Msaada wa haraka tatizo la damu

fedawa

Member
Dec 16, 2014
40
7
jaman natumain mu wazima.

mi ni bint ,nna tatizo la kupungua damu tangu mwez wa kwanza.nikitumia vyakula au dawa inapanda hata had 13,lakn nikiacha baada ya wiki kama tatu naikuta 9,,.nimepima vipimo ving kama full blood picture,vidonda vya tumbo ,minyoo,kote naambiwa niko normal cna tatizo.kiukweli nachanganyikiwa sana cjui cha kufanya.mwezin naenda kama kawaida cna tatizo lolote.
madokta na watu wengine wenye ujuz mbalimbali naomba mnisaidie nateseka sana.
 
Tatizo lako linaweza kuwa linatokana na kasoro katika:

A:uzalishaji wa cell nyekundu za damu ambazo huzalishwa katika bone marrow au R.B.C zinazozalishwa hazipo sawa(abnormal).

B:pia inaweza kuwa ni kutokea kwa uharibifu wa cell nyekundu kabla ya umri wake..umri wa R.B.C ni siku 100-120.

C:pia inawezekana ni tatizo la urithi kama Thalassaemia au sickle cell.

Thalassaemia ni defect iliyopo katika gene ambayo hupelekea kuzalishwa kwa abnormal RBC na dalili zake ni kuchoka,fainting,kupumua kwa shida na fatigue.

Kuna aina kama 2 za Thalassaemia ambazo ni:

1:alpha Thal ambapo gene moja ndiyo inayokuwa na tatizo na haina athari sana kwa mtu na kama zimeathirika mbili basi mtu huyo atakuwa na anemia ya kati na kama ni tatu huyo mtu atakuwa na Haemoglobin H disease ambayo itamuhitaji kufanyiwa bood transifusions ili kuitibu chronic anaemia,

2:Beta Thal ambayo ipo katika hali tofauti tofauti kama beta thalassaemia major(BTM) hiyo maisha yote ni kubadilisha damu na hasa kwa kipindi cha wiki 4-6,na pia kula vyakula vyenye calcium nyingi,vitamini D na kufanya mazoezi kuimarisha mifupa

Then kuna beta thalassaemia intermedia(BTI) hii ni non-transfusion dependant thalassaemia(NTDT) kwa jina jingine na hii ipo katika hali ya kati na inatofautiana kati ya mtu na mtu kuanzia mild anaemia hadi kubadilishwa damu mara kwa mara na hapa matibabu yanatofautiana kati ya mtu na mtu kuanzia kupewa supplements za folic acid hadi kubadilishiwa damu.

Thal ni ugonjwa wa KURITHI na utagundulika kwa kuchukua vipimo vya damu na mara nyingi mgonjwa anaweza akaambia ana upungufu wa madini ya chuma tu kama hatachukuliwa vipimo vya uhakika.

Matatizo yasababishwayo na Thal ni kama

1:kuongezeka kwa ukubwa wa kongosho

2:Matatizo ya hormone ambayo yanapelekea ukuaji wa mwili kuwa taratibu na kuchelewa kubalehe au kuvunja ungo.

3:Matatizo ya moyo ikiwemo mapigo ya moyo kutokuwa regular na heart failure.

4:Matatizo ya ini ikiwa ni pamoja na hepatitis na ini kuwa kubwa(fibrosis) na cirrhosis

5:Matatizo ya mifupa kama maumivu ya viungo na osteoporosis.

Sasa pia naweza kuelezea kwenye kifungu A.pale juu kwa ufupi kama ifuatavyo.

Mtu unaweza kuwa na Anaemia kama mwili utazalisha RBC chache au RBC zilizo na matatizo kutokana kuwa na upungufu wa madini na vitamins ya kuzalishia RBC,na hapa unaweza kuwa na

1:Iron-deficiency anemia
2:Vitamins deficiency anemia
3:Bone marrow na stem cell problem
4:na sababu nyingine tu za kiafya.

Kwenye Vitamins-deficiency inasababishwa na kutokula vyakula vyenye madini chuma vya kutosha hasa katika infant stage,children,teens.

Kwenye vitamin ukosefu unaweza kuwa ni B12 na folate kuwa si wa kutosha au unaweza ukawa na poor B12 absorption kama ulifanyiwa upasuaji wa kuondoa kipande katika tumbo au utumbo,minyoo au ugonjwa wa Crohn's na maambukizi ya HIV.

Katika bone marrow kunaweza kukawa na tatizo litakalopelekea rbc kuzalishwa kwa kiasi kidogo....na kama stem cell katika uroto wa mifupa ni kidogo,unamatatizo au umekuwa replaced na cell nyingine kama metastatic cancer cell hapo anemia itatokea.Sasa matatizo ktk uroto wa mifupa au stem cell unaleta anemia zifuatazo:

1:Aplastic anemia,ambayo hutokea kunapokuwepo na upungufu wa idadi za stem cell au kutokuwepo kabisa na inaweza kurithiwa.Hili tatizo linaweza kutokea kutokana na kujeruhiwa kwa uroto wa mifupa,radiation,chemotherapy au infection.

2:Thalassemia ambayo nimeshaielezea juu kabisa ambayo hutokana na rbc haiwezi kukomaa na kukua vyema.

Kama ulikuwa au unafanya kazi ambazo madini ya lead unayashika mara kwa mara ujue uwezekano wa tatizo la uroto wa mifupa kukukumba upo.

Pia magonjwa kama ya figo,hypothyroidism,saratani,maambukizi,rheumatoid arthritis,lupus na kisukari zinaweza kukuletea matatizo ya anemia.

Nafikiri kwa kifupi nimekupa mwangakuwa anemia inaweza kuwa katika ma-group hayo so ni wewe kuangalia hapo tatizo lako linaweza kuwa wapi na nimeelezea kwa kirefu kidogo hiyo Thal kwa kuhisi tu kuwa inaweza kuwa chanzo cha tatizo lako.
 
hv na typhoid ikiwa 320,inaweza kusababisha upungufu wa damu?
 
Typhoid kama imefikia hatua mbaya utaona damu kwenye choo,na sidhani kuwa hiyo ni typhoid inayopelekea hilo tatizo kwani nafikiri kwa hatua hiyo hata kuingia hapa jf tu usingeweza
 
jaman natumain mu wazima.

mi ni bint ,nna tatizo la kupungua damu tangu mwez wa kwanza.nikitumia vyakula au dawa inapanda hata had 13,lakn nikiacha baada ya wiki kama tatu naikuta 9,,.nimepima vipimo ving kama full blood picture,vidonda vya tumbo ,minyoo,kote naambiwa niko normal cna tatizo.kiukweli nachanganyikiwa sana cjui cha kufanya.mwezin naenda kama kawaida cna tatizo lolote.
madokta na watu wengine wenye ujuz mbalimbali naomba mnisaidie nateseka sana.

Hata mie niliwahi kutokewa na ilo tatizo LA kupungua damu , ndani ya miezi miwili niliongezewa chupa Tisa, lakin niliwahi kupata uxhauri kwamba nikajaribu kutumia kinywaji kiitwacho ribena. Kinyaji hiki hakika kwa aslimia 75 kinaongeza damu mwilini. Mm tatizo hili lilinikumba wakati na umri wa miaka 14, wew unaumri gani saiv
 
25,tatzo lako lilidum mda gan
 
25,tatzo lako lilidum mda gan

Tatizo langu lilianza mwaka 2001 na likadumu miezi miwili hapa niliongezewa damu chupa 9:kixha likapitea , na lilijirudia mwaka 2006_ mwezi wa 12 likajirudia na hapa niliongezwa damu chupa 4_ ndipo wakaniambia tatzo langu litaixha nikifikixha miaka 15_ Namuxhukuru mungu mpaka saiv mm n mzima wa afyaa kabisaa...jitahidi kumxhirikixha mungu katka hili atakuxaidia ndg
 
mungu namshirikisha ndug na naamin atanisaidia.
 
Jirani yangu nae alipata tatizo hilo sina uhakika na umri wake lakini alikuwa na umri wa kati ya miaka 14-16 ameongezewa damu sana hospitalini baadae walezi walimpeleka kule ukerewe na akaanza kutumia dawa za kienyeji tangu januar hadi leo hii tatizo hilo limeisha kabisa
 
typhof 320..!? wap huko umeambiwa....ni imposble kujua idadi ya salmonella spp..walio mwlin..kwan typhd maranyng huwa 2na ipika kwenye serology( agultnation) ivyo ni ngmu kujua idadi....nirud kwenye swal typhod aiwz sababisha ANEMIA(upngfu wa damu) bal huwa ina leta complication kama sepcaemia,pneumonia(nemonia) pia tatzo lako la HB kuwa below normal range ambyo ni 12.6-15g/dl kwa mwanamke...nawz kuku shauri uka fanyiwe sickling test..yaweza kuwa reason bhnd.
 
Back
Top Bottom