifo kitakapowatenganisha.
Hii pia ni option nyingine, ila mtu ukae unamuombea mbaya wako afe ili wewe uolewe naona ni issue nyingine, ndio maana kanis ala huyu mama limempa uhuru ila tu hiyo ndoa yake ivunjwe isilete mushkeri.
Sasa mie najiuliza huyu mtu ambaye miaka saba haonekani kisheria anatambulika ni mume? Namaanisha kitu gani aonyeshe kuwa huyu mtu sijui alipo wala matunzo kwa mtoto sipati?
 
mama joe,asante kwa kisa hiki but my advice iz huyo mama kapima lkn?maana isije ikawa anataka ndoa but pia hajajua kuhusu afya yake.ZINGUKA,TANZANIA BILA UKIMWI INAWEZEKANA

Thanks dear, ni mzima wa afya na ni best wangu tulimshauri kupima mara tu alipoondoka kwa mumewe, pia mwaka jana amepima, hana tatizo kabisa.
 
ok thats very gud dia,pole kwa matatizo haya ndo todays news kila sikuni talaka kuachana thats our planet Earth
Thanks dear, ni mzima wa afya na ni best wangu tulimshauri kupima mara tu alipoondoka kwa mumewe, pia mwaka jana amepima, hana tatizo kabisa.
 
Mama Joe..

ANGALIZO
Kifungu hiki cha sheria kitamsaidia iwapo tu atabadili sababu ya maombi yake ya talaka kutoka kwenye uasherati (adultery) na kuwa kutelekezwa (dessertion) ili kumsaidia kupata talaka yake haraka kwani inavyoonekana kutokomea kwa huyo mume mi mpango wa makusudi ili huyu mama asifanikiwe lengo lake.

Hapa nimekusoma nami nakubaliana nawe nahisi mwanamme anafanya kusudi, naona arudi tena barazani na kuwaeleza hili kwa mara nyingine, kisha aende tu mahakamani kujaribu tena
 
ok thats very gud dia,pole kwa matatizo haya ndo todays news kila sikuni talaka kuachana thats our planet Earth
Ni kweli yaani inasikitisha watu kufanya life commitment halafu wasizitimize, wanachukulia simple tu, mbaya zaidi mtoto anakosa malezi ya mzazi mmoja
 
Sambamba na michango mingine, hoja iliwahi kujadiliwa hapa hivi:

TALAKA

Kuhusu taraka sheria ya ndoa inaweka bayana haki ya mwana ndoa yeyote kuomba talaka au kutenganishwa. Kuhusu taraka, Mahakam inaweza kutoa pale itakaporidhika kuwa ndoa kati ya mwombaji na mjibu maombi imevunjika na haiwezi tenga kutengamaa au kurekebishika(broken down irreparable). Sheria inaelekeza ifuatavyo:


……………………Any married person may petition the court for a decree of separation or divorce on the ground that his or her marriage has broken down. but no decree of divorce shall be granted unless the court is satisfied
that the breakdown is irreparable.

Sheria inaweka vigezo vifutavyo kutambua kuwa ndoa haiwezi kutenga maana na ndio sababu zinazomwezesha mwanandoa kuomba talaka;

(a) pale mwomba talaka atakapothibitisha kuwa mwezake ametenda uzinzi (adultery) zaaidi ya mara moja na anaendelea kufanya hivyo;

(b) mjibu maombi/ mdaiwa ni msumbufu katika ndoa (sexual perversion)

(c) mjibu maombi/ mdaiwa ametenda vitendo vya kikatili kwa mfano kumpiga mdai au watoto vipigo visivyo cha kawaida au kumnyima chakula nk (cruelty) ;

(d) mjibu maombi/ mdaiwa kutokuwa tayari kwa makusudi kutoa "unyumba" au kushiriki tendo la ndoa.

(e) mjibu maombi/ mdaiwa kumtelekeza mdai au familia kwa zaidi ya miaka mitatu

(f) iwapo mjibu maombi/ mdaiwa atakuwa amehukumiwa kifungo cha maisha zaidi ya miaka mitano jela (ili litazingatia zaidi aina ya kosa alilotenda na kifungo anachotumikia) si wakati wote inaweza kusaidia.

(g) Iwapo itathibitishwa na madaktari zaidi ya mmoja wenye uzoefu na magonjwa ya akili kuwa mjibu maombi/ mdaiwa anasumbuliwa na ugonjwa wa akili ambao hawezi kupona.

(h) Iwapo mjibu maombi/ mdaiwa atakuwa amebadili dini ikiwa wahusika wote walikuwa wakifuata dini moja wakati walipooana na ikiwa kwa sharti la dini hiyo inaweka sharti kuwa kubadili dini kunaweza kuvunja ndoa (change of religion by the respondent, where both parties followedthe same faith at the time of the marriage and where accordingto the laws of that, faith a change of religion dissolves or is aground for the dissolution of marriage) .


UTARATIBU WA KUWASILISHA MAOMBI YA TARAKA MAHAKAMANI

Sheria ya Ndoa inatafsri ndoa kuwa ni muungano wa hiyari kati ya mtu mke na mtu mume ambao wamedhamiria kuishi pamoja katika maisha yao yote. Adidha, ndoa inachukuliwa kama mkataba ambao unaweza pia kuvunjika iwapo kuna tatizo au kutokuelewana kwenye masharti ya makubaliano hayo au mmoja kati ya wahusika kushindwa kuheshimu au kutotimiza wajibu wake katika makubalinao.

Hata hivyo, ndoa haiwezi kuvunjwa iwapo haijaikisha umri unaotambulika kisheria na maombi ya kuivunja hayajazingatia utaratibu wa kuyawasilisha Mahakamani. Sheria ya ndoa inasema:

*******No person shall, without the prior leave of the court, petition for divorce before the expiry of two years from the date of the marriage which it is sought to dissolve. Leave shall not be granted to petition for divorce within two years of marriage except where it is shown that exceptional hardship is being suffered by the person applying for such leave******


No person shall petition for divorce unless he or she has first referred the matrimonial difficulty to a Board 'and the Board has certified that it has failed to reconcile the parties: (Board – Mabaraza ya ndoa au Marriage Reconciliatory Boards)

Mabaraza ya usuluhishi ya ndoa ni yale yanayotambulika kisheria kwa mfano kupitia madhebu ya Dini kuna mabaraza yab ndoa.

Sharti la kuanzia kwenye Baraza la Usuluhisi wa ndoa linaweza lisizingatiwe katika mazingira yafuatayo:

(a) where the petitioner alleges that he or she has been deserted by, and does not know the whereabouts of, his or her spouse; or

(b) where the respondent is residing outside Tanganyika and it is unlikely that he or she will enter the jurisdiction within the six months next ensuing after the date of the petition; or

(c) where the respondent has been required to appear before the Board and has wilfully failed to attend; or

(d) where the respondent is imprisoned for life or for a term of at least five years or is detained under the Preventive Detention Act, and has been so detained for a period, exceeding six months, or

(e) where the petitioner alleges that the respondent is suffering from an incurable mental illness; or

(f) where the court is satisfied that there -are extraordinary circumstances which make reference to the Board impracticable.

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-sheria-the-law-forum/45799-sheria-ya-ndoa-2.html

 
Ustawi wa Jamii bongo ni longalonga tu. Hawa ndio wanaowafanya wanawake wengi hata wanaume wanateseka kupata haki zao. Talaka ni haki ya mdai na mdaiwa kwa nini iwe na uwalakini. Wenyewe wameshafika mahali hawawezani tena ninyi mnataka wasuluhishe ili iweje? Ombi la talaka linachukua miaka kumi huku si kunyimana haki wajameni? Mahakama, Ustawi wa jamii wote dugu moja rushwa kwa sana ndio tatizo.
 
Jamani nashukuru sana kwa msaada huu, maana binafsi nimekaa na swali hili muda sikuwa najua nimsaidieje, mbarikiwe wote. Na print hizi inforamtion zoote nadhani wiki ijayo ataanza tena kudai haki yake
 
Back
Top Bottom