Msaada wa kimawazo

Lady G

JF-Expert Member
Dec 13, 2010
515
130
Kuna rafiki yangu ambae amezaa na mwanaume, mtoto anamiaka mi 3 sasa, mahusiano yao yanamiaka mitano. Mpk leo huyo mwanaume hajasema chochote khs ndoa japo huyo dada sn anafahamika upande familia ya mwnaume. Ila mwanaume hafahamki sn upande wa ukeni, mwanaume anawatoto wa2 wakubwa tu. He is now 43 yrs. Juzi kati wametofautiana na mwanamke kaamua kumuacha. Ila bado anampenda anaomba ushauri ktk kpnd hk kuelekea mwak mpya, abaki na donge la hasira moyoni, au amsamehe lkn mahusiano yasiwepo?
 
mh 45 sasa ndugu mahusiano yasiwepo atampat huyo mwengine???? allahu yaalamm,,,,maybe she can bcouse vijana wa sasa wanatafuta majimama wenyewe,,, all dah best inshaallah!!
 
Atulie na kulea mwanaye...huyo jamaa middle age...hana pakukimbilia...nini faida ya ndoa kama haina maelewano,upendo na uvumilivu???
 
Kwa maoni yangu mwanamke 32 still anaweza kupata mtu wa kumuoa maana siku kuna watu wanataka age hiyo so let her hope for the best kama akitokea akakubali kwenda na hali yake
 
i also think the same idea,,,, better to stay far from him,,, he is nothing but something,,,,
Kwa maoni yangu mwanamke 32 still anaweza kupata mtu wa kumuoa maana siku kuna watu wanataka age hiyo so let her hope for the best kama akitokea akakubali kwenda na hali yake
 
Asante kwa maoni/ushauri napata point za kumshauri

Lady ilikuwaje huyo rafiki yako akakaa na jamaa for 5 years na hawajafunga ndoa ina maana hajawahi kumgusia jamaa kuhusu suala la ndoa within those 5 years au ndio life style waliyokuwa wameamua kuishi nayo
 
Wamekorofishana nini lady? Ila kuwekeana kinyongo c vzr hata kama hawatakani tena akumbuke wana mtoto ambae atakua anawakutanisha
 
Kuna rafiki yangu ambae amezaa na mwanaume, mtoto anamiaka mi 3 sasa, mahusiano yao yanamiaka mitano. Mpk leo huyo mwanaume hajasema chochote khs ndoa japo huyo dada sn anafahamika upande familia ya mwnaume. Ila mwanaume hafahamki sn upande wa ukeni, mwanaume anawatoto wa2 wakubwa tu. He is now 43 yrs. Juzi kati wametofautiana na mwanamke kaamua kumuacha. Ila bado anampenda anaomba ushauri ktk kpnd hk kuelekea mwak mpya, abaki na donge la hasira moyoni, au amsamehe lkn mahusiano yasiwepo?

Lady, nisaidie kufahamu ni nani ambae bado anampenda mwenzake na anataka kumrudia, kati ya mwanamke na mwanaume??? Na chanzo cha kukosana kati ya wawili ni nani kati ya m/ke na m/ume??

naona wametofautiana na mwanamke kaamua kumuacha, lakini sijajua vema nini chanzo cha mgongano na nani bado anampenda mwenzie na anataka kumrudia. NISAIDIE HAPA KWANZA
 
ndoa si jambo la kukurupuka na unaweza kuwa katika uhusiano hata wa miaka kumi na usiwe na sifa za kuingia kwenye ndoa.wanaume wako makini sana katika hili na unaweza kushaangaa akakuacha wewe uliyedumu naye miaka yote kisha akapata mpenzi miezi sita tu akatangaza ndoa.kuishi na mtu miaka mingi sio sababu na mtoto pia sio sababu.
pia yawezekana wakati wanaanza uhusiano walikuwa na makubaliana tofauti ndio hayo ya kuzaa yakatokea mbeleni ila mwanaume hakuwa na mpango wa ndoa.
ushauri.
kama bado wanapendana wawe pamoja hakuna haja ya hasira kibao.akae na mwanaume walizungumzie hilo na amuoneshe nia yake ya kuhitaji kuolewa kwa vitendo sio maneno zaidi(namaanisha aanze kubehave kama mwanandoa mtarajiwa)
wish her luck
 
Hawajawahi kuishi pamoja, ni mahusiano tu, kwa hyo miaka mi 5 na ndani ya mahusino akapatikana mtoto, yule dada kila akimuuliza huyo m'me khs ndoa, haonyeshi kujali sana, ila anamwambia anajipanga. Dada wa mwanaume na ndg wanampenda sn huyo dada. Tatizo mwanaume haeleweki ana msimamo gani
 
Tofauti yao anasema ni ugomvi wa mara kwa mara. Mwanaume kutomjali huyo dada wala mtoto, he dont show love any more. Japo m'me anasema anampenda huyo dada.
 
Hawajawahi kuishi pamoja, ni mahusiano tu, kwa hyo miaka mi 5 na ndani ya mahusino akapatikana mtoto, yule dada kila akimuuliza huyo m'me khs ndoa, haonyeshi kujali sana, ila anamwambia anajipanga. Dada wa mwanaume na ndg wanampenda sn huyo dada. Tatizo mwanaume haeleweki ana msimamo gani

Lady kama mwanaume haeleweki msimao wake basi ni mtu hatari huyo.

Kwa muda wote aliokaa na mwanaume mpaka sasa haonyeshi msimamo wowote?????? Hapana kwa kweli.

Am against kutengana kwa watu walioko kwenye mahusiano but am more against na mtu ambae haonyeshi u-serious kwenye mahusiano.

Let her take time, he still can find better future. Ajiamini tu kwamba anaweza kuwa na future nzuri, atulie ajipange na kulea mtoto wake vema, then kujiheshimu na upendeo wa dhati ulio ndani yake ULIOMFANYA KUVUMILIA USAINI WA JAMAA MIAKA YOTE, utamsaidia kupata mtu alieko serious nae.

Mpe pole kwa masahibu yote na mwambie asi-give up, bado umri una mruhusu
 
ndoa si jambo la kukurupuka na unaweza kuwa katika uhusiano hata wa miaka kumi na usiwe na sifa za kuingia kwenye ndoa.wanaume wako makini sana katika hili na unaweza kushaangaa akakuacha wewe uliyedumu naye miaka yote kisha akapata mpenzi miezi sita tu akatangaza ndoa.kuishi na mtu miaka mingi sio sababu na mtoto pia sio sababu.
Pia yawezekana wakati wanaanza uhusiano walikuwa na makubaliana tofauti ndio hayo ya kuzaa yakatokea mbeleni ila mwanaume hakuwa na mpango wa ndoa.
Ushauri.
Kama bado wanapendana wawe pamoja hakuna haja ya hasira kibao.akae na mwanaume walizungumzie hilo na amuoneshe nia yake ya kuhitaji kuolewa kwa vitendo sio maneno zaidi(namaanisha aanze kubehave kama mwanandoa mtarajiwa)
wish her luck

wewe halafu hiyo signature yako
 
sio kila kitu ni mwanaume ndio a-initiate,mwambie rafiki yako avunje ukimya amuulize kwa upole nini hatma ya mapenzi yao,ana mpango gani naye...
sio wote wanalifeel hilo swaga la ndoa,kutotangaza ndoa haimaanishi huyo kaka hampendi,ajipime mwenyewe huyo dada aone mapenzi ya huyo kaka yakoje....kama anampenda na yuko rensposible as a father and as a lover -and she is happy,theni sioni umuhimu wa cheti cha ndoa-kitabaki kuwa karatasi!!!ila kama anadoubt mapenzi ya huyo kaka kwake then achape lapa.

ndoa ni makaratasi tu hayana meaning kama hauko happy,anaweza amuache huyo kaka ampate mtu mwingine atakayetangaza ndoa haraka haraka..ila mapenzi yasiwepo,so ni yeye na uamuzi wake anataka nini:teeth:
 
Mimi ningependa pia kusikia upande wa mwanaume pia kwasababu hadi sasa hivi ni upande wa mwanamke tu ndio unazungumziwa ambaye ndiye kaleta haya malalamiko so it will be wise kama mwanaume nayo akatoa malalamiko yake pia then tukapima uzito.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom